Kufunga minyororo magari yanayodaiwa ushuru wa maegesho mijini ni utaratibu wa ovyo kabisa


Kweli kabisa kwenye kufunga minyororo inaudhi sana kwa sababu

1: Hakuna mazingira mazuri au maeneno ambayo wametengeneza kama maegesho wao wamebuni kukusanya tu tena hata ukifika unashusha mtu tayari wanapiga picha gari na kukuwekea deni


2: Nilishawahi wapa maoni kwanini wasiwe wanaweka risiti kuonyesha unadaiwa? Kwa nini iwe kama kuviziana? Nitajuaje nadaiwa bila kuwa na taarifa? ndiyo madhara mwisho wanakuja na minyororo kama siyo wizi ni nini?

3: Magari yote huwa yana na namba za wamiliki kwanini wasishirikiane na taasisi husika kama tra kupata namba za wamiliki ili wawe wanatuma taarifa kwenye simu zao?

4: Au waweke mfumo watu wajisajili kwenye simu ili kuwe na notification kwenye simu. Maana tunabanbikiwa sana maegesho na mawakala wao sababu wamewapa target unakuta deni hulijui au unakuta ukifatilia deni la mkoa ambao hujawahi hata kwenda na gari.

5: Masaki wanavizia ofisi za watu kama vile wamejenga parking wao nilishangaa hadi see clif hotel parking zao za nje wamejenga vizuri jamaa wakaingia na mashine zao kulipisha .Kuna kanisa moja lipo sinza tla kkkt tukiwa jumapili tunaenda sali wanakuja hata kama umepaki mbali kwenye ntymba za watu wanapiga picha namba na kuandikiwa deni.

Inaudhi sana sasa firikia haya yote juu unakuta sasa limnyororo na hapo upo na mke na watoto na pesa huna ambayo wanakudai na adhabu juu, kwanza ni kukutukanisha mbele ya familia yako na kukudhalilisha. Dawa kutembea na mkasi wa kukatia mnyororo ndiyo dawa
 
yaani ni aliyewatuma wafunge minyororo huko shule alikwenda kusomea upumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…