Pre GE2025 Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa! Sheria ya Uchaguzi ni kosa. Kwanini tunarudia kosa? Haki si hisani, ni stahiki. Bunge tutendeeni haki!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tuna muda mrefu sana tukiwa hatutekelezi Sheria ipasavyo, na kuitii katiba kwa usahihi.
ni kweli kwasababu wanaopaswa kuijua katiba, hawaijui!. Ndio hawa wanaotutungia miswada yenye sheria batili!. Bunge la magoigoi linapitisha sheria batili kuwa sheria!. Mahakama Kuu inaitangaza ni batili na inaitengua, serikali yetu ikakata rufaa!, inashindwa!, inapeleka Bungeni muswada wa mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura na kuuchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu kiubatili!. Mahakama Kuu inatangaza, mabadiliko hayo ya katiba ni batili, Mahakama ya Rufani inarudisha Bungeni ndio liuondoe ubatili huo ambao upo mpaka Leo!.
Kwa sasa utashi wa rais ndio katiba na Sheria.
Ni kweli!.
Nakuhakikishia hakutakuwa na mabadiliko ya kweli iwapo kifungu kinachomkinga rais kutoshitakiwa akiwa madarakani au ametoka kitaendelea kuwepo.
Ni kweli...
Hiyo Kinga kwa rais ndio sababu ya udhaifu wa mifumo yote ya kisheria, na taasisi zote zinazosimamia utawala hapa nchini.
Naunga mkono hoja
Hiki ufanyacho hapa ni kufurahisha genge tu, kama rais hayuko tayari kubadili chochote kwenye katiba itakuwa ni porojo as usual.
it's true, take it from me, hata hiyo furahisha genge, ikijirudia rudia, hatimaye genge linafurahi!, genge ndio wenye nchi, wenye katiba, ndio wenye sheria, hao walioko madarakani ni watumishi wao, wao ndio waajiri wao, wanaowalipa mishahara tax free, hivyo genge wakifurahi, wanawafuta kazi!.
P
 
Shida wanaozitunga hizo sheria wanafikiria wataendelea kubaki na nafasi walizo nazo leo. Kwa maneno mengine, wanatunga sheria zinazowapendelea wao na familia zao.
Basi siku moja sheria hizo hizo ndo zitawahukumu wao, nakuhakikishia 100%, unamkumbuka kiongozi flani wa Laiberia?!
 
Asante kuchangia, please edit to save JF space . Pia nimewaomba modes wafanye the needful

P
 
Sawa sawa Kaka paul hiyo Avater na wewe halisi havifanani.
 
Duh...!.
P
 
Lakini je wanasikia! Viongozi wanaopatikana chini ya sheria batili na wso ni Batili?
Sheria ya uchaguzi iliyopo inayokwenda kubadilishwa, ina makosa fulani ya kikatiba, na kisheria, yaliyopelekea sheria hiyo kuwa na ubatili Fulani. Hili nimelizungumza sana humu!.
 
Hivi vyote vimechagizwa na kupenda Starehe ya uzinzi, pombe na uvivu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…