SoC04 Kufikia Tanzania tuitakayo: Uwajibikaji mzuri wa Viongozi na Matumizi mazuri ya Rasilimali

SoC04 Kufikia Tanzania tuitakayo: Uwajibikaji mzuri wa Viongozi na Matumizi mazuri ya Rasilimali

Tanzania Tuitakayo competition threads

Hopper lyfer

New Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
4
Reaction score
4
Tanzania Ni Nchi ambayo imebahatika kuwa na Kila kitu hivyo

1: Uwajibikaji mzuri wa Viongozi
Tanzania ni nchi mojawapo ambayo inatumia demokrasia katika kuongoza, hivyo viongozi wanaichaguliwa ni vizuri wakawa wawajibikaji zaidi na kuwa wabunifu katika kuhakikisha Wanatenda vyema Yale yote ambayo wananchi wanayategemea kutoka kwao Kwa kuwa Wawazi, wachapakazi, watatuzi wa matatizo ya wananchi, wenye kuepuka uchu wa madaraka hususani katika matumizi ya fedha wanazopewa na serikali katika kutimiza miradi mbalimbali.

Matumizi ya Fedha za bajeti zinazotolewa kutimiza miradi mbalimbali kama zitatumika vizuri bila upigaji na ufujaji wa Mali za serikali basi tunaweza kuijenga Tanzania ambayo ni ndoto ya Kila mtu na Kila Mtanzania atafaidi mema ya nchi Kwa uwajibikaji wa viongozi na sambamba na Hilo kuwe na ufuataji wa sheria na katiba ya nchi Kwa viongozi wowote watakaoendana kinyume nao bila kupindisha ukweli Kwa maslahi ya watu wachache ambao wanairudisha maendeleo Nyuma Kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe pamoja na matumbo Yao.

Pia viongozi waache utegemezi kutoka mataifa ya nchi zilizoendelea hivyo wawe wabunifu katika kutatua changamoto zinazohusu Uchumi katika Taifa letu na sio kuwa na mawazo hafifu na kushindwa kutatua baadhi ya changamoto zinazowahitaji wao kuzitatua mpaka Watafute msaada kutoka nje Pia viongozi wawe wazalendo na wenye uchungu Kwa Taifa letu kupitia uzalendo huo tutaandaa viongozi wenye ujasiri na uthubutu wa kufanya makubwa ndani ya nchi yetu katika kuleta maendeleo makubwa ya Tanzania.


2: Matumizi mazuri ya rasilimali
Tanzania ni nchi mojawapo iliyojaliwa utajiri wa rasilimali za kila aina, hivyo rasilimali hizo zitumike katika kuimarisha uchumi wa nchi na siyo Kwa watu wachache tu ambao wameshikilia bomba.

Na pia kusiwe na upangiwaji wa matumizi wa rasilimali zetu kutoka Kwa nchi zilizoendelea Kwa kutaka rasilimali zetu Kwa manufaa ya nchi zao, hivyo kuwekwe sheria mpya na Kali ambazo zitalinda rasilimali zetu zisiweze kuibiwa na watu wa mataifa mengine mfano. Tanzania imebarikiwa madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana Tanzania pekee lakini Cha kushangaza kupitia madini hayo ya Tanzanite tumejikuta Tanzania tukiwa wazalishaji namba tatu wa madini hayo jambo ambalo linatupa mkanganyiko kama watanzania.
Kupitia madini, vivutio na rasilimali zote zilizopo Tanzania zikitumika vizuri tunaweza kuijenga Tanzania ambayo ni ndoto ya Kila mtu na iliyomema Kwa vizazi vyetu vya baadae.
 
Upvote 2
Tanzania Ni Nchi ambayo imebahatika kuwa na Kila kitu hivyo

1: Uwajibikaji mzuri wa Viongozi
Tanzania ni nchi mojawapo ambayo inatumia demokrasia katika kuongoza, hivyo viongozi wanaichaguliwa ni vizuri wakawa wawajibikaji zaidi na kuwa wabunifu katika kuhakikisha Wanatenda vyema
Ewaaah!, tunakubaliana kabisa. Tuko na kila kitu na tunachohitaji kama taifa ni uwajibikaji wa kila mtu. Kila anayelipwa kukifanya kitu fulani na akifanye na asipokifanya basi awajibishwe ova.

Pia viongozi waache utegemezi kutoka mataifa ya nchi zilizoendelea hivyo wawe wabunifu katika kutatua changamoto zinazohusu Uchumi katika Taifa letu na sio kuwa na mawazo hafifu na kushindwa kutatua baadhi ya changamoto zinazowahitaji wao kuzitatua mpaka Watafute msaada kutoka nje
Umeenda vizuri kwa hatua zote. Hatua ya kwanza ilikuwa kujitambua na kutambua uwezo wetu, na ya pili ni kuutumia huo uwezo wetu kama Taifa. Tanzania tuitakayo. Ahsante.
 
Back
Top Bottom