Mimi nakimbia huu mwaka wa 5 mfululizo. Mazoezi ya kukimbia barabarani (Road runner's) yapo dunia nzima watu wanakimbia. Ili kuimarisha usalama wako UCHAGUZI wa route ya kukimbilia ni muhimu sana, umakini barabarani, nguo na vifaa vya kukimbilia ni vitu vya kuzingatia sana na kumuomba Mungu.
Barabara nyingi kubwa kwa mfano kutoka Tegeta hadi posta mjini etc zina space iliyojitenga mbali kabisa na main road kwa waenda kwa miguu tumia hizo space vizuri..pia kuna barabara nyingine zina mstari unaotenganisha eneo la waenda kwa miguu hizi uwe nazo makini hasa uyaface magari upande yanapotoka ( keep right). Pia pendelea barabara ambazo hazina movement sana ya magari..hapo utakuwa safe sana.Zingatia sheria za barabarani kwa kuvuka kwenye zebra etc.
Kama unapenda kuvaa
headphones,vaa ambazo zitakufanya usikie kila kinachoendelea around.
Always focus mbele kuangalia kinachoendelea usipende kukimbia unaangalia chini.
Usipende kukimbia speed kali,hiyo speed kali nenda uwanjani
Pendelea kuvaa nguo za rangi rangi kama njano, ,orange ,nyeupe, pink, red etc au usiku zenye reflector au taa kabisa ili uweze kuonekana vizuri.
Hili la kusema kukimbia barabarani na utavuta harufu ya moshi na utakuathiri ni propaganda za madaktari.ziko kufikirika zaidi kuliko ukweli
Kikubwa muombe Mungu akupe ulinzi kama vile unavotaka kwenda kwenye shughuli zako unavoomba
Faida za mazoezi ya kukimbia ni nyingi sana ..inatibu magonjwa yote ya mtindo wa maisha, inasaidia kukata weight ,inakupa relaxation of body and mind (afya ya akili) , inaimarisha ulinzi wa mwili , nguvu za kiume inarejesha , magonjwa yote ya mfumo wa kike Tiba ni kukimbia, inakufanya uonekane kijana na mtu imara na nadhifu, magonjwa yote haya madogo madogo ya homa , mmengenyo wa chakula etc utayasikia tu kwa wengine, inasaidia kikubwa pia inasafisha damu kwa kuondoka sumu kwenye damu etc..inaimarisha mifupa na misuli, .Faida za mazoezi ya kukimbia ziko nyingi sanaaaa..naona wabongo wengi wanakimbia kupunguza vitambi tu.
USIOGOPE KUKIMBIA BARABARANI
"WE KIMBIA TU"