Kufaulu mitihani vizuri sio ‘kipaji maalumu’


Mkuu KUSOMEA KATIKA MAZINGIRA MZURI, WALIMU WAZURI NA VIFAA VYA KUJIFUNZIA VYA KUTOSHA na UKAFAULU VIZURI sio kipaji maalum!!!!!!! Kama wana vipaji maalum basi wangejifundisha wenyewe bila walimu ndipo tungepambanua vizuri vipaji vyao. Mtu hawezi kusoma St Marian akapata divisheni ONE na mwingine akasomea shule kama hii hapa akapata divisheni 4 halafu ukasema eti yule wa Marian ana kipaji maalumu kumzidi huyu aliyesomea vichakani.

Haiwezekani hata kidogo na hakuna ulinganisho wa namna hiyo mahali popote pale. Inachokifanya serikali ya CCM ni kujaribu kufukia kichwa mchangani kama mbuni huku akidhani mwili mzima hauonekani!!!!1
 
Kuna wengne wanaiba lakin hawewez hata pata hyo div One,,so waache wenye bahati zao wasifiwe mkuuu acha roho mbaya


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 

Watu mnadhaniaga kuwa special school huwa zinakuwa na upendeleo wa waalimu. Hapo mnajidanganya sana. Hizi shule zina waalimu wa kawaida sana. Ila juhudi za wanafunzi zinawapa sifa waalimu, ungekuwa umepitia hata moja kati ya hizo shule ungeelewa.

Mitaala ya Tanzania haina shule za michezo, so wewe ulitaka wanafunzi wanaofikiria vyema wapimwe vipi tofauti na hii njia ya kufaulu vyema.?. Na isitoshe zile sio shule za michezo, wala za sanaa. Zile ni shule za elimu ya kawaida/darasani so ni lazima watu wapimwe uelewa na umaalumu wao katika kile wanachofundishwa. Hata havard, MIT, Oxford na top dogs wote katika elimu wanatumia njia hii kutambua vipaji. You can not be there pasipo kufaulu vyema na kutokea hapo kipaji kilicho ndani yako kitasimamiwa vyema. Hapa TZ hakuna system nzuri ya usimamizi wa watu hawa. Na hakuna plan endelevu juu ya hawa watu.

Usitake kulaumu tuu. Kwa hiyo unataka kusema kuwa wanaosoma hizo shule wanapendelewa au ni aje.? Na kwa upande mwingine unazungumziaje tanzania ones.? Jee ni kipaji ama nini.?

Unazungumzia kuiba pepa na kufaulu. Kwa taarifa yako huwezi kusustain mazingira ya zile shule ikiwa umeiba pepa, lazima nature itakukataa tuu. Na watu wengi wanaaminishwa kuwa hizo shule wanaiba paper. Hakuna kitu kama hiko. Tuwe wakweli tuu, wale kusoma hapo ni wanastahili na efforts zao ndio zimewaweka hapo.

Wengine mnasingizia wanasoma sana, hivi kwa akili yako unataka upate vipi taarifa pasipo kusoma ama kufundishwa kwa usahihi na ukaelewa.?
 

mkuu naomba maana ya "shule ya vipaji maalumu"?? je tanzania zipo? na kama zipo hawa wanaosoma huko wanakipaji gani maalumu?
 
mkuu naomba maana ya "shule ya vipaji maalumu"?? je tanzania zipo? na kama zipo hawa wanaosoma huko wanakipaji gani maalumu?

Inategemea unazungumzia kipaji gani, maana vipaji/vipawa viko vya aina nyingi. Hapa kinachozungumziwa ni kipaji katika elimu, kwa maana ya kusoma, kuelewa na kukumbuka ulichokisoma. (Ama hufahamu kama kusoma nako na kuelewa ni karama.?)

Katika nyanja hii ndio utakuta Ilboru, Mzumbe & Co as specified na standards zilizowekwa miaka hiyo ya nyuma.
 
Mademu wazuri wana akili Sana ILA wanazingatia Sana urembo wao kuliko akili zao
 
»Kusoma Kuelewa kukesha mbwembe
»Watoto wenye vipaji maalumu kipekee kiakili
»Kama hausomi lazima utafeli ndio maana watu wanapiga hadi pointi 8(olevo) meta na wengine wanapiga four ilboru
»Kufaulu ni jitihada binafsi na si shule
 

hapo kama hajaelewa ana lake jambo
 
Uwepo wa shule na vyuo vya kata na bodi ya mikopo kumefanya kila mtu ajione msomi!!

Hizi dharau zimekuja baada ya utitiri wa degree na PHD za kina Nape!
 
Kuna wengne wanaiba lakin hawewez hata pata hyo div One,,so waache wenye bahati zao wasifiwe mkuuu acha roho mbaya


Sent from my iPhone using JamiiForums.����

Unamaanisha kwamba wezi wote hawapati divisheni ONE ama? Je, mtoto aliyesomea chini ya mwembe akapata divisheni THREE na mwingine aliyesomea Tusiime akapata divisheni ONE ni nani mwenye KIPAJI MAALUM kati ya hawa wawili?
 

Bold: Hakuna mtu anayesema hivyo hapa. Hayo unayasema wewe.

Red: wewe unadhani kwamba kipaji cha michezo ndicho kipaji pekee walichokuwa nacho wanafunzi wa Tanzania? Vipi kuhusu sanaa ya uchoraji, maigizo, ugunduzi wa kisayansi, useremara, ufundi mchundo, nk? Rudia kusoma mada yangu ili ikusadie kutafakari vizuri pointi hii. Kwenye mada nimeweka mifano ya wagunduzi wa kitanzania wenye vipaji ambao kama wangeendelezwa tungekuwa mbali sana katika mapinduzi ya kisayansi.

Blue: Kipaji cha mtoto hakigunduliwi afikapo sekondari (kama serikari inavyotupaka mafuta kwa mgongo wa chupa). Hii dhana yako ni potofu. Kipaji cha mtoto katika nchi za wenzetu hugunduliwa katika umri mdogo (under 5) na kuendelezwa. Rudia kusoma uzi wangu hapo juu na utafakari upya.

Green: Hapa tuko sawa; na hii hasa ndio ilikuwa concern yangu kubwa katika kuanzisha uzi huu. Nashukuru hapa tumeenda sawa. Welldone!

Bright green: Hakuna mtu aliyelaumu ila nimejaribu kuonyesha jinsi gani serikali inavyoshindwa kuendeleza vipaji vya watanzania katika fani mbali mbali.

Grey: Mkuu, huu usemi wako ni wa jumla mno. Una uahakika gani watu wote wanaochaguliwa kwenda ‘special schools' hakuna miongoni mwao wanaoiba paper? Kwani mtu hawezi kuiba paper akapata ONE akifika pale Ibouru anapiga msuli na kutoka na ONE ya Ilbouru? Unachekesha kweli!

Faint red: unamaanisha kwamba wanafunzi wote husomea katika mazingira yanayofanana? Huoni kwamba wanaosomea chini ya mwembe walipaswa kuwa na pass mark zao tofauti na wale wanaosomea madarasani?
Hata serikali hupanga ufaulu wa shule kulingana na idadi ya wanafunzi katika shule husika, kama matokeo yanavyotangazwa na NECTA kila mwaka. Kwanini basi utaratibu kama huu usitumike kutenganisha ufaulu wa wanafunzi waliosmea chini ya mwembe kutoka ufaulu wa wale wanaosomea darasani? Hapa kuna ulinganifu gani hadi wote wawekwe kundi moja?


Kuna baadhi ya shule wanafunzi huanza kidato cha kwanza hadi cha nne wakiwa hawana mwalimu wa somo kama Hesabu, Fizikia, Kemia, nk. Wanafunzi hawa hujisomea wenyewe na mwisho wa siku baadhi yao hupata alama C kwenye masomo hayo kwa juhudi zao binafsi, ukilinganisha na alama A wanazopata wanafunzi wanaofundishwa kwa miaka yote minne, tena kwa ufasaha na wanafundishwa na walimu wazoefu na wanaojituma kweli kweli. Katika kesi kama hii unawezaje kuwalinganisha wanafunzi hawa-ukasema kwamba waliopata A (kwa kufundishwa kwa miaka 4) wana ‘kipaji maalum' wakati waliopata C (kwa kujisomea wenyewe kwa miaka 4) ukawaona kwamba hawana kipaji?

Mfano mdogo ni huu hapa: Mwanariadha X alikimbia meta 100 kwenye kiwanja cha nyasi, akiwa amevaa viatu vya kukimbilia, kwa kutumia sekunde 5 na mwanariadha Y alikimbia meta 100 kwenye kiwanja chanye miiba ya mbigiri, na akiwa pekupeku, kwa muda wa sekunde 8. Je, ni nani kati ya hawa wawili (X & Y) ambaye ni mwanariadha bora (‘mwenye kipaji maalum')? Ukitafakari hali kama hii ndipo utagundua kwamba classification ya passes kwa wanafunzi katika nchi hii haiko fair. Wanafunzi wanasomea chini ya mpera na wale wanaosomea darasani mwisho wa siku hupimwa sawasawa! Uliona wapi upimaji wa kiwendawazimu kama huu?

View attachment 163616
Wanafunzi wakisomea chini ya mkuyu


Wanafunzi wakisomea darasani
 
Unamaanisha kwamba wezi wote hawapati divisheni ONE ama? Je, mtoto aliyesomea chini ya mwembe akapata divisheni THREE na mwingine aliyesomea Tusiime akapata divisheni ONE ni nani mwenye KIPAJI MAALUM kati ya hawa wawili?

Mwenye div One ndo anakipaji mkuu ww wa wapi?


Sent from my iPhone using JamiiForums.🔩🔨
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…