Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Waswisi ni wezi werevu, wanaishi kama peponi kwa pesa za wezi na kuhalalisha wizi wao wamejitungia sheria za kujilinda na kubariki wizi huo.
Wana mabilioni ya dola wanayafanyia biashara na miamala mbalimbali huku wamiliki wao wakiwa kimya tuli kabisa, hawaulizi kuhusu riba wala faida itokanayo na mapesa yao! Wataanzia wapi nao ni wezi?
Mtu anayesumbukia pesa yake, mfanyabiashara mwenye biashara zake halali kamwe hawezi kwenda kuficha pesa zake kule! Anajiamini kazipata kwa halali.
Waswisi wajanja wana utaratibu mzuri na salama sana unapotaka kuwapelekea pesa za wizi, hawashindwi kukodisha ndege kufuata mzigo popote ulipo, customer care yao ni nzuri sana kwenye hilo! Lakini kimbembe ni siku utakapotaka kuzichukua, utaambiwa kuna sheria za kimataifa za kusafirisha pesa utapewa utaratibu mgumu mno na wenye gharama kubwa wa kutoa hizo pesa
Pesa nyingi huishia mikononi mwao, ni pesa ya wizi kwahiyo hata kuhifadhi kwake ni kwa siri
Pesa ya Uswisi Haina mrithi
Signatory ni mmoja tu (muwekaji)
Haina mashahidi
Hizi pesa nyingi huishia huko huko kama mmiliki akifa au akifungwa
Na ikitokea nchi husika ikajua kuwa kiongozi/viongozi wake wameficha hela huko na wakadai hiyo hela utaratibu wake was kuipata nao ni mgumu mno tuneyaona kwa Sani Abacha wa Nigeria na wengineo
Hapa nchini tunaambiwa kuna watanzania kama mia hivi wameficha mapesa Kule! Hao imekula kwao nyingi zitaishia huko! Na hakuna mtu mwenye uwezo wa kwenda kuzirudisha ni porojo za kisiasa tuu