tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,854
- 1,129
Mkuu,suala la kufilisika linategemea sana na muundo na historia ya jamii.Ukiangalia jamii za wenzetu ,nikimaanisha wenzetu wa Asia,bara arabuni,america na ulaya zipo koo ambazo zimekuwa consistently tajiri kwa vizazi vingi hata zaidi ya vitano (old money).Jamii hizi zimejijengea uwezo mkubwa wa:
1.-kuheshimu utajiri
2.kuweka akiba
3.kutokutumia zaidi ya kipato chao,hata kiwe kikubwa vipi.
hizi tabia wamezipandikiza kizazi hadi kizazi.
Turudi kwa wabongo:
wenzetu wahindi na waarab wamekuwa wafanyibiashara miaka mingi na Nyerere aliwapa fursa ya kuendelea na utaratibu wao,na mpaka leo wako bomba,wakiishi Upanga na kushea apartment tunawacheka kumbe ndo kutengeneza savings,nywele ngumu tuliambiwa na Mwalimu kuwa 'ubepari ni unyama' tukakubali tukaishia aidha kuishi kwa mshahara au kuwa wakulima.
Ogopa limbukeni anayeibuka ghafla,Mzee Mwinyi ndo alitufungulia milango ya kushika hela,kwa ushamba wetu ndo maana yanatokea hayo uliyosema hapo juu.
Mkuu it is only a matter of time na sisi nywele ngumu tutajifunza namna ya kuheshimu na kutunza hela,haya mambo ya kupata hela kila mwanamke Dar ukamnunulia rav4 tutaacha.
Mkuu umenifanya nikumbuke watu waliokuwa waliokuwa wana pesa za kutosha, sasa hivi mpaka unawaonea aibu, wengine bado wana maisha ya mazuri tu. Lakini ukikumbuka maisha yake ya kipindi cha nyuma yalivokuwa, unajuaa kabisa huyu anatembelea rim.Wakuu mara nyingi hili jambo huwakuta watu wengi. Kuna wanaodai mali ya dhuluma lazima ije kupotea kabisa japo wapo wenye kupata mali kihalali na wanafilisika. Mimi nimemshuhudia jirani yetu ambaye alikuwa na pesa nyingi sana miaka ya 90, wakati huo alikuwa akifanya biashara za Zambia. Yule jirani alikuja kufilisika kabisa..na hakuweza kurudia hali ya mwanzo mpaka sasa. Je wewe umekutana na watu wa aina hiyo/umewahi filisika? Je sababu hasa huwa ni nini? Inawezekana mali ya halali na uliyotafuta mwenyewe, ikaisha na ukashindwa kunywa hata chai? Tukienda kwa mifano naamini tutajifunza mengi, hasa kwa tunaoyaanza maisha. NB: Masikini huwa hafulii
mmu.........
Jamani hivi unaweza kutenganisha pesa/utajiri/kufilisika na mapenzi,mahusiano na urafiki? they are interwined,hivyo acha mada hii tuijadili hapa hapa maana hakuna kinachovunja nyumba/mahusiano kama kufilisika.Jukwaa hili sio husika kwa habari hii.
ashakosea, kilichobaki ni mods wa move sredi hii sehemu inayostahili.
Jamani hivi unaweza kutenganisha pesa/utajiri/kufilisika na mapenzi,mahusiano na urafiki? they are interwined,hivyo acha mada hii tuijadili hapa hapa maana hakuna kinachovunja nyumba/mahusiano kama kufilisika.
Jukwaa hili sio husika kwa habari hii.
ashakosea, kilichobaki ni mods wa move sredi hii sehemu inayostahili.
Mimi niko tofauti kidogo! Angalia umepigana toka chini hadi umefika juu. Hapo ndo unakuta kila ndugu anakuja kuomba msaada na hizi tabia zetu za kuoneana aibu! basi unaanza kusaidia kila kichwa. Kwa nini usifilike? Kwa hiyo extended family, tamaduni zetu, namna ambavyo tusivyojua kuongeza faida kutokana na mikubwa tunayokuwa nayo ni matatizo makubwa yanayowakumba watu ambayo hupelekea kufilisika.
Ahsante kwa maada nzuri.
sasa kuna mana gani ya kuwa halafu husaidii ndugu?Mimi niko tofauti kidogo! Angalia umepigana toka chini hadi umefika juu. Hapo ndo unakuta kila ndugu anakuja kuomba msaada na hizi tabia zetu za kuoneana aibu! basi unaanza kusaidia kila kichwa. Kwa nini usifilike? Kwa hiyo extended family, tamaduni zetu, namna ambavyo tusivyojua kuongeza faida kutokana na mikubwa tunayokuwa nayo ni matatizo makubwa yanayowakumba watu ambayo hupelekea kufilisika.
Ahsante kwa maada nzuri.
naomba nijue, hivi kufulia/kufilisika pia hutokana na kupata hasara katika biashara, if yes mbona hiyo ni hali ya kawaida kabisa katika biashara, in business it is obvious that profit or loss is inevitable but businessman always strive for profit
kwa hiyo kuna maana gani kama unakuwa na hela halafu husaidii ndugu zako? To me is Stupid!
sasa kuna mana gani ya kuwa halafu husaidii ndugu?