Kufeli Mathematics sekondari; Mtazamo wangu.

Trance M

Senior Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
183
Reaction score
37
Habri za mchana wanajamvi.

Poleni na shughuli za kila siku za kuhakikisha mlo unaenda kinywani. Pia poleni na hongereni kwa mfungo mtukufu ndugu zetu waislam.

Napenda kutoa mawazo yangu juu ya kuongezeka kwa kiwango cha kufeli somo la Hesabu katika mashule ya sekondari. Jambo hili huwa linaniumiza kicha sana nikiwa kama mwanamahesabu niliyebobea na nikishuhudia wanafunzi wengi wakifeli somo hili.

Huwa nafikiri pengine ni wanafunzi wenyewe kuwa vilaza au wakati mwingine wanafunzi kutopenda somo la Hisabati. Mwanafunzi hawezi kuanza kulichukia somo bila sababu za msingi na wala si kwamba wanafunzi wetu ni vilaza.

Nachojaribu kufikiri ni hii sekta ya elimu kufanyiwa marekevisho hasa katika sera za kuajili walimu (recruitment policy). Walimu wanaoenda kufundisha Hisabati katika shule za sekondari au hata msingi wengi wao ni wale waliokuwa na ufauru wa Division III kushuka chini na hawajafaulu hesabu.

Kwa wale wanoenda kufundisha masomo ya Arts kama History na Geography wengi wao wamefanya vizuri ukilinganisha na wa Hisabati. Kwa hiyo bado utaona kuwa walimu wanaoenda kufundisha Hisabati wengi ni wale waliofeli Hesabu. Mwanafunzi hawezi kufundishwa hesabu na mwalimu aliyefeli hesabu kwani matokeo yake wanafunzi ni kulishwa sumu na mwisho wa siku kifeli somo hilo na kulichukia katika maisha yao.

Sekta ya elimu iboreshwe kwa kuongeza mishahara kwa walimu na kutengeneza mazingira ya kufundishia kama nyumba za walimu na madarasa bora ili waliofaulu Hisabati Form six au Four wachague kuwa walimu badala ya kwenda kwenye fani nyingine kama Uhasibu, Engineerin, Udaktari na fani kama hizo.

Kwa kufanya hivi kutawavutia wanafunzi waliofaulu Hisabati kujiunga na Ualimu na kwa kuwa wamefaulu vizuri hesabu, watakiwa na uwezo wa kuwafundisha vizuri wanafunzi na wakafaulu. Tofauti na sasa ambapo walimu wengi wa hesabu ni waliopata hesabu Subsidiary au D. Huu ni mtazamo wangu. Karibu kwa mawazo
 
nawe pia nakutakia mfungo mwema pia nakuunga mkono kwa hilo nazan ni mtazamo chanya if u wish to die poor try to be a teacher hapa kwetu.
 
Kwa sasa hilo unalosema ni la kweli. Inafikia hatua walimu wanadharaurika kutokana kazi yao. Mfano mzuri ni yule mkuu wa wilaya Tanga (Holo holo) aliyebadikisha matumizi ya nyumba za walimu zilizojengwa na donors na kuwa zahanati kwa maelezo kuwa hazina hazi ya walimu. Kama umefuatilia Cloudstv jana utakuwa umeona. Kwa kweli mabadiliko ni muhimu sana katika hii sekta
 
Mkuu Trance M.
Kufeli kwa wanafunzi soma la hesabu ktk mashule yetu kuna sababu nyingi,
hapo umeandika kwa ufupi sana
ila ukweli yapo mengi yanayosababisha.
Mimi nikiwa kama Mwalimu ninaefundisha somo hili ukweli,
kufaulu hesabu kuna itaji mambo mengi ikiwa ni pamoja na yafuatayo. Kwanza mwalimu awe anaifahmu hesabu kiasi cha kutosha. Mwalimu ajitume kufundisha somo hilo na kuhakikisha topic zinaisha na zinaeleweka.
Kuwepo mitihani ya hesabu ya kuwajaribu wanafunzi kama weekly test, monthly test,n.k. Pia mwalimu anapaswa kusahihisha na kuwarudishia karatasi wanafunzi kwa muda. Kuwapa motisha wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye somo hilo na pia kuwaadhibu vikali wanafunzi watakao feli,tena adhabu ambazo ni productive punishment kama kufyatua tofali, shamba work, n.k na wala sio mafimbo kila mara.
Sasa utakuta sikuhizi haya hayapo kutokana na uhaba wa walimu wa somo hili, pia uchumi wa shule na wazazi ambapo pia naita sababu isiyo na msingi, kwanini? Sababu wakuu wa shule wanafanya uhuni wa kutotoa pesa kwa ajili ya kuchapisha mitihani hiyo ya marakwamara na kuelekeza mapesa kwenye mambo mengine yasio na maana kwakuwa ninachoamini cha msingi shuleni ni kumsaidia mwanafunzi afaulu mtihani wake.
~Pia sikuhizi kutokana na hii kampeni ya serikali ya kuwapekeka sekondari wanafunzi wengi, shule zinakuwa na wanafunzi wengi wakati huohuo walimu wa somolenyewe ni wa chache. Darasani wanafunzi hawazingatii masomo ni ufuatiliaji unakuwa mgumu sababu ya wingi wa wanafunzi wenyewe.
Nini kifanyike?,
serikali kutilia mkazo na kuongeza incentives wanafunzi wanaochagua kusoma mavyuoni ualimu hasa wa sayansi.
Kwa walimu hasa wa sayansi pia wapewe vipaumbele katika mashule na pia serikali iyoengeze mshahara japo sababu mimi binafsi siichulii uzito kwakuwa walimu/mtu apewe kiasi gani haridhiki.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru mkuu CHAMVIGA kwa mchango wako. Nadhani mwalimu kucover syllabus mapema si hoja, kinachotakiwa hapo ni je anaelewa vizuri anachowafundisha wanafunzi? Nina maana hisabati anaijua vizuri?

Pia nakuunga mkono kwa suala la Management za shule kwa kweli ni tatizo kubwa na hasa pale utakapokuta Head wa shule ni mbinafsi. Matumizi ya fedha ya shule inatakiwa yaelekezwe katika kuhakikisha mwanafunzi anafauli na si vinginevyo. Nadhani kuna utaratibu mzuri wa kuripoti masuala mabovu kama haya ya uongozi kwa REO au wizarani kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Ntakuwa mchoyo wa fadhila nisipo mshukuru mwl Songelaeli Kitundu (St. francis de sales) kihonda Morogoro.
Hesabu mbali na ufanisi wa walimu vilevile wanafunzi inabidi kujituma. kwa mf. huyo mwalimu niliyemtaja hapo juu katufundisha wanafunzi wengi ila mimi najiona ndio peke yangu niliyemuelewa kwa sababu nilitoka shule ya msingi sijui hesabu.
wanafunzi hawaipendi hesabu hili ni tatizo la kwanza. hapa inabidi itafutwe dawa mbadala kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaipenda hesabu. motisha iwepo n.k.. wengi huamini kuwa anayefaulu hesabu yupo katika nafasi nzuri ya kuelewa masomo mengine nawaunga mkono katika hili. katika ulimwengu wa science and technology, watu inabidi waijue vema hesabu, kwa sababu mambo mengi ya science yanataka application of maths. mf kwa wanaosoma IT wanajua hii.
swala la msingi ni kuhakikisha hesabu inapendwa. pia kutoa woga kwa wanafunzi kuwa hesabu ni ngumu. kwa leo
 
realness.



^
Ulichokisema ni ukweli kwamba mtu aliye na uwezo ktk hesabu pia anakuwa mrahisi ktk uelewa wa masomo mengine.
Ukiachalia mbali tatizo la upungufu wa walimu na mengineo kubwa ni katika uwezo wa mwalimu binafsi ktk hesabu.
 
Last edited by a moderator:
kumbe mtu akipata s au D hajui hesabu?,hilo siyo kweli kwasababu unaweza ukawa unajua hesabu lkn paper likaja tofauti.Ila kikubwa ni kwamba wanafunzi wengi hawapendi kufanya mazoezi au maswali ya hesabu wakiwa hm au darasani mwl akiwa hayupo namaanisha kuwa wanafunzi hawapendi kujisomea mara kwa mara somo la hesabu,kingine ni kwamba serikali siku hizi inampeleka mtoto form one ambaye ukiangalia matokeo yake ya hesabu unakuta ana 2,3,10 na 15 kati ya 100% halafu huyo mtoto mnataka akienda sekondari akapate 70% au 80% je inawezekana?.Naona mtoa mada hujui mambo ambayo walimu wanakutana nayo ndiyo maana unaongea hayo.
 

Mkuu realness nashukuru kwa mchango wako. Kimsingi kufaulu hisabati katika leve ya secondary mara nyingi hutokana na msingi mzuri mwanafunzi alioupata akiwa shule ya msingi. Mwanafunzi akiwa na mwalimu mzuri wa Hisabati shule ya msingi na akiwa ana moyo wa kujisomea/kufanya hesabu basi matokeo yake yanakuwa mazuri.

Hisabati ina appliction shehem nyingi sana. Nashukuru pia kwa maelezo waliotoa wengine.

Aidha umenikumbusha mwalimu wangu wa tuition Mr Mako katika shule ya msingi Mikumi. Jamaa alikuwa ni kichwa sana na pepa zake pasua kichwa. Kwakweli bado namkumbuka sana huyu mwalimu na pepa zake za Pure Mathematics (Calculus, integration
 
Last edited by a moderator:
realness.



^
Ulichokisema ni ukweli kwamba mtu aliye na uwezo ktk hesabu pia anakuwa mrahisi ktk uelewa wa masomo mengine.
Ukiachalia mbali tatizo la upungufu wa walimu na mengineo kubwa ni katika uwezo wa mwalimu binafsi ktk hesabu.

sure CHAMVIGA. Uwezo wa mwalimu ni muhimu sana laasivyo utawafelisha wanafunzi na watakupa majina ya ajabu ajabu tu
 
Last edited by a moderator:


Mkuu Dulley elimu ya sasa imeingiliwa na siasa jambo ambalo linahatarisha sana maendeleo ya elimu nchini mwetu. Watoto kutokujua kusoma na kuandika masekondari ni zao la siasa katika elimu.

Kama umenielewa vizuri nasisitiza zaidi katika sifa za mwalimu wa Hisabati kuwa ni lazima awe amefaulu hilo somo ili awe na sifa. Ukweli ni kwamba ukiangalia walimu wa Hisabati walio wengi wamefeli somo hilo. Kuna wazo lilitolewa la kuwapima walimu kwa kuwapa mitihani ya kufanya nadhani na lenyewe lingefanya kazi.

Otherwise naunga mkono mapendekezo yako mengine.
 
Last edited by a moderator:
all in all... hesabu inahitaji msingi na kujituma kwa mwanafunzi, ukimuongezea mwalimu asiye na stress A za hesabu mtazichoka. Tuache kuwatisha watoto kuwa hesabu ni ngumu kwa kufanya hivo tunawafanya wafeli kabla ya pepa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…