Kufuatia Upotoshaji Unaofanywa: Naomba kutoa Elimu kuhusu Mihimili mitatu ya Dola

Kufuatia Upotoshaji Unaofanywa: Naomba kutoa Elimu kuhusu Mihimili mitatu ya Dola

Pole sana Mkuu. Umeishia kupewa Elimu wewe. Unapaswa kuwashukuru wote waliokuelimisha. Jifunze kufikiri kabla ya kutenda. Nafikiri umenielewa.
 
Unapotoka hadharani na kudai unataka kutoa Elimu kwenye jukwaa kama hili basi matarajio ya watu ni kupata Elimu hiyo kwa kiwango stahiki.
Ukitaka watu watoe maoni yao juu ya kile ukichokiandika basi Ungesema unaomba kutoa maoni yako juu ya mihimili hiyo na sio kutoa Elimu ambayo hauna ujuzi nayo na mwisho hapo hukutoa Elimu kama ulivyodai ila ulitoa ushabiki wako juu na kile unaamini.
Sawa. Wapi nilipokosea?
 
Umeandika utopolo..yaani wewe unaona executive iko juu ya bunge hivo unaona sawa hata kama serikali ikasign mkataba wa kuuza nchi au rasilimali Bila bunge ni sawa?

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Umeelewa vibaya. Sina mahali nilipoandika kuwa executive iko juu ya bunge bali niliainisha majukumu ya kila mhimili.

Nimesema kuwa wakati serikali inapokuwa inaingia mikataba mbalimbali HAILAZIMIKI kulishirikisha bunge
 
Wewe utakuwa ni mlinzi wa ile kampuni iliyojenga uwanja wa chato
 
Ukimsikiliza mpinzani halafu ukasome sheria atayokutajia unakuta ni vitu viwili tofauti kabisa,

Inakupasa kuwa makini mno na hawa watu au la utaingia chaka.
 
Huyo mbadhirifu wenu mwaka huu hachomoki.
Ana makandokando kama yote.

Lissu ni lazima atinge ikulu tarehe 28 Oktoba 2020.
Sawa ila hujajibu hoja. Maneno yamekuwa mengi kuwa mikataba ni ya siri na kuwa bunge lilitakiwa lishirikishwe kwenye uingiwaji wake. Mimi nimeandika hapo kuwa sio LAZIMA bunge kushirikishwa. Wee unasemaje?
 
Pole sana Mkuu. Umeishia kupewa Elimu wewe. Unapaswa kuwashukuru wote waliokuelimisha. Jifunze kufikiri kabla ya kutenda. Nafikiri umenielewa.
Nimekuelewa sana mkuu. Kwakweli kujifunza ndio kunatufanya tuwe watu bora zaidi kila siku na napenda kujifunza ila bahati mbaya sijaona hicho ninachofundishwa hapa. Unaweza kuniambia nimefundishwa nini? Kuna yeyote akiyejibu hoja zangu zaidi ya kuonesha dharau na kebehi? Unajuaje kuwa wso ndio wa kujifunza kwenye hili?

Hiyo haki, Uhuru na maendeleo mnayohubiri ndio haya?
 
Magreti thinka humu ni wachache sana. Hakuna siku utapata mtu akakuchalenji ukaona kweli hapa ninachakujifunza kuwa niliteleza. Vijana wachadema maoni yao utasikia

Mpumbavu
Utopolo
Weka namba ya simu
Umeandika ujinga

Yaani hii inaonesha ni aina gani ya wanachama waliopo huko.


Inasikitisha ngoja niendelee na huu utafiti
 
Waungwana,

Kwa kipindi kirefu wapinzani wamekuwa kwa kujua au kutokujua wanapotosha umma Kuhusu kazi na wajibu wa mihimili mitatu ya dola yaani serikali, bunge na mahakama.

Serikali kazi yake ni kuendesha shughuli za kila siku za nchi, bunge kutunga sheria na kuisimamia serikali wakati mahakama inakazi ya kutafsiri sheria.

Kazi ya kuingia mikataba ni kazi ya serikali na hakuna ulazima wa kulitaarifu bunge wakati wa kuingia mikataba hiyo.

Kama bunge linaona kuna shida kwenye mkataba fulani basi linaitaka serikali kupeleka mkataba huo, kujadili na mwisho kutoa maamuzi. Mbunge binafsi pia ana haki ya kuitisha mkataba wowote ilimradi tuu akidhi matakwa ya kisheria

Waulizwe wapinzani, haya wanayolalamikia kuwa ndege, uwanja wa ndege na mengine kuwa mikataba yake haikupita bungeni, tatizo liko wapi? kwangu mimi ni sahihi na hakuna sheria iliyovunjwa hapo.

Wapinzani wanatumia kigezo cha uvivu wa baadhi ya watanzania kujisomea na kujua mipaka hii na kuwadanganya kwHufai a kiwango kilekile cha kusema hakuna reli Wala treni ya kaliua mpanda, uwanja wa ndege kujaa maji n.k.

Wanaosema kuna makosa, waseme ni makosa gani.

JPM kanyaga twende.

Amani Msumari
Tanga
Hufai kuwa hata balozi,kiwango chako cha uelewa kidogo sana.
 
Hufai kuwa hata balozi,kiwango chako cha uelewa kidogo sana.
Ulichoandika ndio my concern. Hivi ni elimu yetu, utamaduni au nini? Au usikute naongea na watoto wa form iv humu halafu nalazimisha waelewe concept kubwa. Hupati watu wa kujenga hoja na kujifunza kutoka kwao.

Hii inanikumbusha hadithi fulani, isome hapa:

WATANZANIA WANAJIBU SWALI KWA KUULIZA SWALI

Mzungu mmoja aliambiwa kuwa ukikutana na mtanzania ukamuuliza swali, basi hakika hatakupa jibu la moja kwa moja, atakujibu kwa kukuuliza swali.

Mzungu akafunga safari kuja Tanzania ili atafute ukweli wa taarifa hiyo. Alipofika uwanja wa ndege aliamua kuanza kwa kumuuliza mhudumu;

Mzungu: Samahani dada, eti ni kweli kuwa ukimuuliza mtanzania swali yeye atakujibu kwa kukuuliza swali?

Mhudumu: Kwani wewe ni nani aliekuambia habari hiyo?

Mzungu: Naomba unikatie tiketi ya ndege inayoondoka mida hii nirudi nyumbani
 
Jambo la kwanza nililojifunza hapa ni kuwa vijana wengi wana ujuzi mdogo sana wa kimawasiliano ( very poor communication skills). Hili ni eneo la muhimu sana kulifanya kazi.
 
Back
Top Bottom