Mabibi na mabwana heshima kwenu.
Mgombea wa Chadema alifungiwa kukampeni kwa wiki moja kwa makosa ambayo si yeye, chama chake wala wafuasi wake ambao yameweza kuwaingia akilini. Hukumu ya namna hii ina tija gani?
Pana hisia na mwonekano wa wazi kuwa ka uonevu fulani kalipita. Ni kwa sababu kama hizo CDM walisema watasajili malalamiko yao mahakamani kwa kumbukumbu stahiki.
Wapongezwe mgombea yule, Chadema kama chama na wafuasi wao kwa kuamua kupisha shari kwa ile style ya funika kombe badala ya ile ya kata funua.
Siku 7 ndiyo hizo zinayoyoma sasa na tunaelekea kurejea tena majukwaani.
Kama hakuna somo lolote tutakalokuwa tumejifunza sisi sote ikiwamo tume basi aliyeturoga tutatakuwa hatunaye hapa duniani. Kama hali ni hivyo ni suala la muda tu (just a matter of time).
Mtuhumiwa wa tume (na haswa wa yule daktari) katika kipindi hiki cha siku 7 ameendelea kuwa kivutio cha wengi kote alikopita akiwa bila ya ulinzi wowote wa polisi.
Polisi walijaribu kumzuia kwenda mlandizi. Haieleweki ilikuwa kwa manufaa yapi au maelekezo ya nani? Au hata kwa sababu gani?
Mgombea huyu hata baada ya kuzuiliwa kwa saa takribani 8 kiluvya aliporuhusiwa kuendelea, bado amani na utilivu pasipokuwa na polisi vili endelea kutamalaki. Akaenda mlandizi salama, akafanya kilichompeleka kule salama na kurejea salama.
Ni vivyo hivyo kwa mabomu yaliyoshuhudiwa tarime na hata kule ifakara. Ya kiluvya, tarime na ifakara yameonyesha wazi kuwa mleta fujo ni polisi.
Ya kumzuia mgombea kukampeni kulinganisha na mapokezi ya wananchi kwa mgombea huyo nayo yanawanyooshea kidole tume kuwa pana kitu hakiko sawa.
Tume, polisi na mamlaka zote zingatieni sheria zenu ambazo wenyewe ndiyo mmeziweka ili kutodhulumu haki za wengine.
Sheria mpya haziwezi kuongezwa katikati ya mechi. Ni vyema mkajua, wananchi mliowanyima haki zao za kumsikia mgombea wao wakampima wenyewe, hawawezi kuwa na maneno matamu sana kuwahusu nyie.
Enyi tume, itakuwa haiwafikirishi kweli kuwa mnaungwa mkono na chama kimoja ambacho ndicho mnachotuhumiwa kukibeba?
Halahala kabla ya hatari. Wananchi wamevumilia tarime, ifakara, kiluvya na hata sintofahamu hii kumsimamisha mgombea wao kukampeni. Kwa maamuzi na hatua fyongo kama hizi, basi tunakokwenda haihitaji nabii kung'amua kuwa pana hatari mbele yetu inayotujongelea.
Tendeni haki, vinginevyo si muda mrefu kutoka sasa patakuwa na watu ambao wala si wachache watakaotaa hii buruzwa buruzwa isiyokuwa na kichwa wala miguu.
Maendeleo hayana chama!
Ninawasilisha.