Kufanya biashara kunafikirisha sana hasa ukiwa na mtaji mdogo unahitaji uwe na back-up usogee

Uaminifu ndo silaha ya mafanikio..bahati mbaya wabongo uaminifu hatuna na ni ngumu tajiri kukuamini ndo mana wanasemaga matajiri wana roho mbaya kwa watu wanaojitafuta ila ni kwasababu kuna sehem walipigwa kwa watu waliokosa uaminifu wakawa wabinafsi.. unampa mtu mzigo kwa mali kauli anauza hakupi pesa anakimbia au anakulipa kwa kuchelewa mno ili hali ashauza.
 
Ningependa kutia neno hapo. Yote hayo ni ukweli kabisa..Ila naomba nitoe mfano hapa..moja ya biashara yangu ni maziwa...mtaji wangu kusema ukweli ni milioni +,japo hapo mwanzo ulikuwa mdogo sana...kutokana na kuaminika na kudumu kwenye biashara kwa muda mrefu naletewa maziwa na wakulima tena sio kwa kubembeleza..mwanzo nilikuwa nanunua Lita kumi Hadi kumi na Tano. Ila biashara ilianza kukaa sawa nikawa naagiza Lita ishirini ndipo boss mwenye ng'ombe wake aliponiona mm nimteja wake potential na akaanza kunipa maziwa hata kama sinapesa anaamini nitamlipa.baada ya mwezi tulikaa chini tukaweka makubaliano..Mana hata kipindi maziwa ni adimu atatafuta kwa wakulima wengine ili tu nisikose mzigo..sasa imefika hatua napokea mpaka Lita sitini..Mana naanza kuuza jumla kwa wengine wanaofanya biashara..hivyo hiyo m6 ni nyingi sana Ila Anza chini.. biashara ni chain
 
Lengo la biashara ni mauzo.. supplier au manufacturer yeye anachotaka ni bidhas zake ziuzike..kama wewe mfanyabiashara utakuwa na wateja wa uhakika na cash flow nzuri..hata mtaji wako uwe mdogo kiasi gani..jua kuwa lazma uzingatiwe.. biashara ni uwakala.
 
Dah yan nmepata hasira huu uzi member wawili wanasema walianza na mtaji wa Mil 1, hv ni kismati au nishafanya zaidi ya biashara 5 za mtaji wa zaidi ya huo holaa hadi naogopa biashara! ajira nayo miyeyusho kweli. Mtu hupigi hatua
 
Unampa mtu hela ndio anaona shida zake ni kubwa kuliko zako.
Mil 6 uliyonayo ni kubwa sana kama hautajilinganisha na mtu.
Wewe nunua kwa hao wenye mtaji wa kati na uza, faida irudishe kwenye mzunguko na ndani ya miaka mitano utaingia kwenye system na wao wakuunganishe na matajiri.
Maisha ni mipango na sio shortcut.
 
ukiifananisha ukurasa wako wa kwanza kwenye biashara na mwingine aliyeko ukursa wa katikakati utakata tamaa. Anza hayo mengine yatajipa huko mbele
 
K
Dah yan nmepata hasira huu uzi member wawili wanasema walianza na mtaji wa Mil 1, hv ni kismati au nishafanya zaidi ya biashara 5 za mtaji wa zaidi ya huo holaa hadi naogopa biashara! ajira nayo miyeyusho kweli. Mtu hupigi hatua
una kitu hukufanya kwa usahihi
 
Dah yan nmepata hasira huu uzi member wawili wanasema walianza na mtaji wa Mil 1, hv ni kismati au nishafanya zaidi ya biashara 5 za mtaji wa zaidi ya huo holaa hadi naogopa biashara! ajira nayo miyeyusho kweli. Mtu hupigi hatua
Ndugu yangu kila kitu ni mikakati asikwambie mtu, Fanya tafiti sahihi katika hizo biashara unazofanya mfano wateja wako wanahitaji nin? Na maboresha pamoja unbunifu wa hapa na pale, Bila kusahau uaminifu kwa wateja wako na kwa wale utakaochukua mizigo ya jumla kwao!...
..
 
Nashkuru Mkuu, 100% 🤝
 
BUSINESS BENEFITS MORE THAN EMPLOYMENTS DO/ BIASHARA INA FAIDA ZAIDI YA AJIRA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…