The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,778
- 8,232
Mtaalamu maarufu wa mustakabali wa teknolojia, Ray Kurzweil, ametabiri kuwa kufikia mwaka 2030, binadamu wataweza kuunganisha akili zao moja kwa moja na akili bandia (AI) kwa kutumia nanoboti, Virobiti vidogo vya kimitambo vinavyosafiri kupitia damu bila hitaji la upasuaji.
Kwa mujibu wa Kurzweil, nanoboti hizi zitakuwa na uwezo wa kufika kwenye sehemu ya ubongo iitwayo neocortex, ambayo ndiyo kitovu cha kumbukumbu, lugha, na maamuzi. Kupitia muunganiko huo, akili ya binadamu itaweza kuwasiliana moja kwa moja na mifumo ya akili bandia inayohifadhiwa katika wingu (cloud-based AI).
Teknolojia hii inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika maisha ya binadamu kwa kuongeza uwezo wa kumbukumbu, kasi ya kujifunza, na ubora wa maamuzi. Kurzweil anaeleza kuwa mtu ataweza kupakua ujuzi mpya moja kwa moja kwenye ubongo wake na kupata msaada wa akili bandia katika kuchakata taarifa kwa haraka.
Kurzweil, ambaye amewahi kutoa utabiri mwingi uliofanikiwa kuhusu maendeleo ya kiteknolojia, anaamini kuwa hatua hii itakuwa sehemu ya mapinduzi ya kihistoria ambapo akili ya binadamu itapanuliwa kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
✍️