Kufanya Mambo Yanayolipinga Jina La Yesu Kunaweza Kukupelekea Ukawa Mtumishi Wake

Kufanya Mambo Yanayolipinga Jina La Yesu Kunaweza Kukupelekea Ukawa Mtumishi Wake

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Matendo 26:9 NEN
[9] “Mimi pia nilikuwa nimeshawishika kwamba imenipasa kufanya yote yale yaliyowezekana kupinga Jina la Yesu wa Nazareti.

Wapingaji wa uwepo wa Mungu ni wengi, wanaolikataa jina la Yesu ni wengi, wanaopinga Injili ya kweli ni wengi, wanaokataa kumwamini Yesu ni wengi.

Mtume Paulo ni mmoja wao, alikuwa mpingaji/mpinzani mkuu wa wale wote waliokuwa wanahubiri jina la Yesu, alitesa na kuua wale wote waliokuwa wanamhubiri Yesu Kristo.

Saa ilipofika ya yeye kukamatwa na Yesu na kumfanya kuwa mtume wake, naye alikutana na upinzani uleule aliokuwa anaweletea wengine.

Mdo 26:14 SUV
[14] Tukaanguka nchi sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi? Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo.

Inatufundisha kwamba wanaopinga Injili na uweza wa Yesu, na wengine kukataa uwepo wa Mungu, hawajaanza leo, walikuwepo akina Farisayo Sauli ambaye baadaye akawa mtume Paulo.

Wao walikuwa hawazuii Injili kwa mdomo tu, walikuwa wanakamata kisha kutesa na kuua watumishi wa Mungu waliokuwa wanaeneza habari za Yesu.

Kuua kwa Sauli na wenzake, haikuzuia Injili kuendelea kuhubiriwa, ikafika wakati Mungu mwenyewe akaamua kumgeuza Sauli ambaye ni mpinzani mkubwa wa Injili, na tunaona Paulo akigeuzwa na kuwa mtume wa Mungu.

Mdo 26:16-17 SUV
[16] Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako; [17] nikikuokoa na watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao.

Mungu anaweza kumgeuza yule anayemtaka, bila kujalisha mtu huyo anamkataa na kumpiga, kwa kuwa amemuumba Yeye, anaweza kumbadilisha mawazo yake akamgeukia Yeye.

Chombo cha Mungu kinaweza kikawa kinatumiwa na Shetani kupinga kazi za Mungu, ila muda ukifika wa kuondolewa kwenye utumwa itakuwa hivyo siku moja.

Watu wanaomkataa Yesu na kupinga kazi zake wasikuondoe kwenye kusudi la Mungu, walianza siku nyingi ila hawakuweza kuzuia Sauli kushughulikiwa na Yesu.

Upinzani mkali wa kuzuia watu wasiokoke hauwezi kuondoa uwepo wa Mungu kuwatumia wote wanaotangaza habari za Yesu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Amen... ndugu zetu
Atheist! Nawaona kama Paulo alivyokuwa msomi na ambaye hata petro, alikiri kuna baadhi ya mambo kuyaelewa ni vigumu!!!
be blessed mkuu!
Cc. Yoda
 
Back
Top Bottom