Kuficha pesa Uswisi, ujinga wa kiwango cha juu

Kuficha pesa Uswisi, ujinga wa kiwango cha juu

Hawa Waswisi wanajionyesha ulimwenguni kuwa ni wachapakazi na wanafanikiwa kwa jasho lao, kumbe ni wizi mtupu.

Sijui ulimwengu unalichukulia vip hili suala, maana linafahamika kuwa ni wizi
PUNKY hili suala lilishawahi kusemwasemwa hapo nyuma, kwamba Uswisi isipokee pesa chafu za wizi , lakini hakukuwa na matokeo yeyote ya maana kwakuwa hao waliojifanya wanaongea hivyo ndio wawezeshaji wakubwa wa zoezi zima na wafaidikaji wa pesa za wajinga
Ukishakuwa na pesa unaweza kufanya chochote unachotaka kadiri ya mipango yako! Waswisi pesa ya wajinga wanayo hivyo ni rahisi kupaa kimaendeleo
 
Last edited by a moderator:
Uyo mtt wa wade yupo jela,kashaanza kutumikia kifungo chake cha miaka 6 na lazima alipe fine ya 210 millions of euros

Hiyo ni hukumu ya nchini mwake pesa iko nje ya nchi ulaya mpaka ije irudi Senegal itakuwa jasho limewatoka na niamini hawatapata zote, wataletewa mlolongo mrefu wenye taratibu nyingi na gharama kubwa kuweza kuzipata na sio ishu ya miaka miwili au mitatu, za Abacha ilichukua miaka 16 kuzipata
 
Waswisi ni wezi werevu, wanaishi kama peponi kwa pesa za wezi na kuhalalisha wizi wao wamejitungia sheria za kujilinda na kubariki wizi huo
Wana mabilioni ya dola wanayafanyia biashara na miamala mbalimbali huku wamiliki wao wakiwa kimya tuli kabisa, hawaulizi kuhusu riba wala faida itokanayo na mapesa yao! Wataanzia wapi nao ni wezi?
Mtu anayesumbukia pesa yake, mfanyabiashara mwenye biashara zake halali kamwe hawezi kwenda kuficha pesa zake kule! Anajiamini kazipata kwa halali
Waswisi wajanja wana utaratibu mzuri na salama sana unapotaka kuwapelekea pesa za wizi, hawashindwi kukodisha ndege kufuata mzigo popote ulipo, customer care yao ni nzuri sana kwenye hilo! Lakini kimbembe ni siku utakapotaka kuzichukua, utaambiwa kuna sheria za kimataifa za kusafirisha pesa utapewa utaratibu mno na wenye gharama kubwa wa kutoa hizo pesa

Pesa nyingi huishia mikononi mwao, ni pesa ya wizi kwahiyo hata kuhifadhi kwake ni kwa siri
Pesa ya Uswisi
Haina mrithi
Signatory ni mmoja tu (muwekaji)
Haina mashahidi
Hizi pesa nyingi huishia huko huko kama mmiliki akifa au akifungwa

Na ikitokea nchi husika ikajua kuwa kiongozi/viongozi wake wameficha hela huko na wakadai hiyo hela utaratibu wake was kuipata nao ni mgumu mno tuneyaona kwa Sani Abacha wa Nigeria na wengineo

Hapa nchini tunaambiwa kuna watanzania kama mia hivi wameficha mapesa Kule! Hao imekula kwao nyingi zitaishia huko! Na hakuna mtu mwenye uwezo wa kwenda kuzirudisha ni porojo za kisiasa tuu
Hujui unachoongea

Watu hawafichi Bali wanaweka pesa uswisi, na zile pesa zina taarifa za wenyewe hata warithi wao wanajua...
 
Hujui unachoongea

Watu hawafichi Bali wanaweka pesa uswisi, na zile pesa zina taarifa za wenyewe hata warithi wao wanajua...

Naongelea pesa za dili na si pesa halali, nina uhakika na ninachoongea KIWAVI, zingekuwa hivyo za Abacha, Mobutu na wengineo zingeenda kwa warithi wao tena bila zengwe! Hebu pitia post ya BAK hapo juu
 
Last edited by a moderator:
Uswisi, kiboko yao ni Marekani tu. Pamoja na ujanja wao wa kutunga sheria za kuwalinda, Marekani imewashitaki na kuwatoza fine zaidi ya Dola Bilioni TATU mpaka sasa kwa kuwasaidia raia wa Marekani kukwepa kulipa kodi. Benki zao 14 zimeshitakiwa mpaka sasa.

Benki zao zinawaogopa serikali ya Marekani mpaka kuanza kukataa pesa za raia wao. Raia wengi wa Kitajiri wa Marekani wanaamua kuukana uraia wao ili waepuke kushitakiwa au kulipa kodi zaidi. Kila mwaka zaidi ya 2000 kufanya hivyo.

Soma zaidi kutoka Forbes.com na CNBC.com

Credit Suisse—not just a subsidiary but the parent—has plead guilty of conspiring to help Americans evade taxes. Plus, Switzerland’s second-largest bank more than triples the $780 million fine UBS paid over similar charges.

Credit Suisse will pay nearly $1.8 billion to the Justice Department, $100 to the Federal Reserve, and a whopping $715 million to New York’s Department of Financial Services.

Under the deal, Credit Suisse’s parent must plead guilty to a conspiracy charge, admitting that it fostered U.S. tax evasion.

The deal was not offered to the 14 Swiss banks under U.S. investigation, but 106 Swiss institutions took the IRS deal by the Dec. 31, 2013.

Source: forbes.com

___According to the latest data from the Treasury Department, a record 3,415 Americans renounced their citizenship in 2014. That was up from the 2,999 in 2013 and more than triple the number for 2012.

Why are Americans giving up their citizenship?

While some may see taxes as the main reason to flee, that's only part of the story. The big policy change that's causing people to give up their American citizenship is FATCA, the Foreign Account Tax Compliance Act.

The act requires foreign banks to reveal any Americans with accounts over $50,000. Banks that don't comply could be frozen out of U.S. markets.

The program was designed to catch wealthy overseas tax cheats.

Source: CNBC.com
 
Naam Mkuu na hili labda litarahisisha hata nchi za Africa ziweze kujipatia pesa zilizokwapuliwa na mafisadi haraka badala ya kuwa na kesi ya miaka 16 au zaidi. Naamini kabisa US ikilisimamia hili kwa dhati kuhakikisha bank za Switzerland zinatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kurudisha pesa za wizi kutoka nchi mbalimbali za Afrika haraka iwezekanavyo basi kutakuwa na mafanikio makubwa sana.

Uswisi, kiboko yao ni Marekani tu. Pamoja na ujanja wao wa kutunga sheria za kuwalinda, Marekani imewashitaki na kuwatoza fine zaidi ya Dola Bilioni TATU mpaka sasa. Benki zao 14 zimeshitakiwa mpaka sasa.

Benki zao zinawaogopa serikali ya Marekani mpaka kuanza kukataa pesa za raia wao. Kama unataka kuficha, lazima uukane uraia wa Marekani. Kila mwaka raia zaidi ya 2000 wanafanya hivyo.

Soma zaidi kutoka Forbes.com na CNBC.com

Credit Suisse-not just a subsidiary but the parent-has plead guilty of conspiring to help Americans evade taxes. Plus, Switzerland's second-largest bank more than triples the $780 million fine UBS paid over similar charges.

Credit Suisse will pay nearly $1.8 billion to the Justice Department, $100 to the Federal Reserve, and a whopping $715 million to New York's Department of Financial Services.

Under the deal, Credit Suisse's parent must plead guilty to a conspiracy charge, admitting that it fostered U.S. tax evasion.

The deal was not offered to the 14 Swiss banks under U.S. investigation, but 106 Swiss institutions took the IRS deal by the Dec. 31, 2013.

Source: forbes.com

___According to the latest data from the Treasury Department, a record 3,415 Americans renounced their citizenship in 2014. That was up from the 2,999 in 2013 and more than triple the number for 2012.

Why are Americans giving up their citizenship?

While some may see taxes as the main reason to flee, that's only part of the story. The big policy change that's causing people to give up their American citizenship is FATCA, the Foreign Account Tax Compliance Act.

The act requires foreign banks to reveal any Americans with accounts over $50,000. Banks that don't comply could be frozen out of U.S. markets.

The program was designed to catch wealthy overseas tax cheats.

Source: CNBC.com
 
Naam Mkuu na hili labda litarahisisha hata nchi za Africa ziweze kujipatia pesa zilizokwapuliwa na mafisadi haraka badala ya kuwa na kesi ya miaka 16 au zaidi. Naamini kabisa US ikilisimamia hili kwa dhati kuhakikisha bank za Switzerland zinatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kurudisha pesa za wizi kutoka nchi mbalimbali za Afrika haraka iwe iwezekanavyo basi kutakuwa na mafanikio makubwa sana.

Ninakubaliana na wewe. Lakini ni muhimu kutofautisha pesa za wizi na pesa halali. Ninavyosoma hapa JF, wengi wameshaamini kuwa pesa za raia wa Tanzania nje ni za ufisadi, kitu ambacho siyo kweli kwa raia wote.

Pia, ni muhimu kujua sheria zetu kama zinalazimisha ulipaji kodi kwa pesa za mfanyabiashara alizochuma nje pia? Tuna mikataba ya kodi na nchi nyingine kupunguza kodi kama nchi nyingine?

Siyo nchi zote zina sheria kama za Marekani za kutaka kodi kwa pesa yote iliyochumwa na raia wake duniani kote baada ya kiasi kadhaa. Pia huwa na mikataba na nchi nyingi ili kuepuka na double- taxation.
 
Asante kwa kuleta post yenye mashiko. Halafu kuna watu humu JF wanataka tupishe katiba pendekezwa ambayo itaruhusu wizi na uhujumu wa uchumi wa nchi. Eti wakubwa waruhusiwe kufungua akaunti nje ya nchi as if wamemuona Cameroon, Obama, Merkel, Putin, Lee na wengineo wamefungua akaunti hapo NMB Bongo. Sijui nani ametuloga sisi Waafrika. Wakati mwingine tunawaza hovyo hovyo tu

Acha hao sutas wazipige tu hizo hela. maana ni fedha za wizi. Mwizi akiibiwa hakuna shida
 
Mafisadi wameshashtukia hilo ndio maana now days hawazipeleki uswis wanazikimbizIa mkomboz na badae wanagawana kwenye viroba.
 
Sioni sababu yoyote itakayomleta kiongozi wa nje kufungua account Tanzania hata kama wakiruhusiwa.

Sioni sababu ya kutomruhusu kiongozi au mfanyabiashara kufungua account nje hata kama unataka katiba isiruhusu.

Kama pesa alizochuma ni halali na zimelipiwa kodi, ni haki yake kuhifadhi pesa yake kokote duniani.

Pia, benki za nje hazifuati sheria za Tanzania. Sheria zinazofuatwa ni zile za mataifa tajiri. Hiyo ya katiba kutaka imnyime haki hiyo ni sawa sawa na kujaribu kumnyima Mtanzania uraia wa nchi nyingine; sijakutana na Mtanzania hata mmoja nje aliyokataa uraia wa nchi za kitajiri kwa sababu ya uzalendo au sheria zetu. Na wapo wengi tu waliorudi na uraia wa nje ila wameuficha.

Kumbuka, kutungwa sheria Tanzania hailazimishi nchi nyingine kuzifuata, hasa ukiwa masikini kama sisi.
 
Kwakweli si kosa kabisa kwenda kuweka pesa Uswisi, kila mtu ana uhuru wa kuweka pesa popote pale kulingana na mahitaji na utashi wake

Lakini bahati mbaya sana pesa ya kule kwa asilimia nyingi tu si pesa halali. Haiingii akilini mtu huna biashara zozote nje ya nchi. Ni kiongozi wa kisiasa au afisa serikalini au ni mfanyabiashara wa kawaida lakini Mara ghafla unapata usd million moja cash, pesa ya namna hii isiyo na maelezo yaliyonyooka pahala pake ni Uswisi hakuna 'kwere' wala usumbufu
Unawasiliana nao kupitia madalali wao waliotapakaa duniani kote fasta unasaidika
Pesa nyingi kule ni pesa chafu, pesa ya wizi, pesa ya kamisheni
 
We unafikiri pesa yako iliyoko CRDB haifanyiwi biashara? Unalipwa riba kiasi gani?
Sheria zinaruhusu Uswisi mtu yeyote kuwa na akaunti ya benki isiyo hata na jina, na wafanyakazi wa benki wanalazimishwa na sheria kuficha siri za mteja, na sheria inaweza kumfunga mtu anayetoa siri za mteja. Ni mazingira mazuri mno kwa mtu kuficha pesa chafu zisizolipiwa kodi. Pia pesa yao ni moja ya fedha zilizo stable zaidi duniani, hivyo hauna risk ya kushuka thamani, unaweza kufungua akaunti hata ya aina yoyote ya pesa, unaweza kufungua akaunti hata ukiwa hapa bongo bila kwenda popote unatuma tu vitambulisho, japo akaunti zisizo na majina utatakiwa kwenda mwenyewe. Kuhusu kutoa pesa umekosea Mshana, benki za Uswisi zinaruhusu mwenye pesa yake kutoa kiasi cha pesa kwa notisi ya siku kadhaa kulingana na kiasi unachotaka kuchukua, ukitaka kujaza kwenye magunia unaruhusiwa, ukitaka cheki ya wasafiri wewe mwenyewe tu hawana masharti.
Wezi wanaoweka pesa huko siyo wajinga, nyie mnaoliwa ndiyo wainga, mnataka waziweke hapa ili siku mkitaka mzitaifishe...thubutuuu! Pesa za Uswisi siyo kwamba hazitaifishiki, zinahitaji milolongo mingi sana, lakini inawezekana, tena mkitaka CASH mnapewa chash, siyo huduma.
 
Mafisadi wameshashtukia hilo ndio maana now days hawazipeleki uswis wanazikimbizIa mkomboz na badae wanagawana kwenye viroba.

hao madagaa tu na pesa za mboga, madili makubwa wala hawashiki cash.
 
We unafikiri pesa yako iliyoko CRDB haifanyiwi biashara? Unalipwa riba kiasi gani?
Sheria zinaruhusu Uswisi mtu yeyote kuwa na akaunti ya benki isiyo hata na jina, na wafanyakazi wa benki wanalazimishwa na sheria kuficha siri za mteja, na sheria inaweza kumfunga mtu anayetoa siri za mteja. Ni mazingira mazuri mno kwa mtu kuficha pesa chafu zisizolipiwa kodi. Pia pesa yao ni moja ya fedha zilizo stable zaidi duniani, hivyo hauna risk ya kushuka thamani, unaweza kufungua akaunti hata ya aina yoyote ya pesa, unaweza kufungua akaunti hata ukiwa hapa bongo bila kwenda popote unatuma tu vitambulisho, japo akaunti zisizo na majina utatakiwa kwenda mwenyewe. Kuhusu kutoa pesa umekosea Mshana, benki za Uswisi zinaruhusu mwenye pesa yake kutoa kiasi cha pesa kwa notisi ya siku kadhaa kulingana na kiasi unachotaka kuchukua, ukitaka kujaza kwenye magunia unaruhusiwa, ukitaka cheki ya wasafiri wewe mwenyewe tu hawana masharti.
Wezi wanaoweka pesa huko siyo wajinga, nyie mnaoliwa ndiyo wainga, mnataka waziweke hapa ili siku mkitaka mzitaifishe...thubutuuu! Pesa za Uswisi siyo kwamba hazitaifishiki, zinahitaji milolongo mingi sana, lakini inawezekana, tena mkitaka CASH mnapewa chash, siyo huduma.

Pamoja kuna baadhi ya sehemu umetumia lugha ya kukera lakini sio shida kwangu, nimeangalia zaidi kwenye hitimisho nilichokisema mimi ndio hichohicho ulichokirudia wewe, kuweka ni rahisi sana sio kutoa

Vile vile ishu ya kupewa cash kwenye viroba inawezekana kabisa wala si tatizo lakini hebu niambie baada ya hapo utatoka vipi na viroba vyako vya minoti mpaka nchini mwako!?

Kumbuka kuna sheria za kimataifa za kusafirisha pesa, zina milolongo mingi na maelezo mengi, usidhani utapewa viroba vyako upande navyo ndege kama begi la nguo

Watu wana mabilioni nje ya nchi lakini kila siku wanaumiza vichwa jinsi ya kuyaingiza nchini salama bila kukamatwa wala kushukiwa ndio maana kuna ishu za kutakatisha pesa kila siku zinaripotiwa
 
Hahahahaa, pole Mshana kama kuna Lugha imekukwaza, sijuwi ni ipi.
Kuhusu mahala pa kuzipeleka hizo pesa siyo juu ya benki, ni kama Tanzania tu ukishakabidhiwa pesa yako mule bulk cash imeshatoka kwenye hesabu ya benki ni juu yako kuilinda na kuisafirisha kwa njia unayoona inafaa. Kazi wala siyo kuingiza cash tanzania, hiyo ni kazi ndogo sana, hata ukinipa mimi kazi ya kuingiza kontena zima la pesa nipe miezi miwili tu nakamilisha kazi yako bila kupotea hata elfu kumi. Kazi ipo kwenye kuisafisha hiyo pesa, kuilipia kodi. Kwa vile ni pesa nyingi sana si kazi ndogo kuisafisha, hilo ndiyo linawaogofya watu mpaka wengine wanajikuta wanaingia mikataba isiyo na maandishi na wafanyabiashara, influence yako ikishuka anaweza kukuuza sekunde yoyote. Tanzania ina mazingira mazuri tu ya Wafanyabiashara wenye pesa chafu kusafisha pesa zao, lakini kuna nchi nzuri zaidi ya Tanzania zenye mazingira mazuri zaidi ya kusafisha pesa kiasi chochote, kwa public fuigure hawezi kujificha, lakini kwa mtu asiyejulikana analay low na kufanya mambo kimyakimya...saafi.
 
Back
Top Bottom