Kufikia sasa maandamano Nairobi yamekua ya amani leo

Mkianza kuchinjana Baba Jesca atawaamulia. Msijali.
Baba Jesca awe ndio mpatanishi wa Kenyatta na Raila!!?. Hapo Kenyatta atakuwa haamini kila anachoelezwa, atakuwa anajua anapigwa changa la macho!
 
Sote twaomba Kenyatta na Polisi wawe na hayo maono!
 
Kwa hali ilivyo huyo Bwana M7 anakubalika pande zote za huo mgogoro
M7 atakua anamcheka Uhuru anamwambia, hii ni nini unafanya. Mbona unacheza cheza na huyu mtu.... this guy is disrespecting you.... hebu uliza kiza besijye
 
Kama hali ni hiyo wamtafute Mkwere!

Nakuunga mkono mkuu......Nguvu pamoja na level aliyo nayo Raila ni kubwa kushinda viongozi wa upinzani wengi Afrika.......Nijuavyo pia siasa za Kenya na Uganda wapi na wapi???......KATIBA NI MPYA, MAHAKAMA KUU ZAIDI INA NGUVU NA UHURU.
Kenyatta akithubutu ya Museveni ataingia kichakani.
 
Sote twaomba Kenyatta na Polisi wawe na hayo maono!

Dunia nzima yaitazama polisi wa Kenya, watetezi wa haki za kibinadamu (UN Human Rights Commission) pamoja na ICC....Kenyatta kesha sahau.....vifo vya raia vitapelekea mashtaka dhidhi ya serikali ya kihuni ya Kenya.
Tayari mataifa yenye nguvu yana zungumzia uwezekano wa polisi wa Kenya kuzuiwa kununua vifaa(yaani equipments/ammunition sanctions),huku niliko.
 
Sote twaomba Kenyatta na Polisi wawe na hayo maono!

Dunia nzima yaitazama polisi wa Kenya, watetezi wa haki za kibinadamu (UN Human Rights Commission) pamoja na ICC....Kenyatta kesha sahau.....vifo vya raia vitapelekea mashtaka dhidhi ya serikali ya kihuni ya Kenya.
Tayari mataifa yenye nguvu yana zungumzia uwezekano wa polisi wa Kenya kuzuiwa kununua vifaa(yaani equipments/ammunition sanctions),huku niliko.


Naomba niwa taarifu kuwa nguvu hizo zatokana na ufuasi alio nao....ikumbukwe kuwa Odinga alipata kura karibia nusu kwa nusu na mpinzani wake ,wakati huo Kenyatta ...yaani almost 50% to 50%.....Nusu ya wakenya wote wanampenda kwa hiyo ana nguvu kama za raisi Kenyatta kwenye mioyo ya raia wa nchi hiyo......pia nguvu za raisi zilipunguzwa kikatiba pamoja na upinzani kuwa na nguvu zake zenyewe kwenye katiba ya nchi hiyo tukufu.
 
Tuwaombee polisi na Kenyatta ili Muumba awajaze busara na hekima katika kuivusha Kenya katika hili janga.
 
Ila watu weengi tunasahau kwamba kwenye hii sinema yupo Bwana Ruto, yeye anajifanya kama hahusiki lakini ndie mratibu mkuu wa hili jambo. Kenyatta ni mtu msikivu lakini Rutto ni mjivuni sana na ana mambo ya utesi. Tafadhalini Wakenya hebu tupieni jicho kwa huyo Bwana Rutto.
 

Bwana wee waijua Kenya kwa undani , wacha tu!....na hilo la jitu hilo Ruto haliitaji mtu kuambiwa.....ana roho chafu nyeusi kupindukia...mithili ya mkaa....pamoja na DHARAU NA KIBRI .ndiye aliyekataa mazungumzo wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 Kenya, akiwa upande wa ODM wakati huo, ni yeye aliyekasirika aliposikia Odinga amekubali kuzungumza na Kibaki.....anahusishwa pia na kupanga mauaji mkoa wa Bonde La Ufa......pamoja na kushitakiwa kule ICC.
Nionavyo mimi huenda ni yale yale tu!....labda kamkataza Kenyatta kuongea na upinzani kutatua mgogoro huu.....chaka tofauti nyani ni yule yule.
Nakubaliana nawe kuwa Kenyatta hupenda mazungumzo/usikivu.

Do you see the pattern here?...kila aliko kuna kauli za roho ngumu ngumu.....nuksi jamaa huyu.
 
Muda mwingi sana napenda kuangalia vipindi vya TV za Kenya. Unajua Wakenya wengi hawapendi hii hali ila kuna huyo Bwana Ruto, yupo kwenye kila aina ya uchafu uanaotekea Kenya.
JK alimuelewa mapema na ndio maana hakupata shida katika upatanishi. Alitaka kushinikiza awepo mezani, JK akamkatalia. Mazungumzo yakafanyika na maelewano yakawepo bila kinyongo kwa pande zote zilizokuwa kwenye huo mgogoro.
 

Habari ndiyo hiyo!

Tumuombe Mungu Kenyatta awe na hekima aanzishe mazungumzo mara moja,sioni hasara yoyote kwake na kwa upande wa upinzani.....ni lazima pande zote mbili ziwe na imani na tume ya uchaguzi(IEBC) kama "referee".
Bila hivyo itakua mchezo wa kujidanganya kwenye mambo bandia.....alivyosema mwanamziki maarufu wa Burundi, Kidum.

Bila marekebisho haya ya tume hili tukutu, hakutakua na uchaguzi(upinzani utasusia) ama kutakua na machafuko yatakayoimaliza nchi hiyo mara ya mwisho milele haswa jinsi Kenyatta anavyotumia askari wake katili.

Kwaheri kaka!
 
Kibe
Kibera na mathare sio Nairobi..!?
 
Tuwaombee polisi na Kenyatta ili Muumba awajaze busara na hekima katika kuivusha Kenya katika hili janga.

KWEZISHO
Ninachojua ni kwamba wana siasa wote wana undugu na shetani na hakuna mzuri. Hata huyo Raila ilibidi maafa ya watu zaidi ya elfu wafe ndio anufaike na cheo cha uwaziri mkuu. Na ndio hapo chanzo cha uadui wake na bwana Ruto, maana Ruto alituhumiwa kuwaua watu wengi na kuzichoma nyumba na makazi, ila hatimaye aliyenufaika zaidi ni huyo Raila, halafu Ruto akawa anataka afanye ufisadi kiholela, kitu ambacho Raila aligoma kumuachia.

Yeye Ruto alitaka awe na uhuru wa kuiba kabisa, maana ufisadi ulikua unatajwa kwenye ofisi ya Raila, kama vile wizi wa hela nyingi zile za mradi wa Kazi kwa Vijana, hivyo Ruto nahisi alitaka naye apate fursa ya kuiba maana alihusika pakubwa katika kumuwezesha Raila awe waziri mkuu. Kama Ruto asingewaua watu hivyo, Kibaki (ambaye naye ni mwanasiasa mwenye roho ngumu kama shetani) asingekubali kugawana madaraka na Raila.

Hata haya yanayotendeka kwa sasa, nina uhakika asilimia zaidi ya 100%, Raila angelitaka yawe na machafuko zaidi, watu wafe hadi Uhuru akubali kumpa anachotaka. Hili la maandamano ya amani anajua vizuri hayawezi kubadilisha chochote, wataishia kuimba nyimbo mjini na kurudi manyumbani kila jioni. Uhuru na Ruto nao pia kama wanasiasa, wana roho ngumu pia na watagoma hadi mwisho. Hakuna mwanasiasa mzuri zaidi ya mwenzie, asikudanganye mtu.

Raila tayari amekutana na Uhuru ikulu na akaorodhesha mambo anayoyataka ni zaidi ya hilo la IEBC, hivyo hapo patakua patamu, lazima vurugu zitendeke hapa maana hamna namna. Naiombea nchi yangu sana, hawa viongozi wapunguze ushetani na waige kwa viongozi kama akina Lowassa kuweka taifa mbele
Nimeanzisha mada nyingie inayohusu hili huku Yaliyojiri kwenye kikao cha rais Uhuru na Raila kule ikulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…