Kufungiwa kwa Viwanja vya soka vya Zanzibar liwe funzo kwa TFF na vilabu vya Tanganyika

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa kutoka Zanzibar imeeleza kwamba Shirikisho la Soka la Nchi hiyo limezuia matumizi ya Viwanja vya soka vya New Aman Complex na Gombani kwa kile kinachoitwa kupisha matengenezo.

Uwanja wa Aman umezinduliwa hivi karibuni ukiwa umekamilika, Sasa leo tunaambiwa unafungwa ili kupisha Matengenezo!

Lakini taarifa zingine zinaeleza kwamba, Jambo hilo limefanyika ili kukomesha Upuuzi wa Timu za Tanganyika kuutumia uwanja huo kwa masilahi ya kisiasa yenye lengo la kufifisha ligi ya Zanzibar inayosimamiwa na ZFF.

Nachukua nafasi hii kuipongeza ZFF kwa kulinda Rasilimali za Nchi yao na kuondoa Mamluki waliotaka kuzitumia kisiasa.

Jambo hili liwe funzo kwa Watanganyika, Watambue kwamba si kila Nchi ni Shamba la Bibi kama ilivyo Nchi yao.

Mungu Ibariki Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
 
sidhani kama ulichoandika unakijua!
 
Amani stadium ni kiwanja kinacho chezewa Ligi mara kwa mara na kime idhinishwa na CAF kwa mashindano ya kimataifa.
Unguja upo uwanja mwingine wa kuchezea Ligi wa Mao.

Ni vizuri kiwanja Cha Amani kikarabatiwe kwakua Upo uwezekano mkubwa Yanga ikapeleka baadhi ya mechi za CAF Champion league zikachezwa pale.
 
Taarifa kutoka Zanzibar imeeleza kwamba Shirikisho la Soka la Nchi hiyo limezuia matumizi ya Viwanja vya soka vya New Aman Complex na Gombani kwa kile kinachoitwa kupisha matengenezo.

Uwanja wa Aman umezinduliwa hivi karibuni ukiwa umekamilika, Sasa leo tunaambiwa unafungwa ili kupisha Matengenezo!

Lakini taarifa zingine zinaeleza kwamba, Jambo hilo limefanyika ili kukomesha Upuuzi wa Timu za Tanganyika kuutumia uwanja huo kwa masilahi ya kisiasa yenye lengo la kufifisha ligi ya Zanzibar inayosimamiwa na ZFF.

Nachukua nafasi hii kuipongeza ZFF kwa kulinda Rasilimali za Nchi yao na kuondoa Mamluki waliotaka kuzitumia kisiasa.

Jambo hili liwe funzo kwa Watanganyika, Watambue kwamba si kila Nchi ni Shamba la Bibi kama ilivyo Nchi yao.

Mungu Ibariki Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Tayari nyuma mwiko wanataka kuchimbia ugagula wao humo uwanjani tetesi ya jambo hilo tunayo
 
Kwa jjnsi Wazanzibar walivyo na misimamo hasa linapokuja suala la Watanganyika, inawezekana kweli
 
Back
Top Bottom