Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Nimefanya biashara kwa miaka kadhaa. Nimefanya na watu mbali mbali wake kwa waume, ninaowajua kwa sura na wengine kwa mawasiliano pekee. Nimefanya na wa masafa ya mbali na majirani pia.
Kati ya biashara zote hizo biashara niliyoona ni ya kipekee sana na zile nilizofanya na wake zangu. Kumbuka mimi nina wake watatu kwa sasa. Mmoja kati yao anajishughulisha na mambo ya kupika na kulea watoto tu. Wawili ndio nafanya biashara nao.
Mimi ndiye niliyewafungulia biashara na kuwaingizia bidhaa. Siku wakitaka kutumia kitu kwenye biashara zao lazima waniombe pesa ili wajinunulie wanachokitaka au kuwanunulia ndugu zao. Nikisema siku hiyo sina pesa basi huwa wanachukua na wananiandikia hesabu. Deni hilo huwa nakumbushwa mpaka nitalilipa japo kwa kuchelewa. Hata mara nyengine wakisahau kuwa nimeshawalipa mimi huwa nalipa tena.
Kitu ambacho nimegundua ni cha ajabu sana. Kwani wake zangu wote hao wawili ni wakarimu zaidi kwangu. Binafsi mimi mtu akinidai dai huko mitaani kwa namna kama hizi mara narushiana naye mangumi. Kwa hawa wake zangu huwa sina maneno kabisa. Kwa upande wao nimegundua ni wakali na hawachukui pesa kwa mtu mwengine.
Wenye wake na ambao hawajaoa chukueni mafunzo hapo. Na wanawake ambao hawajaolewa tafuteni wanaume wa kuwaoa ili mpata raha za ndoa kama za wanawake wenzenu hao.