Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Hakika tunapita katika kipindi ambacho janga kubwa la kibinadamu siyo vita wala majanga ya asili ila ni janga lisilotajwa mara kwa mara ambalo nimelipa kichwa kufugwa kwa akili ya Binadamu. Hili ni janga kubwa kuwahi kufikia hatua lilipofikia.
Mifumo mikubwa ya kidunia na kijamii (Dini, Elimu, Siasa, Teknolojia) haijikiti tena kwenye lengo la kustawisha maisha ya binadamu wengi ila imebeba maslahi binafsi ya kuhakikisha wachache wanawatawala wengine au wanawafuga wengine.
Watu wengi tumefugwa na mifumo na tumefugika hakika. Gereza la mwanadamu ni akili yake iliyofugwa na kufugika. Uhuru wa kiakili haupo katika zama hizi kwa sababu umepokwa mamlaka yake na wachache jambo linalotufanta wanadamu kuishi Duniani kama Jehanamu.
Karubu kila Mwanadamu leo anaishi katika gereza kubwa la mitazamo ya watu wengine ambao wengine kwa Hakika hawapo tena katika Dunia hii. Kuishi maisha halisi katika zama zetu ni sawa na kuishi motoni. Watu wanaumizwa na kila kitu, mioyo haitoi sauti ila imejawa na Kelele za ukimya.
Hakika Plato hakukosea katika kile kisa cha An allegory of the cave huenda pango alililogusia na kuta zake ni mifumo.