Habri za mchana wanajamvi.
Poleni na shughuli za kila siku za kuhakikisha mlo unaenda kinywani. Pia poleni na hongereni kwa mfungo mtukufu ndugu zetu waislam.
Napenda kutoa mawazo yangu juu ya kuongezeka kwa kiwango cha kufeli somo la Hesabu katika mashule ya sekondari. Jambo hili huwa linaniumiza kicha sana nikiwa kama mwanamahesabu niliyebobea na nikishuhudia wanafunzi wengi wakifeli somo hili.
Huwa nafikiri pengine ni wanafunzi wenyewe kuwa vilaza au wakati mwingine wanafunzi kutopenda somo la Hisabati. Mwanafunzi hawezi kuanza kulichukia somo bila sababu za msingi na wala si kwamba wanafunzi wetu ni vilaza.
Nachojaribu kufikiri ni hii sekta ya elimu kufanyiwa marekevisho hasa katika sera za kuajili walimu (recruitment policy). Walimu wanaoenda kufundisha Hisabati katika shule za sekondari au hata msingi wengi wao ni wale waliokuwa na ufauru wa Division III kushuka chini na hawajafaulu hesabu.
Kwa wale wanoenda kufundisha masomo ya Arts kama History na Geography wengi wao wamefanya vizuri ukilinganisha na wa Hisabati. Kwa hiyo bado utaona kuwa walimu wanaoenda kufundisha Hisabati wengi ni wale waliofeli Hesabu. Mwanafunzi hawezi kufundishwa hesabu na mwalimu aliyefeli hesabu kwani matokeo yake wanafunzi ni kulishwa sumu na mwisho wa siku kifeli somo hilo na kulichukia katika maisha yao.
Sekta ya elimu iboreshwe kwa kuongeza mishahara kwa walimu na kutengeneza mazingira ya kufundishia kama nyumba za walimu na madarasa bora ili waliofaulu Hisabati Form six au Four wachague kuwa walimu badala ya kwenda kwenye fani nyingine kama Uhasibu, Engineerin, Udaktari na fani kama hizo.
Kwa kufanya hivi kutawavutia wanafunzi waliofaulu Hisabati kujiunga na Ualimu na kwa kuwa wamefaulu vizuri hesabu, watakiwa na uwezo wa kuwafundisha vizuri wanafunzi na wakafaulu. Tofauti na sasa ambapo walimu wengi wa hesabu ni waliopata hesabu Subsidiary au D. Huu ni mtazamo wangu. Karibu kwa mawazo