Kufunga tairi za size 225/70/R16 badala ya 225/65/R16

Kufunga tairi za size 225/70/R16 badala ya 225/65/R16

kiufundi tatizo lipo.

Tairi ya 225/70/R16 itakuwa na mduara mkubwa kidogo kuliko tairi ya 225/65/R16. Hii inaweza kuathiri usahihi wa spedomita na odomita ya gari. Kwa mfano, spedomita inaweza kuonyesha kasi ya chini kuliko kasi halisi ya gari.

Mduara mkubwa wa tairi unaweza kuathiri matumizi ya mafuta kwa kiasi fulani, kwani inahitaji nguvu zaidi kuzungusha tairi kubwa, hasa wakati wa kuanza mwendo.

etc

lakin kilegend badiri tu hamna noma sana. 😱 👨‍🔬
Hapana. Herufi R, inasimama kwenye Rim, size ya mduara wa chuma linaloshika mpira. Na hilo halibadiliki. 225, 205, n.k. huo ni upana wa mpira na 45, 55, 60, 70 nk ni ujazo wa kwenda juu.
 
Wakati wote muhimu ni ile R ndio size ya Rim. Sizes nyingine zinaweza kufanya gari liwe chini au juu, na kwa upana huwa likiwa pana sana na liko mbele litagusa katika mudguard/ chassis ukikata kona.
 
Hapana. Herufi R, inasimama kwenye Rim, size yac mduara wa chuma linaloshika mpira. Na hilo halibadiliki. 225, 205, n.k. huo ni upana wa mpira na 45, 55, 60, 70 nk ni ujazo wa kwenda juu.
NOTE
  • 225: Hii ni upana wa tairi kwa mm, kutoka upande mmoja wa tairi hadi mwingine. Katika kesi hii, tairi ina upana wa 225mm.
  • 65: Hii ni uwiano wa kipenyo cha tairi (aspect ratio). Ni asilimia ya upana wa tairi inayojumuisha kipenyo chake (sidewall height). Kwa tairi hii, urefu wa upande ni 65% ya upana wa tairi, ambayo ni 225 mm. Ili kupata urefu wa upande kwa milimita, unafanya hesabu ifuatayo:
Sidewall height= [65/100]x 225 =146.25mm
  • R: Hii inaonyesha kuwa tairi ni ya muundo wa radial. Hii ndiyo aina ya kawaida ya tairi zinazotumika kwenye magari siku hizi. Radial inamaanisha kuwa nyuzi za tairi[tire's cords] zinaenea kutoka katikati ya tairi (hub) kuelekea nje katika angle ya 90° kule gar linpoelekea.
  • 16: Hii ni kipenyo cha rim kwa inchi ambazo tairi inafaa. Kwa hiyo, tairi hii imeundwa ili kufaa kwenye rim yenye kipenyo cha inchi 16.
 
Maelezo yako ni ya kitaalamu mno kwa mtu wa kawaida kukuelewa. Upo sawa tu.
 
Back
Top Bottom