Kufanya mapenzi kwa wanandoa kwa wiki mara 3 kunapunguza kupata shambulio la Moyo!

Kufanya mapenzi kwa wanandoa kwa wiki mara 3 kunapunguza kupata shambulio la Moyo!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KUFANYA MAPENZI KWA WANA NDOA KWA WIKI MARA 3 KUNAPUNGUZA KUPATA SHAMBULIO LA MOYO (HEART ATTACK) KWA ASILIMIA 50% WANA SAYANSI WAMESEMA.


heart_disease_s1_heart.jpg


heart_disease_s7_cardiac_arrest.jpg


stock-photo-sexy-young-couple-kissing-and-playing-in-bed-115994308.jpg


Utafiti umebainisha kwamba kufanya mapenzi angalau mara tatu kwa wiki kunapunguza uwezekano wa kupatwa Heart Attack (Shambulio la Moyo) kwa 50% ukilinganishwa na yule ambaye anapitisha wiki nzima bila kupiga mambo yetu. Pia utafiti huo unasisitiza ya kwamba mwenye Kufanya Mapenzi killa siku anaondoa uwezekano wa kupata Heart Attack kwa Asilimia 100%


ZIJUE FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI

Kiafya

Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu
atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.

Tendo la ndoa
huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu

Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi
ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji. Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

Hupunguza mafuta yenye kileo
(Cholesterol)
Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa
mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

Kupunguza maumivu

Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.

Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)
Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara.

Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa
huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

Kupunguza mfadhaiko wa moyo

Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Huongeza uzalishaji wa homoni za
kiume(testosterone) na za kike (Oestogen)
Faida nyingine inayopatika
ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

Kuishi muda mrefu
huku ukionekana kijana
Wakati wa
tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka.

Kutokana na elimu hiyo DHEA ni
kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

Hupunguza baridi na mafua

Elimu inaonesha kuwa wanaofanya
tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Hizo ni faida chache tu za kufanya
tendo la ndoa.

NB: Jambo kubwa la kuzingatia ni
kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa

HAYA KWA WANA NDOA FANYENI MAPENZI JAPO KWA WIK MARA 3 MUPATE FAIDA ZA TENDO LA MAPENZI NDANI YA NDOA. KWA WALE WASIOWA HAWAPATI HIZI FAIDA SHAURI YENU MSIE OWA OWENI MUPATE FAIDA ZA TENDO LA NDOA.
 
mimi49 njoo huku.......
Umesikia Kaizer itabidi uongeze idadi ya siku kwa wale wake zako!!Ni kweli alosema MziziMkavu...Heart attack inatokea pale moyo unaposhindwa kusukuma damu ya kutosha kwenda sehemu tofauti za mwili...na hii inaweza kusaabishwa na atheoschleorosis( mafuta kwenye mishipa ya damu ya moyo) au weakness kwenye muscle ya moyo hatimae moyo kushindwa kuwajibika ipasavyo n.k Tendo la ndoa ni mojawapo ya mazoezi inavyofafanua hio research na mazoezi ni mazuri kupunguza mafuta!! Hii article ipo more based for healthy normal people..ila siwezi kusema ni garantee 100% coz kama mtu ni kibonge nyanya inabidi akimbie mchakamchaka gym..
 
Umesikia Kaizer itabidi uongeze idadi ya siku kwa wale wake zako!!Ni kweli alosema MziziMkavu...Heart attack inatokea pale moyo unaposhindwa kusukuma damu ya kutosha kwenda sehemu tofauti za mwili...na hii inaweza kusaabishwa na atheoschleorosis( mafuta kwenye mishipa ya damu ya moyo) au weakness kwenye muscle ya moyo hatimae moyo kushindwa kuwajibika ipasavyo n.k Tendo la ndoa ni mojawapo ya mazoezi inavyofafanua hio research na mazoezi ni mazuri kupunguza mafuta!! Hii article ipo more based for healthy normal people..ila siwezi kusema ni garantii 100% coz kama mtu ni kibonge nyanya inabidi akimbie mchakamchaka gym..

LOL...hivi unawafahamu wako wangapi mimi49? Ww unadhani siri ya kuperfom ni nini lol asante kwa ufafanuzi, mi nadhani appointment yangu iko pale pale
 
Last edited by a moderator:
Mdona mara tatu kwa wiki ni ndogo sana au hii inawahusu wale ambao ni wagonjwa
 
sivuti tena kwani madhara yake makubwa kuliko faida yake tena nakuomba usijaribu kuvuta unaweza kupata matatizo ya kusahausahu na kuvunjika moyo haraka katika mbio za maisha, kukosa umakini na kushindwa na uamuzi wa haraka
Kwa kulinda afya yako arudia tena kuvuta
 
Heeee! Mara 3 kwa wiki? japo utafiti haujaelezea hizo mara 3 au kila siku ni za aina gani. Kuna wengine akipiga 1 inafidia mwezi mmoja. Sasa hii mara 3 kwa wiki au kila siku si atakufa mtu kama alivyosema kahtaan?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom