Wakuu mara nyingi hili jambo huwakuta watu wengi. Kuna wanaodai mali ya dhuluma lazima ije kupotea kabisa japo wapo wenye kupata mali kihalali na wanafilisika. Mimi nimemshuhudia jirani yetu ambaye alikuwa na pesa nyingi sana miaka ya 90, wakati huo alikuwa akifanya biashara za Zambia. Yule jirani alikuja kufilisika kabisa..na hakuweza kurudia hali ya mwanzo mpaka sasa. Je wewe umekutana na watu wa aina hiyo/umewahi filisika? Je sababu hasa huwa ni nini? Inawezekana mali ya halali na uliyotafuta mwenyewe, ikaisha na ukashindwa kunywa hata chai? Tukienda kwa mifano naamini tutajifunza mengi, hasa kwa tunaoyaanza maisha. NB: Masikini huwa hafulii
Kwangu mimi kufilisika kupo but sio lazima ufulie na kushindwa kunywa chai. Matajiri wakubwa, huko ughaibuni na hata hapa Tanzania wanatumia
kufilisika "bankrupt" kama stratergy ya kukwepa madeni wanayodaiwa.Kwa mfano kampuni ya Scandinavia Express ilipooona inashindwa kulipa madeni baada ya kila mtu kuchukua chake ikadeclare "bankrupt" na hivyo kuingia unnder receivership. Nini kilitokea??
Jamaa (shareholders) wapo osterbay wanakula kuku kwa mrija, na kampuni mpya "GREEN STAR" inaoperate kama kawaida(
wanasema ya mdogo mtu) .The same wine but different bottle. Na huu ndio uzuri wa kuincorporate a Limited Liability Company, kwani kisheria mali za kampuni ni tofauti za washikadau wake mmoja mmoja. Sasa hapo looser ni nani? Bank au Scandnavia?. Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini wahindi wanabadilisha majina sana? WAKE UP PEOPLE
Poor Tanzanians, wengi bado tunapambana na sole propriatorships & firms. Wakati hali ibiashara ikibadilika hata pa kulala utakosa kwa sababu ya kufidia madeni, na hata ukisema umefilisika bado asset zako binafsi zitafidia madeni (
lets join this conspiracy of the rich). Halafu hawa matajiri huwa very smart. Wanatenganisha kila kitu kwa kuoutsource, kwa mfano ownership ya Yard, na baadhi ya operation kama Cargo Transportation zilikuwa outsourced kwenye kampuni nyingine (
wanazomiliki wao wenyewe) mwisho wa siku wakisema wamefilisika hizo operation wanabaki wakizimiliki kwani hazikuwa sehemu ya Kampuni husika.
Hii stratery ipo kisheria, na wajanja wanaitumia kwa faida yao. Usihadaike kumuona Mtu alikuwa na hela nyingi na ghafla akasema amefilisika, just wait for his the greatest comeback. Ingawa wenzangu na mimi wakesema wamefilisika ndio for good kwa namna wanavyokuwa wamestructure biashara zao lazima wapoteze kila kitu
Tuamke watanzania, tutumie sheria zetu kwa faida yetu