"Kufufua" Magari kunapunguza gharama?

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Mods kama mtaona vyema naomba ibaki hapa, ni mada inayojitegemea kabisa.

Naomba wataalamu wa Magari waje hapa tujadiliane jambo hili, unapo"fufua" gari unakua umeokoa gharama au umeongeza gharama? Kwa mtazamo wangu mimi unakua umeongeza ghrama kama ifuatavyo;
  • Grarama za Vipuri; Unapofufua gari hubadilishi kila kitu unabadilisha baadhi ya vipuri ambavyo vinakua vimechoka au vimeanza kuchoka; kwa maana hio ni kwamba vitu kama Brake rotors, Axle boots, Timing Belts n.k itabidi uvibadilishe kwa standard yake lakini pia unabadilisha vifaa hivi kwenye "mwili" ambao umeshazeeka, that means hata na vifaa hivi hutakawia kuvibadilisha tena, na hapa ndipo gharama ya vipuri itakapokua kubwa. Kwa mfano, kama ulizoea kwenda service ya kati ya Tzs 500,000 hadi 700,000 kwa 2015 Toyota L/C leo hii ukifufua Toyota ya 2004 usitegemee kuwa bili itakuja kama hio, lazima bili itafika milioni na kuendelea
  • Kitu cha pili ni Fuel Consumption Ratio ambapo kwa hali ya kawaida 2015 Toyota L/C Hardbody "inaweza" kuwa na ratio ya kati ya 7-9km/L (speaking from experience) ila kwa Toyota L/C iliyofufuliwa usitegemee kupata ratio hio hapo inaweza kushuka hadi 5Km/L. Maana yake ni kwamba itabidi mafuta yatumike mengi zaidi yaani gharama za uendeshaji zitakua kubwa zaidi, je tumeokoa au tumetumia?
  • Jingine ni Engine Life Quarantee, sio kweli kwamba eti kwasababu umeifanyia service basi kila kitu kitabaki vile vile hapana, engine nazo zina umri wake, kuna umri ukifika lazima kutakua na Leakage, kuna Oils nyingi utakua unatumia ile kuilisha engine, performance ya refurbished vehicle haitakua sawa na ile ya brand new vehicle, meaning kila siku itabidi ikalale kwa fundi hapo Nduvini Auto Garage, More bills!!!!
  • Hili sijiui kama huwa tunalitazama, Carbon Emission; tuko kwenye ulimwengu wa kupunguza hewa ukaa, athari zake ni nyingi na kubwa na ziko wazi, unapofufua gari, kiwango chake cha kutoa hewa ukaa kitakua juu tu ukilingaisha na gari kama ingekua moya, Refer kashfa ya magari ya VW. Kama tunaamua kuiga vitu vya nje tuige pia kwenye mambo kama haya.
  • Uhai wa Gari lililofuliwa; Tumewahi kujiuliza uhai wake unategemea kudumu kwa muda gani? Halafu baada ya hapo? Kwa mfano, kwenye International NGOs zile DFP na DFPA nyingi unazoziona mara nyingi huanza kupigwa mnada kuanzia miaka mitano hadi kumi (sio zote) kwa sababu kipindi hiki maintenance cost/running cost zinakua juu.
  • Usalama wa gari hizi huwa ni mdogo, imagine unakimbiza jambazi kwenye Defender mara break zimakataa, mara taa haziwaki, mara wiring system imezingua au unasafiri kwenda mkoani kikazi mara imechomoka sijui kitu gani huko, usalama ni mdogo sana sana.
Kwa hio kwa mtazamo wangu, tumetatua tatizo la usoni ambalo hata hivyo gharama zake hapo mbeleni huenda zikawa kubwa kubwa kubwa kuliko matarajio yetu.

Elli
 
Kwa nini tusinunue mpya chache?Magari makuu kuu ni shidaa
Kupaka rangi gari hakulifanyi liwe jipya
 
we huna akili?! ina mana nini bora kati ya kwenda hospitali kutibiwa au uache ufe uzikwe nijibu kabla sijaendelea kukuchukuli hatua za kiakilii!?!

Kumaintain gari chakavu ni gharama sana, huo ni uharibifu wa Pesa tu, hizo gharama za kufufua hayo magari angeweza kupata Eicher au TaTa mpya kabisa
 
Kumaintain gari chakavu ni gharama sana, huo ni uharibifu wa Pesa tu, hizo gharama za kufufua hayo magari angeweza kupata Eicher au TaTa mpya kabisa
Scania ya miaka 10 ni bora kuliko Tata mpya! Vinginevyo watu wengi wangenunua Tata mpya kuliko used Trucks za Scania au Benz ambazo zinazidi bei ya Tata mpya.
 
kukarabati gari ni sawa kabisa lakini sio iwe kazi ya RC tena kuhamasisha au kusimamia, jeshi la polisi lenyewe lilitakiwa likarabati magari yake manake tunajua kuna karakana za polisi kila mkoa na mapolisi ni mafundi wazuri sana wa magari sasa iweje iwe kazi ya mkubwa tena kuingia apo na kushuulikia hilo wakati ana majukumu ya kuleta maendeleo mkoani kwake
 
Yaani kwasababu anaefanya huu ukarabati anachukiwa watu wanatumia nguvu nyingi saaana kuonesha anachokifanya kina matokeo hasi.
Wapi nimetaja mtu? Wapi? Tuache hisia za kitoto, tujibu hoja kwa hoja. Nimezungumzia ukarabati wa magari Vs ununuzi wa magari mapya, wapi nimetaja kuwa namchukia mtu??
 
Scania ya miaka 10 ni bora kuliko Tata mpya! Vinginevyo watu wengi wangenunua Tata mpya kuliko used Trucks za Scania au Benz ambazo zinazidi bei ya Tata mpya.

Kaka umesikia marekebisho yanayofanywa?, nadhani umeshundwa kutoafautisha kati ya kununua used vehicle na kufufua yaliyokufa, tena yamekufa baada ya kuendeshwa na madereva Watanzania, ndani ya Barabara za Tanzania

Hapo ni Bora wangenunua Eicher au Tata Mpya, tena zinatolewa kwa mkopo
 
Mkuu huu sio mzizi wa thread hii, nazungumzia mjadala tofauti na huu
 
Sikiliza ndugu, magari mengi ya seriakli yanayoachwa yaoze sio mabovu kivile. Watu wengi walikuwa wanayaacha ili wayanunue kwa mnada. Kama uko serikalini au unajua mtu yuko huko utanielewa.
 
Kama wameshindwa kufanya hivyo mwingine asifanye?
 
Kazi ya kujenga hayo magar ni ya polisi..
Hapa naona kunalimtu linatafuta kiki..kwakigezo cha uzwazwalendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…