Facebook unasema haina effect??hahaha ina effect kubwa sana kwa hawa madogo,
Hizi page zilizojaa picha za utupu na stori za ng*ono angalia likes zinazopata afu uchunguze nyingi zinatoka wapi kama si kwa wanafunzi,
Mimi hili swala lilinisumbua sana ila nikafuatilia na hawa madogo hata shuleni kusoma muda mwingi hutoroka shuleni, wengi wana makundi tofauti, mara wengine wavuta bangi, wengine makundi ya kupigna mtaani, wengine wapenda muziki kupindukia, wengine wanaunda makundi ya kuchez muziki mtaani, muda woote wanaupotezea huko, afu kazi kuioaumu serikali, Serikali najua ina part yake ila hili labda niseme kwa wanafunzi wengi wa kijijini na wasiojiweza kifedha kabisaaaa ila wenye moyo wa kusoma, nyie wengineeee woote ni ujinga wenu wa kupenda sana starehe na kusahau kusoma, mbona wengine wamepata division 1 na 2, hivi serikali iwafelishe hamjui wanaosahisha mitihani ni kaka zenu, dada zenu na wazazi wenu? Au mnadhani waziri ndio anaenda anakaa anasahihisha mitihani?? Na unadhani ni mtu moja? Kwa taarifa yako wapo wengi sana na kati ya hao wapo wenye uchungu na nci yao hawawezi wakafanya ujinga.
Kwanza anza kujirekebisha mwenyewe alafu ndiyo uiachie serikali, anza mwenyewe uone kama hata serikali utailaumu, mbona mimi nimesoma shule ya vipaji maalumu na walimu hakuna lakini kwa umoja wa wanafunzi tumeweza kujisomea na kusaidiana wale waliosomamtuition na bado nikafaulu vizuri? Sasa wewe wa mjiniunayecheza na facebook usiku kucha unaongea nini? Wengi wenu mkitoka shule tu mnafunika daftari, mtu kupata FFFFFFF masomo yote saba afu ukaniambia ni serikali imekukosesh huku we mtoto wa mjini nakushangaa sana, wa kijijini ambae hana waimu wala pesa anatafuta elimu anapata Div2, Jipange upya dogo, huo sio mwisho wa maisha sasa kaa ufikirie niniunataka ufanye na wapi umekosea usikae unatafuta wa kumtupia lawama mwisho wa siku haitosaidia chochote utakuta umepoteza muda tu, nimeona wengi ambao walifeli na wakaanza chuo ila walikua na goal ya kufika kupata degree kama wengine wakaanza kupigana wakaanza kusoma wakajirekebisha pale walipokua wamekosea na sasa wanasoma degree vizuri. Soma sana, weka malengo kichwani, hata kama umefeli ukisema unataka kua daktari unaweza, rudia form two uone kama hauwi daktari, afu ukirudia piga msuli kwelikweli, kua kama unaanza moja na weka dedication na hiyo kitu moyoni afu uanze kufuatilia field yako vizuri upate ujuzi zaidi, badala ya kupoteza muda facebook kaa youtube unaangalia basi hata video za biology au physics au hata masomo mengine kama wewe hupendi science.. Tumepita huko dogo na sasa tupo vyuo vikubwa duniani tunajua jinsi mambo yalivyo... And tafuta ushauri kwa watu ufanye nini sasa, Fightiiiiing!,