Baadhi ya wadau wa sheria wamekiri kuwa kosa la kufanya mapenzi na mwanafunzi halipo kisheria bali neno kubaka ndilo linalotambulika.
Wameyasema hayo baada ya hukumu ya hivi karibuni ya MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Bukoba kuamua kuwa kufanya mapenzi na mwanafunzi siyo kosa kisheria.
Hukumu hiyo ilitolewa Oktoba mwaka huu na Jaji Gabriel Malata baada ya mshtakiwa Thadeo Pastory kuhukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera kwenda jela miaka 10 kwa kosa la kufanya mapenzi na mwanafunzi na ndipo akaenda kukata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba.
Mbona kuna mwanasheria mmoja alisema kujamiiana na mwanafunzi siyo kosa. Sasa iweje kujamiiana na mwanafunzi niliyekubaliana naye kugeuzwe kuwa ni kubaka?