Kufilisika a.k.a kufulia......


Kusaidia kivipi?

Kama unasaidia ili jamaa yako aweze kujitegemea baadae ni vizuri,lakini kama unasaidia ili watu wakusifu tu mitaani huku wewe ukiteketea na nduguyo unaye msaidia anadumaa ni uzembe.

Fundisha mtu kuvua samaki, mpe nyavu, kisha mpige ban asikanyage kwako tena kuomba omba. Huo ndio msaada, kinyume na hivyo ule mzunguko wa ulofa unaongezeka ktk jamii yako.
 

Kwangu mimi kufilisika kupo but sio lazima ufulie na kushindwa kunywa chai. Matajiri wakubwa, huko ughaibuni na hata hapa Tanzania wanatumia kufilisika "bankrupt" kama stratergy ya kukwepa madeni wanayodaiwa.Kwa mfano kampuni ya Scandinavia Express ilipooona inashindwa kulipa madeni baada ya kila mtu kuchukua chake ikadeclare "bankrupt" na hivyo kuingia unnder receivership. Nini kilitokea??

Jamaa (shareholders) wapo osterbay wanakula kuku kwa mrija, na kampuni mpya "GREEN STAR" inaoperate kama kawaida(wanasema ya mdogo mtu) .The same wine but different bottle. Na huu ndio uzuri wa kuincorporate a Limited Liability Company, kwani kisheria mali za kampuni ni tofauti za washikadau wake mmoja mmoja. Sasa hapo looser ni nani? Bank au Scandnavia?. Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini wahindi wanabadilisha majina sana? WAKE UP PEOPLE

Poor Tanzanians, wengi bado tunapambana na sole propriatorships & firms. Wakati hali ibiashara ikibadilika hata pa kulala utakosa kwa sababu ya kufidia madeni, na hata ukisema umefilisika bado asset zako binafsi zitafidia madeni (lets join this conspiracy of the rich). Halafu hawa matajiri huwa very smart. Wanatenganisha kila kitu kwa kuoutsource, kwa mfano ownership ya Yard, na baadhi ya operation kama Cargo Transportation zilikuwa outsourced kwenye kampuni nyingine (wanazomiliki wao wenyewe) mwisho wa siku wakisema wamefilisika hizo operation wanabaki wakizimiliki kwani hazikuwa sehemu ya Kampuni husika.

Hii stratery ipo kisheria, na wajanja wanaitumia kwa faida yao. Usihadaike kumuona Mtu alikuwa na hela nyingi na ghafla akasema amefilisika, just wait for his the greatest comeback. Ingawa wenzangu na mimi wakesema wamefilisika ndio for good kwa namna wanavyokuwa wamestructure biashara zao lazima wapoteze kila kitu

Tuamke watanzania, tutumie sheria zetu kwa faida yetu
 

Ha haa haaaa nice one.
 

Ni kweli rafiki yangu nakubaliana na wewe inatokea tu huruma na utu inabidi kusaidiana,lakini kwa upande mwingine rafiki yangu hawa wenzetu waasia wao nao wanatabia ya kubebana kwa mfano kuna koo kama wakina sijui Gulam,dewji na wengine wengi unakuta ukoo mzima matajiri kwa hiyo hata mtu wa kusaidia ndani ya ndugu zao hamana.
Hawa jamaa wana style wanayotumia ambayo ni nzuri sana naona wachaga wameanza kuitumia kidogo kidogo lakini hawatafanikiwa kwa kiwango kikubwa nitaelezea hapa chini kwa nini.Style yenyewe ni ya kuwezeshana kibiashara.
Natoa mfano umeenda kwenye duka la mhindi unataka shati au suruali akiona inalipa na kama hana atapiga pass kwa ndugu yake kama ndugu yake hana atapiga pass kwa jamaa yake wa asili hiyohiyo ya kiasia.Style hii ni nzuri sana ambayo wachaga wameanza itumia na inawapeleka mbele.

Kitu kingine ambacho ni kikubwa hawa waasia wamefanikiwa sana kujijengea uaminifu,kwa kweli sio uongo kwa hawa wenzetu waasia ukimpa mzigo akuuzie akikuambia baada ya wiki mbili uje chukua hela kama ukienda utapata hela yako kama hamna hela atakurudishia mzigo wako huo ni mfano,hii uaminifu imewapa umaarufu sana wahindi vigogo wengi biashara zao wakakimbilia kuingia share nao hii ndio imewachangia kuwaweka stable.Hapo tofauti na wenzetu wachaga uaminifu hamna ndio maana nikasema hawa jamaa hawatafika mbali kufilisika kutakua kama kawa.
 

Na hicho ndicho huwa nafanya!! Lakini mtu mwingine anamsaidia mtu mlo wa siku 7, ukiisha anarudi tena!! hiyo haisaidii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…