Kufeli huku ni janga la taifa si suala la Wakristu vs Waislamu

mimi naamini NECTA NI fumo kristo. shule za mikoa yenye waislam kidogo wanapeleka A, zenye waislam wengi wanaambulia D.
huu ni uchunguzi ninaoendelea kuufanya.
 

Mwanaasha na yeye ni wakristo wamemferisha?
 
Nashauri Baraza la Ulamaa litoe watu kumi wenye weledi wa kusahihisha mitihani waingizwe NECTA ili kusahihisha mitihani ya waislam
 
mimi naamini NECTA NI fumo kristo. shule za mikoa yenye waislam kidogo wanapeleka A, zenye waislam wengi wanaambulia D.
huu ni uchunguzi ninaoendelea kuufanya.


Ni ruksa kukata rufaa na kisha kusahihisha makaratasi ya mtihani upya na timu mpya. Shule husika wanaruhusiwa kupeleka wawakilishi mashaidi. Makaratasi bado yako Baraza hayachomwi hadi mwaka mmoja wakisubiri rufaa.


Ukiona shule hazikati rufaa wakati fursa iko wazi basi tunahitaji kujiuliza, why? wanajua aibu watakayoipata. Njia pekee ni kulalamika hovyo na kukwepa wajibu.

chukua mtoto mmoja wa dini yako anayelalamika kuonewa msaidie kwenda naye baraza kukata rufaa kisha tupe ushaidi hapa.
 
Ndalichako anataka kugombea ubunge. ndio maana shule za kwao ni A tu
 
Sasa, jambo moja liko wazi sana kwamba shule za Kikatoliki – si shule za majina ya Kikristu tu -karibu sehemu zote duniani zinatoa elimu ya kipekee na bora zaidi.
Hilo ni kweli India, China, Pakistani, Uingereza, Marekani na hata Indonesia
Mkuu unaweza kunipa majina ya shule ulizodai zinafanya vizuri nchi hizo kuliko shule nyingine?
 
Kama unayosema ni kweli wala hawatashinda, wanaweza kuonekana wemeshinda kwa kuona idadi imekuwa kubwa kuliko upande shindani lakini elimu ikaporomoka zaidi ya hapa. Mfano mzuri ni mahali lawama zinapopelekwa, kwa mtu mwenye akili hawezi kupeleka lawama kwa msahihishaji. Unataka msahihishaji afanye nini, na kama atafanya unavyotaka kuna elimu tena hapo!, si sawa na cheti cha kununua tu!.
Kama ushindi unaouzungumzia ndio huu, nafasi zote za kazi watashika wageni. Nani ataajiri mtu mwenye cheti kizuri lakini hajui afanyalo!
Kama malalamiko haya ni kutokana na matokeo, basi tuchukue hatua tuwabane wanaosimamia elimu yetu taifa linaangamia!.
 
Mmetenga tu bilioni tuchache kwenye hayo mabilioni mengi mnayopokea kwenye hiyo PROJECT ili mjenge shule bora au ni mabilioni ya kuendeshea radio na tv tu?
 
Wakati mwingine tunaangalia output - yaani MATOKEO ya mwisho Divisions (I, II, III, IV, 0) tunsahau inputs. Tunasahau kwamba OUTPUT ni matokeo ya INPUT na input kwa kweli ni mchakato ukianzia tangu makuzi ya mtoto, anapoanza shule, anavyoishi shuleni, nyumbani, na mtaani, n.k.

Tabia ya mtoto anayorithi kutoka kwa wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, walimu, viongozi wake wa dini (kiroho), n.k. aina ya maisha anayoishi (life style), anavyoona wengine wa kundi lake (dini, n.k.) ndani na hata huko nchi za wenzetu (akina Boko Haram, Al-Shabaab, Taliban, wanaopinga elimu dunia n.k.) yana impact kubwa sana kwa maisha ya mtoto kitaaluma n.k.

Hebu fikiria aina ya mahubiri yanayohubiriwa na baadhi ya viongozi wa dini hapa nchini iwe ndani ya majumba ya ibada au maeneo ya wazi - ni mahubiri yanayojengea watoto viburi na dharau. Hebu kwa mfano ukiwa penye kusanyiko la watoto wa shule ngazi ya sekondari mfano ndani ya daladala - Dar es Salaam. Kwa muda mfupi sana, maongezi na tabia zao watakazozionesha, hata kama hawajavaa uniform za shule zao, unaweza kabisa kukisia na ukapatia kwa zaidi ya 90% mtoto huyu ni wa dini gani.

Tujenge kwanza misingi. Tusitegemee matunda bora penye misingi mibovu.
 
Hivi huyu Mcechuru Ndalichako sio mnyarwanda kweli? isijekuwa anatukorogea elimu kwa makusudi!

Hizi ni hisia za kiwendawazimu kwa mtu unayejiita great thinker. Watanzania wenzangu ni lazima tutambue kwamba bila kuwa na walimu wa kutosha wenye viwango na ubora wa hali ya juu,zana bora za kufundishia,maabara na maktaba watoto wetu wataishia kufeli kila mwaka. Shule chache ambazo mpaka sasa zinafanya vizuri ni kwasababu ya kuwa na walimu wazuri na mazingira bora ya kujisomea! Huyo anayedai shule fulani imefelishwa ajiulize kama shule yenyewe inao hata walimu waliohitimu ama ni makanjanja tu wanaotafuta mkate!
 
Umenena mkuu!.
Hizi shule huwa hazina mzaha, wanajitahidi kutafuta walimu wazuri kadri inavyowezekana na wanajitahidi kuwahudumia pia. Licha hivyo wanafunzi ni lazima wajitume, kuvuka darasa inabidi uvuke kiango cha alama zilizowekwa, ukishindwa unarudi nyumbani na hawatanii.
Kama shule zingine zitaiga mtindo huu ni wazi zinaweza kupunguza hii hali ya kufeli inayotisha kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…