Wapi inaashiria hajamaintain peace, ninakula na kubweteka na kulala salama. Mambo ya maandamano hayawezi kunikosesha usingizi, cha msingi ni wale wanaoandamana watii sheria na kuheshimu haki za wale ambao hawajajihusisha. Nao pia polisi waheshimu sheria na wasiwachokoze waandamanaji, hapo ngoma itakua safi. Nairobi leo wameandamana mjini, hapakua na vurugu zozote.
Binafsi nimewahi husika kwenye maandamano, ninachojua ni kwamba, pale unampiga kwa jiwe polisi aliyejihami kwa bunduki, ukumbuke huyo ni binadamu na ana hisia zake, anaweza akaamua kuvumilia uchungu wa mawe yako, au afanye maamuzi ya hasira na kutumia bunduki yake dhidi yako. Hapo rais wa nchi hatakua amehusika kwa chochote kitakachotokea baina yako na huyo polisi.
Kwangu mimi naomba Uhuru ajaribu kila iwezekanavyo kuwasihi polisi wawe wavumilivu ili kutunza amani. Na aendelee na kuboresha nchi kiuchumi, tutakapopiga kura, yangu ataipata asubuhi mapema, ila ikitokea ameshindwa, asithubutu kung'eng'ania kama mnavyofanya huko kwenu, akubali kushindwa na kwenda kijijini kulima ili tumkaribishe rais mpya atakayekua ameshinda, tumpe ushirikiano na kuendelea kupiga hatua kimaendeleo.