Kufanya kura za maoni mtandaoni kwa kulinganisha wanaosemwa kugombea URAIS nchini Tanzania ni makosa?

Kufanya kura za maoni mtandaoni kwa kulinganisha wanaosemwa kugombea URAIS nchini Tanzania ni makosa?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
Team;
Salaam!

Sheria ya mitandao ya kijamii na Sheria zingine zinasemaje kuhusu kura za maoni kwa wamaotajwa kugombea URAIS mwaka 2025?

Kama itakuwa kitu kinachoruhusiwa kufanyika basi ningeomba
  • Hashim Rungwe Spunda;
  • Zitto Zuberi Kabwe
  • Tundu Antipas Lissu
  • Dkt Samia Suluhu Hassan
  • Ibrahim Haruna Lipumba

Tuone nani kati yao atapigiwa kura nyingi za ndiyo.


Kidumu CCM!
 
Team;
Salaam!

Sheria ya mitandao ya kijamii na Sheria zingine zinasemaje kuhusu kura za maoni kwa wamaotajwa kugombea URAIS mwaka 2025?

Kama itakuwa kitu kinachoruhusiwa kufanyika basi ningeomba
  • Hashim Rungwe Spunda;
  • Zitto Zuberi Kabwe
  • Tundu Antipas Lissu
  • Dkt Samia Suluhu Hassan
  • Ibrahim Haruna Lipumba

Tuone nani kati yao atapigiwa kura nyingi za ndiyo.


Kidumu CCM!
Wengine hao wametangazwa lini na Vyama vyao?
 
Hapana, haitakua kosa kwa muktadha wa Takwimu zisizo Rasmi na kama utafuata Sheria ya Takwimu, Sura ya 351 ya 2019 na kuzingatia viwango vya kimataifa, kitaifa, katika kukusanya na kusambaza taarifa za takwimu.

Sheria ya Takwimu ya mwaka 2019 chini ya Kifungu cha 26(1) inampa kila mtu haki ya kukusanya na kusambaza taarifa za takwimu .

Aidha, unatakiwa kufuata misingi, maadili ya kitaaluma na kanuni za kisayansi katika ukusanyaji, uchakataji, uhifadhi na uwasilishaji wa taarifa/data hizo kwa kuhakikisha ni za ukweli na usawa. Hii ni ili kuhakikisha kuwa takwimu zinatumika kwa maendeleo ya taifa bila kuathiri usahihi, faragha, na maadili ya kitaaluma.

Ikumbukwe kuwa takwimu zinazoweza kukusanywa na mtu yeyote ni takwimu zisizo rasmi. Kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu ukusanyaji na usambazaji wa takwimu rasmi nchini unasimamiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Taasisi na idara mbalimbali za serikali zinaweza kukusanya na kuchakata takwimu kwa ajili ya shughuli zao maalum. Hata hivyo, takwimu hizo zinapaswa kuratibiwa na NBS.

Mashirika yasiyo ya kiserikali pia yanaweza kufanya tafiti na ukusanyaji wa takwimu, lakini takwimu hizo lazima zipitie mchakato wa uthibitisho wa NBS kabla ya kutumika kama takwimu rasmi.

Kushindwa kuzingatia sheria kunaweza kusababisha adhabu kama vile faini au hatua nyingine za kisheria.
 
Back
Top Bottom