Kuficha pesa Uswisi, ujinga wa kiwango cha juu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Waswisi ni wezi werevu, wanaishi kama peponi kwa pesa za wezi na kuhalalisha wizi wao wamejitungia sheria za kujilinda na kubariki wizi huo.

Wana mabilioni ya dola wanayafanyia biashara na miamala mbalimbali huku wamiliki wao wakiwa kimya tuli kabisa, hawaulizi kuhusu riba wala faida itokanayo na mapesa yao! Wataanzia wapi nao ni wezi?

Mtu anayesumbukia pesa yake, mfanyabiashara mwenye biashara zake halali kamwe hawezi kwenda kuficha pesa zake kule! Anajiamini kazipata kwa halali.

Waswisi wajanja wana utaratibu mzuri na salama sana unapotaka kuwapelekea pesa za wizi, hawashindwi kukodisha ndege kufuata mzigo popote ulipo, customer care yao ni nzuri sana kwenye hilo! Lakini kimbembe ni siku utakapotaka kuzichukua, utaambiwa kuna sheria za kimataifa za kusafirisha pesa utapewa utaratibu mgumu mno na wenye gharama kubwa wa kutoa hizo pesa

Pesa nyingi huishia mikononi mwao, ni pesa ya wizi kwahiyo hata kuhifadhi kwake ni kwa siri
Pesa ya Uswisi Haina mrithi
Signatory ni mmoja tu (muwekaji)
Haina mashahidi
Hizi pesa nyingi huishia huko huko kama mmiliki akifa au akifungwa

Na ikitokea nchi husika ikajua kuwa kiongozi/viongozi wake wameficha hela huko na wakadai hiyo hela utaratibu wake was kuipata nao ni mgumu mno tuneyaona kwa Sani Abacha wa Nigeria na wengineo

Hapa nchini tunaambiwa kuna watanzania kama mia hivi wameficha mapesa Kule! Hao imekula kwao nyingi zitaishia huko! Na hakuna mtu mwenye uwezo wa kwenda kuzirudisha ni porojo za kisiasa tuu
 
Pesa ya Sani Abacha dola za marekani zinazozidi 250milioni zilikuwa kule, Gaddafi wa Libya ana mapesa yake kule mengi sana mtoto wa Wade naye pia anazo zinazofikia usd 220 hawa wote imethibitika pasi na shaka kuwa pesa ni zao, lakini serikali zao zimekuwa na wakati mgumu kuzidai au kurudishiwa

Uswisi wameweka taratibu ngumu mno, ni pesa ambazo hazina mrithi wala mirathi, wanazifanyia miamala wannazifanyia biashara wanapata faida kubwa lakini mwenye nazo hafaidiki chochote sanasana analipia gharama ya kuzitunza

Na inapotokea wakaamua kuzirudisha kwa serikali husika sio cash bali huzirudisha kwa njia ya miradi mbali mbali kama Barbara elimu na afya na makandarasi hutafutwa na wao wenyewe, mwisho wa Siku bado faida kubwa hurudi kwao, mradi ambao kwa mfano ungegharimu USD laki5 wao huleta makadirio ya milioni

Tunaitajirisha uswisi kwa rohombaya zetu na uchoyo uliopitiliza, Wananchi wetu wanakufa kwa kukosa huduma muhimu viongozi wanakimbizia mabilioni uswisi kuyaficha
 

Mkuu kuna mambo umenifumbua macho: 1. Uingizaji wa pesa rahisi ila kuzitoa ni kasheshe. 2. Pesa za wizi kufanyishwa biashara kwa nchini husika thru projects tena yenye riba kubwa ( hii nisawa na moneylaundering). 3 hivi sasa mamlaka zetu huwa zinafanya nini mfano kazi aliyoifanya Zitto ina maana hukuna alichofanya sasa!
 
Sikufaham kabisa kuhusu hili la uswis. Yani panya buku yanangata na kupuliza. Si ndio hawa wanajisif katika haki za binadam cjui majineva convention na blah blah kibao
 
Uzi mzuri sana. Ndugu mshana napenda sana kusoma nyuzi zako. Halafu wewe siyo kweli the auto spoken super journalist wa raia mwema Johnson Mbwambo??!! Yani nahis his

Hapana ndugu yangu nami huwa namsoma tu kwenye magazeti
 
Muda wa kesi hii umenishangaza kusema kweli, sioni sababu ya kesi kuchukua muda mrefu kiasi. Haya mabenk nayo ni wezi labda walitafuta namna ya kuiba pesa hizi wagawane na wanasheria wao, ila nadhani miaka hii ya karibuni hili zoezi limerahisishwa ukilinganisha na miaka ya nyuma. Kuna nyingine $700 million zilikuwa zimesharudishwa miaka ya nyuma.

Jus imagine kesi imechukua miaka 16 na kwa gharama za serikali ya Nigeria! Uswisi hawawezi kulipa riba wala chochote
 
nasubiri wafuasi wa mafisadi watai''counter attack'' vipi hii hoja.....ama ndio watapita kimyakimya..
 
nasubiri wafuasi wa mafisadi watai''counter attack'' vipi hii hoja.....ama ndio watapita kimyakimya..

Kwasasa wako busy na uchaguzi kuhakikisha upinzani or maybe El hawachukui nchi, wanajua nini kitatokea, ya Senegal yamewapa warning kubwa
 

Anachokifanya Zitto ni michezo ya kisiasa hana mandate yeyote ya kudai zile pesa wala kuzirudisha sio zake hana asili nazo na hajaweka yeye! Yeye ni political opportunist anayejua vema udhaifu wa media za Tanzania! Hazihoji zinaandika tu kwakuwa kaongea Fulani

Utaratibu ni mgumu mno jamani na wenye gharama kubwa! Imagine Sani Abacha alithibitika pasipo shaka kuwa aliweka mabilioni kule lakini kuipata ile pesa Wanaigeria wameisotea kwa miaka 16!!!! Umri wa mtu huo, MIAKA 16; SIO MIAKA 6
 
Ahsante... nimejifunza kitu kikubwa.
Nadhani hata hao wanaoficha wanaficha tu hawajui kwanini wanaficha.
Sawa na kibibi fulani akishiba anaficha tu chakula kilichobaki eti atalula baadae matokeo yake kinaoza. Kumbe ujinga tu.
 
Ahsante... nimejifunza kitu kikubwa.
Nadhani hata hao wanaoficha wanaficha tu hawajui kwanini wanaficha.
Sawa na kibibi fulani akishiba anaficha tu chakula kilichobaki eti atalula baadae matokeo yake kinaoza. Kumbe ujinga tu.

Ni mind setting tu Da Pretty ni ishu ya katiba uzalendo na kujitoa kutumikia taifa badala ya kutumika na kundi fulani lenye malengo Fulani! Ni suala la uzalendo zaidi na kutanguliza maslahi ya nchi kwanza bila agenda yoyote iliyofichika
 
Last edited by a moderator:
Hawa Waswisi wanajionyesha ulimwenguni kuwa ni wachapakazi na wanafanikiwa kwa jasho lao, kumbe ni wizi mtupu.

Sijui ulimwengu unalichukulia vip hili suala, maana linafahamika kuwa ni wizi
 
bora zipotee huko huko tukose wote
mzaramo nyingi hazirudi kwakuwa hazina mirathi, cha wizi ni cha wizi tu hakina haki ya kisheria kukidai kwa taratibu walizojiwekea wao
 
Last edited by a moderator:

Uyo mtt wa wade yupo jela,kashaanza kutumikia kifungo chake cha miaka 6 na lazima alipe fine ya 210 millions of euros
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…