KUFUNGA JAMIIFORUMS NI UPALALALAA WA KISHERIA: Why Gagging the Digital Public Square is a Monumental Failure of Public Policy

KUFUNGA JAMIIFORUMS NI UPALALALAA WA KISHERIA: Why Gagging the Digital Public Square is a Monumental Failure of Public Policy

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Inakuwaje wazee wa udhibiti? Hebu tuongee uhalisia bila kuficha makucha hapa. Hivi mnafikiria kwa kutumia akili au mmeamua tu kufuata bureaucratic reflexes ambazo hazina mashiko kwenye karne hii ya 21? Kufungia JamiiForums sio tu kwamba ni ushamba wa kidijitali, bali ni constitutional overreach na regressive move ambayo haina msaada wowote kwa taifa. Let’s dissect this nonsense kisheria na kimkakati, mfunguke akili kidogo badala ya kukurupuka na mamlaka mlizonazo.

Mnafikiri mkiweka kufuli JamiiForums ndio mmezuia watu wasiongee au wasikosoe? That is a big fat lie! Hiyo ni sawa na kuziba bomba la maji lililopasuka kwa kutumia pamba mwisho wa siku, the pressure will build up na mlipuko wake utakuwa mkubwa na wa hatari zaidi. Ukifunga platform rasmi na iliyofanyiwa moderation kama JF, unachochea watu kukimbilia encrypted networks kama Telegram na Signal au kutumia VPNs ambako hamna uwezo wa ku-monitor wala ku-regulate chochote. Ni upumbavu wa kiwango cha juu kujiondoa kwenye meza ambayo mngeweza kusikiliza maoni ya wananchi wenu (actionable intelligence) na badala yake mnajenga chuki iliyojificha na unregulated underground digital resistance.

Kisheria, hatua yenu hii inavunja kabisa misingi mikuu ya utawala bora na haki za binadamu kwa sababu JamiiForums si mali ya mtu mmoja, bali ni virtual marketplace of ideas kwa mamilioni ya Watanzania. Article 18 of the Constitution (UAT) inalinda wazi Uhuru wa Maoni na Kujieleza (Freedom of Expression), na kufunga JF ni blanket ban inayokiuka haki hii kikatiba bila sababu za msingi zinazokubalika kwenye jamii ya kidemokrasia (not reasonably justifiable in a democratic society). Zaidi ya hayo, Doctrine of Proportionality kwenye sheria za admin (Administrative Law) inataka adhabu iendane na kosa; huwezi kuua mbu kwa bomu la nyuklia! Kama kuna user amekiuka Cybercrimes Act, mshikeni huyo mtu badala ya kutoa collective punishment kwa kuzuia haki ya mamilioni ya watu, jambo ambalo ni haramu kisheria.

Huu uamuzi wenu pia unaua kabisa *the whistleblowing culture na uwajibikaji nchini kwa sababu JF imekuwa the ultimate digital watchdog kwa miaka mingi. Kashfa ngapi za kifisadi, uzembe maofisini, na uonevu wa mamlaka zimeibuliwa pale na zikasaidia hata serikali kuchukua hatua za haraka? By shutting down JF, mnasema nini kwa umma? Kwamba mnataka kulinda mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma wasiseme we? Huu ni uhujumu uchumi wa kifikra kwa sababu mnaua whistleblowing mechanism ambayo ilikuwa inawasaidia hata nyinyi kujua wapi watendaji wenu wanazingua, kana kwamba mnataka wananchi wawe zombies wasihoji chochote, jambo ambalo ni ndoto kwenye ulimwengu wa sasa.

Mwisho kabisa, mnasahau madhara makubwa ya kiuchumi (economic implications) wakati kila siku mnatupigia kelele hapa kuhusu Digital Economy na kukuza ajira kupitia teknolojia. JF si jukwaa la kupiga soga tu, pale kuna biashara, kuna watu wanapata ugali wao kupitia matangazo, na kuna digital ecosystem nzima inayotegemea hilo jukwaa kuishi. Kufungia jukwaa kama hili kunaongeza country risk assessment kwa wawekezaji wa nje (Foreign Tech Investors), kwa sababu hakuna tech-investor mwenye akili timamu atakayekuja kuwekeza kwenye nchi ambayo mamlaka ya udhibiti inaweza kukurupuka asubuhi moja na kufunga *multi-million platform kisa tu wamepata butt-hurt na maoni ya watu.

Ni kwamba kufungia JamiiForums hakutanyamazisha njaa ya watu kutaka uwajibikaji, hakutafuta umaskini, na hakutafanya hoja za wakosoaji zipotee, badala yake mnaonekana waoga na washamba mbele ya macho ya ulimwengu wa wasomi na kiteknolojia (Technological Illiterates). Kama mna hoja, njooni jukwaani mjibu kwa hoja zenye akili, sio kutumia mabavu ya vitufe vyenu vya kudhibiti kwa sababu ushandi wa hoja unapatikana kwa hoja zenye mashiko, sio kwa kuwaziba watu midomo! #BringBackJF #UhuruWaKujieleza #KizaziChaKuhoji*l
 
Ina maana gani sasa wanaifungia halafu hao hao wenyewe kila siku wamejazana humu jukwaani kujisifia/kusifiana!
 
Back
Top Bottom