Kuficha kipara, kuficha mvi, kujichubua ni kujikataa uhalisia wako

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Members nadhani wapo wengine kama mimi ambao wanaona sio sawa kwa mtu kuikataa hali ya uhalisia wake aliopewa na mungu, kwa wale waliozaliwa miaka ya 70 kurudi nyuma watanielewa vizuri zaidi kwani ilikuwa sio rahisi kumuona mwanaume anaficha kipara chake au mvi zake, vilevile ilikuwa hakuna kujichubua kwa akina Dada, kama ni Black basi ata maintain rangi yake na walikuwa wanaonekana wazuri sana. Sasa miaka ya hivi karibuni hasa kuanzia miaka ya 95 kumekuwa na kasi ya ajabu kwa wanaume wengi kuukataa uhalisia wao. kasi ya kunyoa vipara imeongezeka kwa kasi ya ajabu; na vipara hivi vinanyolewa kwasababu kuu mbili. 1-kuficha upara wa asili kutokana na umri. 2- kuficha mvi. kwa mtazamo wangu nadhani masuala kama haya ni vema yakatungiwa sheria nakuchukuliwa kama makosa ya jinai. KOSA LA KUGHUSHI. Ni kwanini ughushi kuwa mweupe kwakujichubua. Pia ikiwezekana itungwe sheria itakayotunza maadili ya uhalisia wa mtu na ikitokea mtu kughushi rangi yake ya asili basi asipewe baadhi ya madaraka au nyadhifa fulani muhimu. Kuukubali uhalisia wako ni kuheshimu aliyekuumba na hiyo ndiyo Busara, lakini kuukataa uhalisia wako nikumkosoa Aliyekuumba na mtu kama huyu hawezi kuwa na busara ya uongozi au ushauri hata kwenye familia yake. Wadau nimeona niwashirikishe kwa hili ili wengi tuikatae tabia hii na tuwashauri vijana/mabinti zetu wakubali nakuthamini uhalisia wao, Nimekuwa na jirani yangu kimara kwa miaka 6, muda wote tangu nimfahamu nilipenda sana nywele zake kwani zilikuwa zinaonekana kuwa na weusi uliokolea sana, ila siku moja moja nikawa naona kama kuna nywele nyekundu maeneo ya shingo, sikujua. Ni jamaa alikuwa na kazi ya maana kwenye kiwanda cha wahindi fulani. sasa ghafla ameachishwa kazi na alikuwa hajajiweka vizuri hivyo akayumba sana, sasa hapo ndipo nikabaini kumbe jamaa alikuwa na nywele kama za EDWARD!!!
 
Wewe una mawazo ya kidikteta. Umesahau enzi hizo wanawake walikuwa wanachoma nywele na kupaka Ambi?
 
Kuna mijamaaa mingi hapa town wanapaka pico kuficha mvi aibu
 
Umeongea vizuri, lakini unapoingiza mambo ya sheria katika nafsi ya mtu, tumeachana! uumbaji wengine hawajui kama kuna kuumba, usiwalazimishe matakwa yako!
 
Kwa definition hiyo hata kuvaa nguo ni kuuficha uhalisia wako(waafrika tulikua tunavaa magome ya miti kabla ya ujio wa wazungu wakoloni wakatuletea nguo za pamba,Mhalisia amebaki mmoja tu Mjomba Mpoto)
 
Wewe una mawazo ya kidikteta. Umesahau enzi hizo wanawake walikuwa wanachoma nywele na kupaka Ambi?
Ila Kuchoma nywele ni isue tofauti KUJICHUBUA. Waafrica tunahitaji kujitambua nakujithamini, je umeona mzungu akijipaka rangi awe mweusi!!?
 
Sioni tofauti kati ya kuchoma nywele na kujichubua. Yote ni yale yale. Wanawake walikuwa wanachoma nywele ili zilainike na zionekane kama za wazungu. Enzi hizo kama unakumbuka kulikuwa na staili ya kujichubua kwa Ambi (mkorogo kwa sasa) ili ngozi ionekane rangi ya chungwa. Wanaume mabitozi walikuwa wanapasua "way" kwenye nywele ili zionekane zimegawanyika kama za wazungu (hii ilikuwepo sana kabla ya miaka ya sabini). Kasumba hizi bado zipo hadi sasa ingawa zinachukua sura tofauti.

Suala la kujitambua na kujivunia kama mtu mweusi ni suala la muhimu na la msingi, lakini sio suala la kutungiwa sheria. Huo utakuwa ni udikteta ambao hautafanikiwa!
 
Je kuweka meno bandia nako unasemaje mkuu? Muite
Wewe sasa umeamua kuchekesha watu. Meno bandia lengo lake kubwa nikimsaidia mtu wakati wa kula. Ingawa inasaidia pia kuficha ukibogoyo. Lakini kujichubua, kupaka peaco na kuficha upara ni ujinga na huondoa heshima fulani
 
Last edited by a moderator:
Sioni tofauti kati ya kuchoma nywele na kujichubua. Yote ni yale yale. Wanawake walikuwa wanachoma nywele ili zilainike na zionekane kama za wazungu. Enzi hizo kama unakumbuka kulikuwa na staili ya kujichubua kwa Ambi (mkorogo kwa sasa) ili ngozi ionekane rangi ya chungwa. Wanaume mabitozi walikuwa wanapasua "way" kwenye nywele ili zionekane zimegawanyika kama za wazungu (hii ilikuwepo sana kabla ya miaka ya sabini). Kasumba hizi bado zipo hadi sasa ingawa zinachukua sura tofauti.

Suala la kujitambua na kujivunia kama mtu mweusi ni suala la muhimu na la msingi, lakini sio suala la kutungiwa sheria. Huo utakuwa ni udikteta ambao hautafanikiwa!
Nimekuelewa vema sasa, nadhani nilikosea kuweka hapa Law Forum. Mantiki yangu ilikuwa kukosoa hizi kasumba zakuukana uasili wetu, pia kuficha uzee
 
Naona siku kuna vyuo vingi vya sheria... Watu wanaibuka tu.
 
Tatizo ukishasomeshwa Chuo kimoja basi unaondoka na yaleyale mawazo uliyopewa pale; Toka nje na tafuta idea mpya!!!! pia elewa kuwa sheria ulizofundishwa chuoni kwako zilitokana na ideas za watu mbalimbali na zikaanzisha mijadala kisha zikaonekana zinafaa ndipo zikakubalika kutumika na zipo ambazo zilionekana hazifai kabisa au zilipunguzwa makali nakupitishwa. Labda nikuambie tu kuwa mjadala kama huu ulishatolewa na mwanaharakati mweusi wa Harvad university baada ya kifo cha Michael Jackson na alikosoa tabia ya mtu mweusi kuidharau rangi na asili yake hadi kujibadilisha ili kufanana na mzungu, ktk maoni yake alitamani kama kungekuwa na sheria inayomkataza binadamu kubadili uhalisia wake. hivyo hata mimi nimetoa kama maoni yangu. Pia usipende kutoa comment za kumdhihaki mtu usiyemjua kielimu, inawezekana akawa ni mwl wa Prof wako.
 
Back
Top Bottom