msaragambo
Senior Member
- Aug 6, 2008
- 127
- 17
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ys mwenzetu Makubo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Awali - kuna habari kuwa mwandishi wa habari wa Tarime ambaye amehusika sana kwenye kutoa habari za uchafuzi wa mazingira uliofanywa na kampuni za madini tarime amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo (moyo umepasuka).
Update:
Kuna taarifa nilizopata muda mfupi uliopita kuwa familia ya marehemu Makubo inahisi kuwa kuna mkono wa mtu umehusika kwenye kifo cha ghafla na cha mazingira ya kutatanisha cha ndugu yao.
Inasemekana kuwa mazishi hayatafanyika mpaka uchunguzi maalumu ufanyike kuhusu kifo cha Makubo.
Zaidi ya yote - RIP Haruni Makubo.
Watu wa Tarime na watanzania wamepoteza mtu muhimu sana kwenye vita ya kutafuta haki dhidi ya kampuni kubwa la madini.
Ni kweli, hakuna mzaha pale maisha ya mtu yanapopoteaHILI NI JAMBO LA MUHIMU KABISA SI MZAHA TENA
Mwenyezi Mungu atawapa subira familia ya marehemu.
Lakini kwa kawaida huwa tunasema msiba usiwe na maeno maneno, lakini kwa kweli huo utamaduni utatufikisha pabaya huko tuendako. Pamoja na imani kutuambia kwamba kila nafsi itaonya mauti, bado tusikubali kila kitu kipite tu hivi hivi. Lazima tuangalie mapana.
Kwa taarifa rasmi ni kwamba:
-Makubo alikuwa mmoja wa waandishi waliohusika na waliokuwa wakiendelea kuchunguza athari za kemikali mgodini Tarime
-Makubo alikwisha kupata ruzuku ya fedha kutoka Tanzania Media Fund (TMF) kwa ajili ya kufanikisha uchunguzi zaidi kuhusiana na athari hizo na alikuwa ndio kwanza ameanza
Kutokana na hayo, si busara hata kidogo kufungwa midomo kujadili mazingira ya kifo na tahadhari kwa wengine. HILI NI JAMBO LA MUHIMU KABISA SI MZAHA TENA