Wakuu
Naomba Ushauri Kwa Wazoefu Waliwahi Kufuga Bata Bukini (Goose)
Ninao Wawili Jike Na Dume, Mara Ya Kwanza Alitaga Mayai Manne
Akatamia Kwa Muda Wa Kutosha Zaidi Ya Siku 21,Ila Baadaye Tukaona Haangui Vifaranga. Ikabidi Tupasue Japo Moja Tukakuta Ndani Ni Meupe
Ametaga Tena Mayai 6 Amelalia Zaidi Ya Siku 28 Lakini Shida Imetokea Ile Ile
Hakuangua Vifaranga, Je Tatizo Laweza Kuwa Nini?
Nifanyeje Aweze Kuangua Vifaranga Endapo Atataga Tena Kwa Mara Ya 3
Tafadhali Wazoefu Na Ambao Wanajua Lolote Ambalo Laweza Kuondoa Shida Niliyoisema. Banda Nimewajengea Nzuri, Sehemu Anayotagia Nimeweka Maranda Ya Mbao Chini, Pia Nimekata Drum La Litres 20 Nikajaza Maranda Vizuri
Kuhakikisha Mayai Yake Yanakuwa Vizuri