Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Mods kama mtaona vyema naomba ibaki hapa, ni mada inayojitegemea kabisa.
Naomba wataalamu wa Magari waje hapa tujadiliane jambo hili, unapo"fufua" gari unakua umeokoa gharama au umeongeza gharama? Kwa mtazamo wangu mimi unakua umeongeza ghrama kama ifuatavyo;
Elli
Naomba wataalamu wa Magari waje hapa tujadiliane jambo hili, unapo"fufua" gari unakua umeokoa gharama au umeongeza gharama? Kwa mtazamo wangu mimi unakua umeongeza ghrama kama ifuatavyo;
- Grarama za Vipuri; Unapofufua gari hubadilishi kila kitu unabadilisha baadhi ya vipuri ambavyo vinakua vimechoka au vimeanza kuchoka; kwa maana hio ni kwamba vitu kama Brake rotors, Axle boots, Timing Belts n.k itabidi uvibadilishe kwa standard yake lakini pia unabadilisha vifaa hivi kwenye "mwili" ambao umeshazeeka, that means hata na vifaa hivi hutakawia kuvibadilisha tena, na hapa ndipo gharama ya vipuri itakapokua kubwa. Kwa mfano, kama ulizoea kwenda service ya kati ya Tzs 500,000 hadi 700,000 kwa 2015 Toyota L/C leo hii ukifufua Toyota ya 2004 usitegemee kuwa bili itakuja kama hio, lazima bili itafika milioni na kuendelea
- Kitu cha pili ni Fuel Consumption Ratio ambapo kwa hali ya kawaida 2015 Toyota L/C Hardbody "inaweza" kuwa na ratio ya kati ya 7-9km/L (speaking from experience) ila kwa Toyota L/C iliyofufuliwa usitegemee kupata ratio hio hapo inaweza kushuka hadi 5Km/L. Maana yake ni kwamba itabidi mafuta yatumike mengi zaidi yaani gharama za uendeshaji zitakua kubwa zaidi, je tumeokoa au tumetumia?
- Jingine ni Engine Life Quarantee, sio kweli kwamba eti kwasababu umeifanyia service basi kila kitu kitabaki vile vile hapana, engine nazo zina umri wake, kuna umri ukifika lazima kutakua na Leakage, kuna Oils nyingi utakua unatumia ile kuilisha engine, performance ya refurbished vehicle haitakua sawa na ile ya brand new vehicle, meaning kila siku itabidi ikalale kwa fundi hapo Nduvini Auto Garage, More bills!!!!
- Hili sijiui kama huwa tunalitazama, Carbon Emission; tuko kwenye ulimwengu wa kupunguza hewa ukaa, athari zake ni nyingi na kubwa na ziko wazi, unapofufua gari, kiwango chake cha kutoa hewa ukaa kitakua juu tu ukilingaisha na gari kama ingekua moya, Refer kashfa ya magari ya VW. Kama tunaamua kuiga vitu vya nje tuige pia kwenye mambo kama haya.
- Uhai wa Gari lililofuliwa; Tumewahi kujiuliza uhai wake unategemea kudumu kwa muda gani? Halafu baada ya hapo? Kwa mfano, kwenye International NGOs zile DFP na DFPA nyingi unazoziona mara nyingi huanza kupigwa mnada kuanzia miaka mitano hadi kumi (sio zote) kwa sababu kipindi hiki maintenance cost/running cost zinakua juu.
- Usalama wa gari hizi huwa ni mdogo, imagine unakimbiza jambazi kwenye Defender mara break zimakataa, mara taa haziwaki, mara wiring system imezingua au unasafiri kwenda mkoani kikazi mara imechomoka sijui kitu gani huko, usalama ni mdogo sana sana.
Elli