Kufunga Mwaka 2021: Jamii Forums na kusanyiko la watoto takribani 600 wa dini mbalimbali

Maxence Melo

JF Founder
JF Staff
Joined
Feb 10, 2006
Posts
4,324
Reaction score
13,967
Katika kufunga Mwaka 2021, Jamii Forums mnamo Desemba 30 ilidhamini kusanyiko la watoto takribani 600 wa dini mbalimbali waliokutana Magomeni jijini Dar na kula, kunywa na kucheza pamoja kwa furaha kuuaga mwaka 2021.

Kusanyiko hili liliwezekana kwa kubuniwa na kuratibiwa na Padre Christian Caristus Likoko Nyumayo ambapo watoto bila kujali tofauti zao za kiimani waliburudika pamoja.

Ilikuwa siku ya furaha kwangu na wenzangu kuweza kuwa na watoto hawa kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni.

Nilipata muda wa kuongea na Padre, Masheikh na Wachungaji walioshiriki katika kusanyiko hili. Tulikuwa familia moja, Taifa moja na ndugu kupitia watoto hawa.

Mwaka 2022 tunatarajia kuwa na watoto zaidi ya 1,500 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar.. Tuunge mkono ukiweza!

Naambatanisha baadhi ya picha:

 
Melo, nimefuta nilichotaka kuandika kwa wema tuu.

Mbadala wake.

You are blessed, more blessings to you.
 
Hili ni wazo zuri mara kumi ya wazo la kukutanisha members,mijitu mizima huishia kutamaniana tu,na kuombana namba za simu ,ukidhani kuna mpango mzuri

Kumbe anania ya kufanya mwenzie mpango wa kando.

Irudiwee hyo ...mwishon mwa mwaka.
 
I believe the children are our future

Teach them well and let them lead the way

Show them all the beauty they possess inside

Give them a sense of pride to make it easier

Let the children's laughter remind us how we used to be.

W. Houston

Safi Sana Melo
 
Hongera kiongozi.
 
Hao watoto mliwapata wapi ndugu Max?
 
Namkumbuka vizuri sana
Hivi kwa mtazamo wako tu unaona wapo sawa yule na huyu wa sasa?

mijadala yake ya hitajio la katiba mpya kipindi kile na ukosoaji wake kipindi kile kuhusu CCM na serikali yake,alafu baada ya teuzi kawa sio yuleeeee,,,wa kipindi kileeeeeee!

Achana na teuzi kasomi utaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…