tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,854
- 1,129
Wakuu mara nyingi hili jambo huwakuta watu wengi. Kuna wanaodai mali ya dhuluma lazima ije kupotea kabisa japo wapo wenye kupata mali kihalali na wanafilisika. Mimi nimemshuhudia jirani yetu ambaye alikuwa na pesa nyingi sana miaka ya 90, wakati huo alikuwa akifanya biashara za Zambia. Yule jirani alikuja kufilisika kabisa..na hakuweza kurudia hali ya mwanzo mpaka sasa. Je wewe umekutana na watu wa aina hiyo/umewahi filisika? Je sababu hasa huwa ni nini? Inawezekana mali ya halali na uliyotafuta mwenyewe, ikaisha na ukashindwa kunywa hata chai? Tukienda kwa mifano naamini tutajifunza mengi, hasa kwa tunaoyaanza maisha. NB: Masikini huwa hafulii