Kufanya meditation bongo ni kazi mno! ile unafunga macho tu mawazo ya ada ya mtoto, ukijirudi kidogo mara inakuja harufu ya chemba imecheua kwa jirani

Kufanya meditation bongo ni kazi mno! ile unafunga macho tu mawazo ya ada ya mtoto, ukijirudi kidogo mara inakuja harufu ya chemba imecheua kwa jirani

Kwanza sijajua unafanya aina ipi ya Meditation, Aina kuu mbili kwa begginers ni Meditation ya Pumzi na Meditation ya Mantra[Kurudia rudia maneno].

Wewe unajaribu kufanya ipi?
mtu kaangalia YouTube tutorial, anafanya meditation zote kwa kuzichanganya. Kingine watu wana haraka ya kuona matokeo ambayo wanasisimuliwa nayo kupitia talks za watu tofauti
 
Duh!..tiba ya nini hii ?
Ninge kupa majibu yangu binafsi, unge ona jau.
Ila hii hapa evidence
Screenshot_20250123-130956_1.jpg
 
Tuambie muujiz gani ulishawah kupata as the result of medtn na manfstn??
Meditation haileti miujiza mkuu, ila inakutengeneza wewe halisi na kukuwezesha kuswitch upande kati ya pande mbili za asili ambazo mtu ako nazo huku ikikuweka imara zaidi kwenye upande huu unaonekana.

Na meditation iko na hatua kadha wa kadha ila hatua ya mwisho kabisa matokeo yake ni kama kujiroot kwa maana ya kujipa uwezo wa ziada ambao ilikuwepo ndani yako ila ulijificha na katika hatua hii ndio huwa watu husema mtu amefungua jicho lake la tatu.

Hapa ndio mtu huanza kuona mambo ambayo hayaonwi kwa macho ya kawaida ila pia huwa anakua yuko wazi na anaact kama sumaku.

Na kutokana na hali hiyo basi mtu anaweza kugeuka kuwa hekalu la nguvu zilizo nje ya uwezo wa kibinadamu bila kujali upande kwa maana wa Nuru au wa giza na ndio hapa wengi hujikuta wanachanganyikiwa na kuanza kufanya mambo tofauti na watu wengine (nadhani hatua hii ndio watu husema hatua ya miujiza ila kiuhalisia si miujiza kwasababu miujiza au muujiza ni jambo jipya ambalo halipo na halitarajiwi kuwepo ila limelazimishwa katika hali isiyo ya kawaida na kufanywa liwepo, ila hayo yote ya kwenye meditation ni mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa Kila mwanadamu).
 
Nitaanza kuongea mwenyewe na mimi (ila sio hadharani nisionekana 'chizi').
hahaha, uki ongea hadharani lazima wakufunge kamba.
Ila self talk Ina saidia Sana, sometimes kukiri au kuyakubali matatizo yako.

hii waweza sema kuungama mambo yako, ila hapa una kuwa mwenyewe.
Learned this nilipo kuwa miaka 14
 
Hii kitu kwangu imekuwa ngumu sana hadi pale nilipoanza kujifanyisha vijimazoezi vya martial art, sasa kuna ile kanuni ukichemka unakuwa unajipa pozi kwa kuingiza pumzi na kuitoa kwa mtindo wa kumeditate angalau hapo sasa nikajikuta naimaster kidogo. Meditation ina nguvu ajabu asikwambie mtu; mfano kwenye yale mazoezi nilikuwa nikirusha ngumi kutokea ndani(kwa kumeditate) aisee inakuwa na power ajabu.
 
Kwani wenzetu wanaofanya Taamuli huko kwa wenzetu wao hawana majukumu ya ada za watoto
 
Kwani wenzetu wanaofanya Taamuli huko kwa wenzetu wao hawana majukumu ya ada za watoto
Hahahah

Ndugu, unajua tabu za mwafrika wewe😂😂😂

Sasa mtu analala ndani na vyombo vya kupikia ajaosha siku mbili unategemea nini
 
Back
Top Bottom