Kuficha pesa Uswisi, ujinga wa kiwango cha juu

Hahahahaa, pole Mshana kama kuna Lugha imekukwaza, sijuwi ni ipi.
Kuhusu mahala pa kuzipeleka hizo pesa siyo juu ya benki, ni kama Tanzania tu ukishakabidhiwa pesa yako mule bulk cash imeshatoka kwenye hesabu ya benki ni juu yako kuilinda na kuisafirisha kwa njia unayoona inafaa. Kazi wala siyo kuingiza cash tanzania, hiyo ni kazi ndogo sana, hata ukinipa mimi kazi ya kuingiza kontena zima la pesa nipe miezi miwili tu nakamilisha kazi yako bila kupotea hata elfu kumi. Kazi ipo kwenye kuisafisha hiyo pesa, kuilipia kodi. Kwa vile ni pesa nyingi sana si kazi ndogo kuisafisha, hilo ndiyo linawaogofya watu mpaka wengine wanajikuta wanaingia mikataba isiyo na maandishi na wafanyabiashara, influence yako ikishuka anaweza kukuuza sekunde yoyote. Tanzania ina mazingira mazuri tu ya Wafanyabiashara wenye pesa chafu kusafisha pesa zao, lakini kuna nchi nzuri zaidi ya Tanzania zenye mazingira mazuri zaidi ya kusafisha pesa kiasi chochote, kwa public fuigure hawezi kujificha, lakini kwa mtu asiyejulikana analay low na kufanya mambo kimyakimya...saafi.
Rene Jr bado ishu iko palepale kuzihalalisha ziingie kwenye mzunguko wa kawaida wa miamala ya pesa
Yani ni sawa na kutaka kuligeuza joka la kibisa liwe joka la mdimu
 
Last edited by a moderator:
Kwakweli si kosa kabisa kwenda kuweka pesa Uswisi, kila mtu ana uhuru wa kuweka pesa popote pale kulingana na mahitaji na utashi wake

Lakini bahati mbaya sana pesa ya kule kwa asilimia nyingi tu si pesa halali. Haiingii akilini mtu huna biashara zozote nje ya nchi. Ni kiongozi wa kisiasa au afisa serikalini au ni mfanyabiashara wa kawaida lakini Mara ghafla unapata usd million moja cash, pesa ya namna hii isiyo na maelezo yaliyonyooka pahala pake ni Uswisi hakuna 'kwere' wala usumbufu
Unawasiliana nao kupitia madalali wao waliotapakaa duniani kote fasta unasaidika
Pesa nyingi kule ni pesa chafu, pesa ya wizi, pesa ya kamisheni

Umeongea ukweli mtupu kwani benki kubwa mbili uswisi ni za wizi tu na wanaozipata kihalali pia ni wizi maana wanakwepa kodi kwa mfano David Bowie, Tina Turner, Phil Collins wote ni musicians lakini wamekwepa kodi na kuficha pesa zao Swiss.
Ukimsoma whistleblower Herve Falciani wa HSBC utaona mengi sana na siri kubwa ya swiss banks, kwanza wanaoweka pesa huko ni tax cheats, corrupt officials, mobsters, arm dealers, na dictators. Hakuna mwenye hela halali huko na bank haikuulizi umezipataje ila kwa kuwa wamebanwa sana na siri iliyojulikana duniani wameamuamua kufanya ngumu kufungua account huko. Na wao wanatoa namba na sio jina kama benki zingine kwa hiyo wasitudanganye eti wanawajua walioweka hela huko kama ni tarakimu labda kwani hiyo ni siri ya bank hata CEO hawezi toa details mpaka mwenye hela aidhinishe kutoa taarifa za mali zake
 
Hawa Waswisi wanajionyesha ulimwenguni kuwa ni wachapakazi na wanafanikiwa kwa jasho lao, kumbe ni wizi mtupu.

Sijui ulimwengu unalichukulia vip hili suala, maana linafahamika kuwa ni wizi

Hawalifichii macho wanajua ni bank walioitengeneza wao kwani hata Hitler kakuivamia Switzerland kwani aliitumia kujilimbikizia dhahabu na mali alizoziteka katika nchi zingine. Bank ya UBS ya Swiss ni ya 19 kwa utajiri duniani wao ukiwaambia nina almasi kibao wanakuja kuchukua na kukuwekea huo ni ukweli kwani siri hiyo imevujishwa na Falciani amesema huwa wanakwenda na kuhifadhi kwenye dawa za mswaki hizo almasi.
 
Rene Jr bado ishu iko palepale kuzihalalisha ziingie kwenye mzunguko wa kawaida wa miamala ya pesa
Yani ni sawa na kutaka kuligeuza joka la kibisa liwe joka la mdimu

Lakini angalau ziko salama na zinasafishika, zikiwa hapa haziko salama na ni ngumu kusafishika, na zikisafishika ni rahisi kutaifishika utapofikwa na majanga. Kwa hiyo aliyeweka hapa na aliyeweka Uswisi mjinga ni aliyeweka hapa.
 
Mmh haya kuficha si tatizo! Tatizo ni kwamba ni mali ya umma kwa ajili ya huduma za jamii, wanaofanya hivyo si wafanyabiashara ni viongozi wetu tuliowaamini tukawapa dhamana ya kuongoza HAPA NDIPO PENYE TATIZO
 
Kwa hiyo unashauri wafanyweje hao watu mkuu/
 
Sioni sababu yoyote itakayomleta kiongozi wa nje kufungua account Tanzania hata kama wakiruhusiwa.

Sioni sababu ya kutomruhusu kiongozi au mfanyabiashara kufungua account nje hata kama unataka katiba isiruhusu.

Kama pesa alizochuma ni halali na zimelipiwa kodi, ni haki yake kuhifadhi pesa yake kokote duniani.

Pia, benki za nje hazifuati sheria za Tanzania. Sheria zinazofuatwa ni zile za mataifa tajiri. Hiyo ya katiba kutaka imnyime haki hiyo ni sawa sawa na kujaribu kumnyima Mtanzania uraia wa nchi nyingine; sijakutana na Mtanzania hata mmoja nje aliyokataa uraia wa nchi za kitajiri kwa sababu ya uzalendo au sheria zetu. Na wapo wengi tu waliorudi na uraia wa nje ila wameuficha.

Kumbuka, kutungwa sheria Tanzania hailazimishi nchi nyingine kuzifuata, hasa ukiwa masikini kama sisi.
Huo ni uhujumu uchumi wa nchi yako, kama una pesa kweli na ni halali, weka ndani ya nchi, wananchi wapate fursa ya kuzikopa na kuzizalisha kwa njia hiyo utakuwa umechangia kuinua uchumi wa nchi yako. Wanakimbiza nje kwa sababu pesa zao ni chafu
 
Wewe huna haki wala serikali haina haki ya kuniamrisha nitumie vipi au niwekeze wapi fedha yangu.
Miaka hiyo imepitwa na wakati.

Pengine hujafundishwa darasani biashara za kimataifa au huwajui Watanzania wanaouza kahawa ya Kilimanjaro Japan, Vifaa vya kilimo Mayanmar, Mbao za Indonesia Australia, dawa za mifugo PNG na simu za Kichina Zimbabwe. Hujui mauzo ya nje yanalipwa vipi wala masoko yanatafutwa vipi.

Kuamini peke yake kuwa fedha za kila Mtanzania alizoziweka nje ni chafu bila ya kutoa kithibitisho chochote inaonyesha jinsi elimu yako ilivyo duni. Ubongo umejaa nazi za ujamaa mpaka umepitwa na wakati.

Biashara siyo Uzalendo, ni faida tu. Na fursa hazipo Tanzania peke yake. Ukifungua macho utaona.
 
Tokyo40 tuonyeshe weledi na hekima zetu katika kuchangia, tuepuke kutumia lugha ngumu na za kuudhi
 
Last edited by a moderator:
Wewe huna haki wala serikali haina haki ya kuniamrisha nitumie vipi au niwekeze wapi fedha yangu.
Miaka hiyo imepitwa na wakati.

Pengine hujafundishwa darasani biashara za kimataifa au huwajui Watanzania wanaouza kahawa ya Kilimanjaro Japan, Vifaa vya kilimo Mayanmar, Mbao za Indonesia Australia, dawa za mifugo PNG na simu za Kichina Zimbabwe. Hujui mauzo ya nje yanalipwa vipi wala masoko yanatafutwa vipi.

Kuamini peke yake kuwa fedha za kila Mtanzania alizoziweka nje ni chafu bila ya kutoa kithibitisho chochote inaonyesha jinsi elimu yako ilivyo duni. Ubongo umejaa nazi za ujamaa mpaka umepitwa na wakati.

Biashara siyo Uzalendo, ni faida tu. Na fursa hazipo Tanzania peke yake. Ukifungua macho utaona.

Mi nafikir ungetumia busara kumuelewesha mwenzio mambo ya ubongo yametoka wapi pia unachojua ww sio anachojua mwenzio mambo ya elimu ya nn tena??? Hata mwalimu huwa anazidiwa na mwanafunzi wake busara ndo kila kitu hapa unakutana na watu wa aina mbalimbali usiwe mwepes wa kupanic
 
Nimekuelewa Mkuu. Lakini mtu akinitusi kikanzu narudisha kombora mara mbili. Hii ni tabia yangu. Sina panic ya aina yoyote. Ninajiamini na ninachokiandika kila siku hapa.

Kila mtu anajifunza kitu hapa lakini kuna tabia ya wengi JF kukimbilia kuwaita watu wahujumu uchumi au mafisadi bila ya kuthibitisha. Inakera sana.
 
Ni kweli mkuu usibitisho ni muhimu sana ktk taarifa sio kuchafuana nakuunga mkono kwa hilo tuko pamoja sna.
 
Kuitwa muhujumu uchumi ni tusi pia kama huna kithibiti.

Basis naomba tusameheane tuu kwa faida ya jukwaa radika na Tokyo40 nafikiri mtanielewa katika hili. Bali kwa faida ya jukwaa naamini kuna mengine tutayasamehe
 
Last edited by a moderator:
Naongelea pesa za dili na si pesa halali, nina uhakika na ninachoongea KIWAVI, zingekuwa hivyo za Abacha, Mobutu na wengineo zingeenda kwa warithi wao tena bila zengwe! Hebu pitia post ya BAK hapo juu

waswiss wajanja sana. hawana mikwara kabisa unapotaka kufungua akaunti kwenye mabenki yao. hawana tatizo na sababu unazowapa za kufugua akaunti. hata ukiwaeleza kwamba unakwepa kodi nchini kwako wao hawana tatizo (waulize wamarekani wanajua hili na jinsi ilivyobidi kuwatolea macho waswisi mpaka wakakubali kutoa taarifa za wamarekani wenye akaunti uswiss).

unapofungua akaunti waswiss wanatakiwa wakushauri vitu unavyotakiwa kufanya ili pesa yako isipotee, lakini wao hawakwambii (hawanahuruma hata kama unaweka swiss frank 1000. tu. ndiyo elfu moja tu). msiniulize ni vitu gani unatakiwa kufanya sitaki kuwapa faida mafisadi. kwa vile mafisadi wetu pesa yao wanaweka kwa kificho basi wanakuwa hawamwelezi mtu mwingine na wala hawaulizi nini kifanyike iwapo watafariki ili warithi wao waupate mshiko (nadhani mafisadi hawaamini kwamba wanaweza kufa bila kuufaidi mshiko wao). hapo ndio wanaliwa.

benki za uswisi ni sawa na vituo vya polisi bongo "kuingia bure kutoka mpaka pesa", japokuwa wapo waingiao bure na kutoka bure. na benki za uswisi hivyo hivyo, kama pesa yako kubwa wanaweza ifuata mpaka kijijini kwako. kimbembe wakati wa kuitoa....
 
1427459770990.jpg
 
So unachotaka kutuaminisha katika hiyo thread yako ni kwamba hawa washenzi wa nchi hawana akili kiasi hicho kuweka pesa sehemu ambayo hawataambulia chochote......,!Huo ni uongo wa kutuhadaa ili tusahau.......!Na wasi wasi maybe na wewe unabenefit kwa namna moja au nyingine..........!
 
Umenisoma na michango ya wengine kabla hujachangia?
Umesoma post za BAK na Kafara? Chukua muda upite huko tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom