PUNKY hili suala lilishawahi kusemwasemwa hapo nyuma, kwamba Uswisi isipokee pesa chafu za wizi , lakini hakukuwa na matokeo yeyote ya maana kwakuwa hao waliojifanya wanaongea hivyo ndio wawezeshaji wakubwa wa zoezi zima na wafaidikaji wa pesa za wajingaHawa Waswisi wanajionyesha ulimwenguni kuwa ni wachapakazi na wanafanikiwa kwa jasho lao, kumbe ni wizi mtupu.
Sijui ulimwengu unalichukulia vip hili suala, maana linafahamika kuwa ni wizi
Uyo mtt wa wade yupo jela,kashaanza kutumikia kifungo chake cha miaka 6 na lazima alipe fine ya 210 millions of euros
Hujui unachoongeaWaswisi ni wezi werevu, wanaishi kama peponi kwa pesa za wezi na kuhalalisha wizi wao wamejitungia sheria za kujilinda na kubariki wizi huo
Wana mabilioni ya dola wanayafanyia biashara na miamala mbalimbali huku wamiliki wao wakiwa kimya tuli kabisa, hawaulizi kuhusu riba wala faida itokanayo na mapesa yao! Wataanzia wapi nao ni wezi?
Mtu anayesumbukia pesa yake, mfanyabiashara mwenye biashara zake halali kamwe hawezi kwenda kuficha pesa zake kule! Anajiamini kazipata kwa halali
Waswisi wajanja wana utaratibu mzuri na salama sana unapotaka kuwapelekea pesa za wizi, hawashindwi kukodisha ndege kufuata mzigo popote ulipo, customer care yao ni nzuri sana kwenye hilo! Lakini kimbembe ni siku utakapotaka kuzichukua, utaambiwa kuna sheria za kimataifa za kusafirisha pesa utapewa utaratibu mno na wenye gharama kubwa wa kutoa hizo pesa
Pesa nyingi huishia mikononi mwao, ni pesa ya wizi kwahiyo hata kuhifadhi kwake ni kwa siri
Pesa ya Uswisi
Haina mrithi
Signatory ni mmoja tu (muwekaji)
Haina mashahidi
Hizi pesa nyingi huishia huko huko kama mmiliki akifa au akifungwa
Na ikitokea nchi husika ikajua kuwa kiongozi/viongozi wake wameficha hela huko na wakadai hiyo hela utaratibu wake was kuipata nao ni mgumu mno tuneyaona kwa Sani Abacha wa Nigeria na wengineo
Hapa nchini tunaambiwa kuna watanzania kama mia hivi wameficha mapesa Kule! Hao imekula kwao nyingi zitaishia huko! Na hakuna mtu mwenye uwezo wa kwenda kuzirudisha ni porojo za kisiasa tuu
Hujui unachoongea
Watu hawafichi Bali wanaweka pesa uswisi, na zile pesa zina taarifa za wenyewe hata warithi wao wanajua...
Uswisi, kiboko yao ni Marekani tu. Pamoja na ujanja wao wa kutunga sheria za kuwalinda, Marekani imewashitaki na kuwatoza fine zaidi ya Dola Bilioni TATU mpaka sasa. Benki zao 14 zimeshitakiwa mpaka sasa.
Benki zao zinawaogopa serikali ya Marekani mpaka kuanza kukataa pesa za raia wao. Kama unataka kuficha, lazima uukane uraia wa Marekani. Kila mwaka raia zaidi ya 2000 wanafanya hivyo.
Soma zaidi kutoka Forbes.com na CNBC.com
Credit Suisse-not just a subsidiary but the parent-has plead guilty of conspiring to help Americans evade taxes. Plus, Switzerland's second-largest bank more than triples the $780 million fine UBS paid over similar charges.
Credit Suisse will pay nearly $1.8 billion to the Justice Department, $100 to the Federal Reserve, and a whopping $715 million to New York's Department of Financial Services.
Under the deal, Credit Suisse's parent must plead guilty to a conspiracy charge, admitting that it fostered U.S. tax evasion.
The deal was not offered to the 14 Swiss banks under U.S. investigation, but 106 Swiss institutions took the IRS deal by the Dec. 31, 2013.
Source: forbes.com
___According to the latest data from the Treasury Department, a record 3,415 Americans renounced their citizenship in 2014. That was up from the 2,999 in 2013 and more than triple the number for 2012.
Why are Americans giving up their citizenship?
While some may see taxes as the main reason to flee, that's only part of the story. The big policy change that's causing people to give up their American citizenship is FATCA, the Foreign Account Tax Compliance Act.
The act requires foreign banks to reveal any Americans with accounts over $50,000. Banks that don't comply could be frozen out of U.S. markets.
The program was designed to catch wealthy overseas tax cheats.
Source: CNBC.com
Naam Mkuu na hili labda litarahisisha hata nchi za Africa ziweze kujipatia pesa zilizokwapuliwa na mafisadi haraka badala ya kuwa na kesi ya miaka 16 au zaidi. Naamini kabisa US ikilisimamia hili kwa dhati kuhakikisha bank za Switzerland zinatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kurudisha pesa za wizi kutoka nchi mbalimbali za Afrika haraka iwe iwezekanavyo basi kutakuwa na mafanikio makubwa sana.
Mafisadi wameshashtukia hilo ndio maana now days hawazipeleki uswis wanazikimbizIa mkomboz na badae wanagawana kwenye viroba.
Asante kwa kuleta post yenye mashiko. Halafu kuna watu humu JF wanataka tupishe katiba pendekezwa ambayo itaruhusu wizi na uhujumu wa uchumi wa nchi. Eti wakubwa waruhusiwe kufungua akaunti nje ya nchi as if wamemuona Cameroon, Obama, Merkel, Putin, Lee na wengineo wamefungua akaunti hapo NMB Bongo. Sijui nani ametuloga sisi Waafrika. Wakati mwingine tunawaza hovyo hovyo tu
Acha hao sutas wazipige tu hizo hela. maana ni fedha za wizi. Mwizi akiibiwa hakuna shida
Mafisadi wameshashtukia hilo ndio maana now days hawazipeleki uswis wanazikimbizIa mkomboz na badae wanagawana kwenye viroba.
We unafikiri pesa yako iliyoko CRDB haifanyiwi biashara? Unalipwa riba kiasi gani?
Sheria zinaruhusu Uswisi mtu yeyote kuwa na akaunti ya benki isiyo hata na jina, na wafanyakazi wa benki wanalazimishwa na sheria kuficha siri za mteja, na sheria inaweza kumfunga mtu anayetoa siri za mteja. Ni mazingira mazuri mno kwa mtu kuficha pesa chafu zisizolipiwa kodi. Pia pesa yao ni moja ya fedha zilizo stable zaidi duniani, hivyo hauna risk ya kushuka thamani, unaweza kufungua akaunti hata ya aina yoyote ya pesa, unaweza kufungua akaunti hata ukiwa hapa bongo bila kwenda popote unatuma tu vitambulisho, japo akaunti zisizo na majina utatakiwa kwenda mwenyewe. Kuhusu kutoa pesa umekosea Mshana, benki za Uswisi zinaruhusu mwenye pesa yake kutoa kiasi cha pesa kwa notisi ya siku kadhaa kulingana na kiasi unachotaka kuchukua, ukitaka kujaza kwenye magunia unaruhusiwa, ukitaka cheki ya wasafiri wewe mwenyewe tu hawana masharti.
Wezi wanaoweka pesa huko siyo wajinga, nyie mnaoliwa ndiyo wainga, mnataka waziweke hapa ili siku mkitaka mzitaifishe...thubutuuu! Pesa za Uswisi siyo kwamba hazitaifishiki, zinahitaji milolongo mingi sana, lakini inawezekana, tena mkitaka CASH mnapewa chash, siyo huduma.
Pamoja kuna baadhi ya sehemu umetumia lugha ya kukera lakini sio shida kwangu, nimeangalia zaidi kwenye hitimisho nilichokisema mimi ndio hichohicho ulichokirudia wewe, kuweka ni rahisi sana sio kutoa
Vile vile ishu ya kupewa cash kwenye viroba inawezekana kabisa wala si tatizo lakini hebu niambie baada ya hapo utatoka vipi na viroba vyako vya minoti mpaka nchini mwako!?
Kumbuka kuna sheria za kimataifa za kusafirisha pesa, zina milolongo mingi na maelezo mengi, usidhani utapewa viroba vyako upande navyo ndege kama begi la nguo
Watu wana mabilioni nje ya nchi lakini kila siku wanaumiza vichwa jinsi ya kuyaingiza nchini salama bila kukamatwa wala kushukiwa ndio maana kuna ishu za kutakatisha pesa kila siku zinaripotiwa