kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Iko siku hao tunaowaita machinga watakuja kulikataa hilo jina Na kudai wapewe jina lingine Na wanasiasa. Sasa hivi neno wamachinga linatumika fuko kuukuu kubwa la kuwafichia vijana wasiokuwa Na ajira, wasiokuwa Na pembejeo za kilimo, wasiokuwa na zana za kuvulia wala maeneo ya kuchungia Mifugo. Fuko ambalo wanadhani limejaa kura zao wakati wa uchaguzi.
Lakini vijana wanazidi kumiminika mitaani kutoka vijijini kuja kuungana Na wenzao waliozaliwa mijini kusaka maisha waliyoyakosa huko vijijini. Bila shaka muda sio mrefu nafasi za wazi zitaisha za kutandaza bidhaa, kuegesha bodaboda, za kuoshea magari, za kupigia kiwi, kukaangia chips mijini.
Natabiri siku sio nyingi vita kubwa ya kugombea maeneo ya wazi, kugombea abiria Na wateja itatokea ambayo itawasha moto mitaa Na mali za watu Na viongozi wa kisiasa.
Kama hatutaboresha kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, uchimbaji Na upatikanaji wa masoko Na mitaji kwa vijana tusijidanganye kwa kuwaacha wamachinga wazagae kila kona wakichafua mazingira Na kuziba njia zote za waenda kwa miguu Na mitaro Na chini ya nyaya za umeme wa msongo mkubwa.