Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Watu 19 wamefariki na 26 kuokolewa kwenye ajali mbaya ya ndege huko Bukoba.Innaa Lilaahi wainna ilayhi raajiuun.
Kwanza ni wazi kuwa ni ajali iliyotokana na mipango ya Mwenyezi Mungu.Shirika la ndege na rubani hawana cha kulaumiwa.Zaidi ni kuwa rubani kwa haraka kabla uchunguzi anaweza akasifiwa kwa kujaribu kuokoa maisha na hatimae kujiokoa mwenyewe bila mafanikio.
Wavuvi walioshiriki kuokoa ni watu wa kupewa nishani na si zawadi ya shilingi milioni 1 tu.
Hata hivyo kuna sehemu inaonekana tujifunze ili ikitokea tusirudie makosa. Kwanza ni namna za uokoaji ulivyochukua muda mrefu na kutumia vyombo hafifu.
Kwa vile ndege ilikuwa imezama baharini na upande wa marubani kuzama zaidi ilikuwa haitakiwa kuikokota majini kwa madau na kamba kama kwamba nayo ni boti.
Kilichotakiwa ilikuwa helikopta za kuokoa ziinue kidogo na huku ikikokotwa na kamba kama ilivyofanyika.Hii ingelisaidia ndege kutoendelea kuvujisha maji na kuwafikia abiria na marubani ambao walikuwa hai mpaka muda huo.
Ndege wakati imezama majini lakini bado kuna sehemu watu wanaonekana wamesima juu ya mabawa na mgongo wake wakiwa na nia nzuri ya kuokoa.
Hili halikupaswa kutokea kwani kwa kufanya hivyo ndio walikuwa wanazidisha kuizamisha badala ya kuipa nafasi kuelea.