Kufulia kubaya sana

Kufulia kwa mtu mmoja mmoja ni kiashiria cha ukosefu wa mipango thabiti.

Unacho kula leo ni jasho na kazi uliyoifanya au kuitengeneza siku zilizopita.

Ili kuondokana na huu mkwamo uliokukumbe jitafakari na jiulize maswali yafuatayo.
1. Je ni nini kilicho sababisha leo ufulie?
2. Je nini unaweza kukifanya kikakuondoa kwenye mkwamo ulionao leo?.
3. Je ni kipi unaweza kufanya kuzuia mikwamo kama hii siku zijazo?

Ukipata majibu ya hayo maswali utakuwa katika sehemu nzuri ya kukuondoa kwenye mkwamo.
 
Haya mawazo tu ila mkuu unaweza pigika na shida na ulikua una fanya yote hayo ila kiasi chote ulicho kihifadhi kikaisha ...haya maisha ni kumuomba Mungu tu atuepushe na mitihani ya duniani.[emoji2972][emoji2972][emoji2972]
 
kufulia kubaya kweli ! hata uzi wako unaonekana uthaminiwi.
*Nzi watakufata njiani wakati umeoga.
*vumbi litakufata wewe hata kama sio sehemu ya vumbi.
*unaweza fungiwa laini ya simu sababu mtandao utashindwa kujua lain yako ipigiwi.
*utazeeka kabla ya umri.
*ukifa utazikwa mapema ili kuepusha usumbufu.
 
Yaani leo hata sijui siku itaishaje na sijui kesho siku itaanzaje, maisha haya yasikieni tu. Sometimes mpaka nawaza kujitumbukiza baharini tu, bora iende. Dah!
Mbaya zaidi umefulia halafu washkaji zako wapo kwenye taasisi wanapiga hela za michongo balaa, wanawekeza tu kwenye nyumba za kupangisha, unawaza wewe umemkosea nini Mungu? Luna wakati unaanza kutamani hata kazi za wenzako hahahaha, kuna muda unajikuta unatamani uimbe uwe na hela kama diamond, au ucheze mpira na umri huu wa 40s uwe kama Ronaldo, hatari sana.
 
Hapo kwenye kumkopa dada wa kazi umenikumbusha mbali mkuu.
 
Usiombe yakukute
 
Pole mkuu. Naijua hiyo feeling.
Yalisha nikuta mara kadhaa huko nyuma....lakini mara zote ilikuwa ni sababu ya uzembe wa kuweka mipango thabiti na kuiteleza.

Ila baada ya hizo changamoto nilijifu za...na nashukuru mungu kwa miaka ya hivi karibuni pamoja na ugumu wa maisha sijaadhirika.

Bado nasisitiza, kufulia ni matokeo ya kutokuwa na mipango thabiti.
 
Motivational speaker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…