Kufeli mitihani si mwisho wa safari, jipange

Kufeli mitihani si mwisho wa safari, jipange

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Februari mwaka huu, Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), lilitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2013.

Katika matokeo hayo, wanafunzi 151,187 walipata daraja sifuri, sawa na asilimia 42.91 ya watahiniwa 404,083 waliofanya mtihani huo.

Bila shaka idadi ya watahiniwa waliofeli ni kubwa na huenda wapo baadhi yao waliokata tamaa ya kuendelea na masomo baada ya kufeli kwa kiwango hicho kikubwa.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mpwapwa iliyopo Dodoma, Rukonge Mwelo anasema umefika wakati kwa Serikali kuanzisha masomo ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili wale wanaofeli wasibaki njiapanda.

“Kuna wanafunzi wamepata sifuri kwenye mitihani yao lakini hao hao wakija kwenye kazi za mikono wanapata alama A,” anasema.

Anasema baadhi ya wanafunzi wanashindwa kufanya vizuri katika mitihani kutokana na kuwepo kwa mazingira mabaya ya kujifunzia, ikiwamo kukosekana kwa walimu na vifaa vya kujifunzia.

Mwelo anaongeza kusema: “Kama kila wilaya itakuwa na kituo cha mafunzo ya ufundi stadi kwa watu waliofeli itasaidia sana, kwa sababu kufanikiwa siyo lazima ufike kidato cha nne.”

Anatoa mfano wa wanafunzi walioacha shule na kujiingiza katika biashara ya kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki baada ya kukatishwa tamaa na wenzao waliopata sifuri.

Hata hivyo, mzazi Marry Kashinde anasema hata ujasiriamali nao unahitaji elimu ili mtu aweze kufanikiwa.

Anasema baada ya binti yake kufeli aliomba afunguliwe biashara ya kuuza nguo za watoto, lakini alishindwa kuendea kwa kukosa ujuzi wa kazi hiyo.

“Mimi nina ushahidi wa kutosha kuwa hata ujasiriamali unahitaji elimu, siyo lazima iwe elimu rasmi lakini mtu ajue hata namna tu ya kufunga mahesabu ya biashara yake,” anasema.

Anatoa ushauri kwa kusema: “Mzazi anatakiwa kujua mtoto wake anapenda kufanya nini mapema kabla hata hajamaliza masomo yake. Kile anachopenda ndicho aendelezwe kwa gharama yoyote.”
 
Back
Top Bottom