Members nadhani wapo wengine kama mimi ambao wanaona sio sawa kwa mtu kuikataa hali ya uhalisia wake aliopewa na mungu, kwa wale waliozaliwa miaka ya 70 kurudi nyuma watanielewa vizuri zaidi kwani ilikuwa sio rahisi kumuona mwanaume anaficha kipara chake au mvi zake, vilevile ilikuwa hakuna kujichubua kwa akina Dada, kama ni Black basi ata maintain rangi yake na walikuwa wanaonekana wazuri sana. Sasa miaka ya hivi karibuni hasa kuanzia miaka ya 95 kumekuwa na kasi ya ajabu kwa wanaume wengi kuukataa uhalisia wao. kasi ya kunyoa vipara imeongezeka kwa kasi ya ajabu; na vipara hivi vinanyolewa kwasababu kuu mbili. 1-kuficha upara wa asili kutokana na umri. 2- kuficha mvi. kwa mtazamo wangu nadhani masuala kama haya ni vema yakatungiwa sheria nakuchukuliwa kama makosa ya jinai. KOSA LA KUGHUSHI. Ni kwanini ughushi kuwa mweupe kwakujichubua. Pia ikiwezekana itungwe sheria itakayotunza maadili ya uhalisia wa mtu na ikitokea mtu kughushi rangi yake ya asili basi asipewe baadhi ya madaraka au nyadhifa fulani muhimu. Kuukubali uhalisia wako ni kuheshimu aliyekuumba na hiyo ndiyo Busara, lakini kuukataa uhalisia wako nikumkosoa Aliyekuumba na mtu kama huyu hawezi kuwa na busara ya uongozi au ushauri hata kwenye familia yake. Wadau nimeona niwashirikishe kwa hili ili wengi tuikatae tabia hii na tuwashauri vijana/mabinti zetu wakubali nakuthamini uhalisia wao, Nimekuwa na jirani yangu kimara kwa miaka 6, muda wote tangu nimfahamu nilipenda sana nywele zake kwani zilikuwa zinaonekana kuwa na weusi uliokolea sana, ila siku moja moja nikawa naona kama kuna nywele nyekundu maeneo ya shingo, sikujua. Ni jamaa alikuwa na kazi ya maana kwenye kiwanda cha wahindi fulani. sasa ghafla ameachishwa kazi na alikuwa hajajiweka vizuri hivyo akayumba sana, sasa hapo ndipo nikabaini kumbe jamaa alikuwa na nywele kama za EDWARD!!!