KUFUNGIWA REDIO IMAAN NA NYINGINEZO: haki haijatendwa!

KUFUNGIWA REDIO IMAAN NA NYINGINEZO: haki haijatendwa!

RADIO Imaan, elimu bila mipaka huu msemo sii sahii lazima elimu iwe na mipaka huwezi fundisha mambo ya ndoa radioni kama wanavyofanya, unamfundisha nani?? IFUNGWE.. IFUNGWE. ELIMU LAZIMA IWE NA MIPAKA

kazi ipo kwelikweli! kumfundisha mtu namna ya kumtafuta mke / mume bora, kuvumiliana ktk ndoa nk.... ni vibaya!? kwa hiyo ifungiwe kwa hilo!? kuwa muadilifu ndugu yangu
 
muandishi anaonyesha kuwa biased. Honestly mi mwenyewe naona kama redio iman ingefungiwa zaman kwa kuchochea mgawano wa kiimani, na kuwafanya waislam waone kama wanakandamizwa hence udini. tukiachana na hayo maana sheria haikuona kama ni kosa mi naona ni sawa kuwafungia wote neema kwa uchochezi ambayo kisheria ni kosa, na imani kukiuka au kufanya watu wakiuke maagizo ya serikali( kugomea sensa nalo ni kosa).

Ila hili swala ukiread btwn the line..........................
 
kuna ubaya wowote kuzungumzia mfumo uwe wa kiislamu au kikristo? mtu kusema anaonewa ni kosa!? waislamu walichunguza na kuona kuwa baraza la mitihani lilifelisha watoto wa kiislamu makusudi katika mtihani wa islamic knowledge. baraza lilikiri na kusema lilikua kosa la kompyuta. pana madai kuwa katika bodi ya NECTA na wana kamati hakuna muislamu hata mmoja. redio ya kiislamu kuongelea suala hilo ni majungu / kosa!?

kwa nini kwa mwanasiasa kuchunguza jambo ni sahihi lakini kwa redio ya dini kuchunguza tatizo linalo athiri dini husika kwa hoja kwa liwe kosa?

naomba unijibu kuhusu madai yaliyotolewa dhidi ya baraza la mitihani. je madai haya yanahatarisha amani?

Dont miss the bigger picture!!!

Kuzungumzia chochote si kosa lakini nimesema hapo, kuzungumza kusikokuwa na mipaka ni uendawazimu!! Kama umoja wa kitaifa na co-existence ndio bigger picture, kitu chochote kingine ni secondary!! Na huu ndio msingi wa hukumu ya TCRA!!

Je ni waislamu wote wanakubaliana na msimamo na maudhui ya Radio Imani?? Au ni wakristu wote wanakubaliana na maudhui ya Radio Neema?? Bila shaka ni HAPANA!! Sasa inakuwaje kituo cha redio kitoe dhana kwa kusingizia dini zao?? Si kila yanayosemwa katika redio hizi yanawasilisha misimamo ya madhehebu/dini zao!!!!!

Jijengee uwezo wa kuchanganua umuhimu wa mambo! Si kila jambo linahitaji kushughulikiwa sawasawa, kwa njia moja, kwa nguvu moja!!
 
hapa hamna sababu ya kuumiza kichwa, hizi redi mbili zimefungiwa ili kuleta balance tu hamna kingine, mimi ninaamini kuwa hawa TCRA, hawajawahi kuona kosa la redio IMAAN,(sio kwamba hawana makosa ya kupotosha hasa habari za baba wa taifa) ndo maana hawakuwahi kuionya huko nyuma juu ya makosa yake, lengo hapa lilikuwa kufungia redio ya kwa-neema ila walijua pasingetosha kwani watu wote wanajua kampeni za redio imaan. sishangai wala sibishi kufungiwa redio kwa-neema kwani sijawahi hata kuisikia- .........ila nashangaa kwanini redio imaan ilichelewa kufungiwa hivyo?

tukubali tukatae huu ni mwendelezo wa yale mambo yetu ya kufanya mambo sio kwa sheria na taratibu bali kwa kuofia dini.

viongozi -tunabalance dini
vyuoni hatutaki kuangalia uwezo -tunataka ku-balance dini
hata magerzani nako tunataka kubalance dini - taifa kama limelAANIWA VILE
Fungia vyombo vya habari vinavyotishia mwenendo wa taifa aah usifungie kwanza subiri mpaka apate mwenzake kwenye dini nyingine----tuna-balance dini
magazeti ya dini (tena kuna moja limefanya yaleyale ya redio imaan)--ila bado subiri subiri mpaka lipate mwenzake kwenye dini nyingine ili tubalance dini

ni ujinga -ujinga kila siku.
 
Ndugu yangu scramble , kwa kuwa unakubali kwamba nchi hii inaendeshwa na inabidi iendeshwe kwa mujibu wa sheria, Walio hukumiwa wote wamepewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 30. Tunategemea watatumia haki yao hiyo kama wakidhani wame dhulumiwa.Lakini kwa maoni yangu kama ikitumika hoja ya;" kwa nini fulani yeye akapewa adhabu hii na mimi nikapewa hii au ile !" na chombo kimojawapo miongoni mwa vilivyoadhibiwa, sidhani kama itakuwa na nguvu.Suala ni kueleza kwamba ni kwa vipi muhusika hakuvunja sheria.
 
Last edited by a moderator:
Radio hii ilikuwa inachochea migomo ya wanafunzi wa kiislam kule Mtwara ikawa ndo toipic kila kukucha ikahamasisha waislam kusafiri kwenda mtwara kuwaunga mkono wanafunzi waliogoma wakitaka misikiti ijengwe mashuleni kama ilivyo makanisa yaliyojengwa tangu enzi zamani shule zikiwa za misheni kabla kutaifishwa na serikali na mengine mengi kila kukicha inaongelea chuki kwa wakristo badala ya maendeleo na mafundisho mema katika dini.
 
Hata kabla ya sensa, wamekuwa wakilinganisha idadi ya watumishi waliopo kwenye taasisi za serikali kuwa hapa pana waisilamu wachache kuliko wakristu. Sasa huo ni uchochezi kwamba kuna mtu au watu walikuwa wanatoa ajira kwa upendeleo, jambo ambalo ukweli wake ni kwamba ajira zinatolewa kwa qualifications alizonazo mtu.[/Q hii redio imefaulu kupanda mbegu ya chuki miongoni mwa wtz adhabu iliyotolewa haitoshi

ha ha ha ati watu wanaajiriwa kutokana na qualification zao, tangu lini?
Hii kitu inaitwa merit is no more kwenye ajira. Its about who you know ie mambo ya mjomba mjomba, chama chama etc.
 
ha ha ha ati watu wanaajiriwa kutokana na qualification zao, tangu lini?
Hii kitu inaitwa merit is no more kwenye ajira. Its about who you know ie mambo ya mjomba mjomba, chama chama etc.
Officially zinazotakiwa ni qualifications, hayo mambo ya mjomba mjomba hayatakiwi na ukiyagundua unatakiwa uyaripoti, sio kulalamika baada ya mtu kupewa ajira!
 
Tumo katika nchi inayofuata sheria. nchi yoyote ile lazima iongozwe kwa kufuata sheria. TCRA ni chombo kinacho simamia vyombo vya habari vya kielektroniki hasa redio na televisheni. kina mamlaka ya kuonya au hata kufungia chombo cha habari kinacho kiuka maadili ya utangazaji.

redio imaan ya morogoro na kwa neema fm ya mwanza zimefungiwa na kamati ya maudhui (content committee) iliyo chini ya TCRA. clouds fm ya dsm imeonywa na kutozwa faini ya 5,000,000/=. sababu iliyo tolewa ya kuifungia redio imaan ni kuhamasisha waislamu wasishiriki katika sensa ya mwezi agosti mwaka jana. kuhusu kwa neema fm imeelezwa kuwa imehamasiha kwa zaidi ya miezi 4 wakristo wasile nyama iliyochinjwa na waislamu hadi uhamasishaji wao ukasababisha watu kuuana!. clouds fm inasemekana walicheza clip ya askofu wa marekani aliekua akiunga mkono ushoga. watangazaji waliiunga mkono kauli yake na kusema kuwa mashoga waruhusiwe. ni haki yao.

lengo lango ni kuizungumzia redio imaan huku nikiakisi redio nyingine mbili. ni takriban miezi 7 tangu sensa ya watu ifanyike. kwa mujibu wa bbc jana jioni, mkurugenzi wa redio imaan alipohojiwa alisema kuwa redio yake ilikua ikiripoti maoni ya watu kuhusu kipengele cha dini kuwekwa kwenye dodosa za sensa. alisema kuwa japo kila mtu ana uhuru wa kuisikiliza redio imaan lkn imewalenga sana waislamu. waislamu ndiyo wenye redio na michango yao ndiyo inaifanya redio iwepo. alisema kuwa waislamu walijenga hoja kuwa wanabaguliwa katika mambo mengi hasa ajira serikalini kwa madai kuwa ni wachache. wao wanaamini ni wengi. walitaka kwenye dodosa kiwekwe kipengele cha dini ili ukweli ujulikane kama zifanyavyo nchi nyingine. alisema kuwa mada ilianzishwa na watu wakawa wanapiga simu kuchangia mada hiyo.

aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi 7 iliyopita, hajawahi kupokea barua kutoka TCRA ikimuonya kuhusu mada ya sensa! inakuaje afungiwe ghafla bila hata karipio!? alisema vipindi vya redio imaan vimekua vikiendeshwa kwa ueledi na kwa kuzingatia taaluma ya utangazaji. redio imaan haijawahi kuhamasisha mtafaruku, kuhatarisha amani na kusababisha vifo vya raia. imekua daima ikieleza na kuripoti ukweli kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia hapa nchini.

MY TAKE:
ukiangalia kosa la kwa neema fm, utagundua kuwa uhamasishaji ulikua wa wazi na hadi ulikaidi amri ya serikali ya kuomba uchinjaji uendelee huku suluhu ikitafutwa. redio ilipuuzia agizo la serikali na kuendelea na uhamasishaji bila ya kuangalia madhara yake. matokeo yake watu wakauana! inakuaje clouds fm inayo shabikia ushoga ipewe karipio na kutozwa faini lakini redio imaan inafungiwa! watu kudai haki ya kutambuliwa katika dodosa za sensa na wanaohamasisha ushoga ni yupi anaekiuka maadili na katiba ya nchi?

kazi kwenu wadau kutoa majibu yenye hoja zilizo kwenda shule!

naomba kuwasilisha!
Mkuu Kwanza nomba wafanyakazi wote wa redio Iman mrudi shule, bora hata mkasome certificate ya uandishi wa habari, utangazaji wenu unaonyesha nikiasi gani mmemaliza digrii za madrasa tu, na izo madrasa mmesoma kwa kiarabu na mwalimu alikua hawambii maana, saa nyingine mnaongea pumba mpaka aibu, nyie mmesomea kupandikiza chuki.

Ombi langu kwa serikali, hiyo redio ifungiwe kabisa make hamna faida katika jamii, mimi muislamu lakini ninawachukia kabisaa, bora nisikilize wapo fm kuliko nyie mnaotangaza kutumia masabuli
 
kila mtu ana haki ya kuabudu. Amna mwenye haki ya kumzuia mwengine kufanya ibada ikiwa anafata kitabu cha imaan yake

Unazungumza kama umetoka usingizini. Jisumbue akili yako kidogo na utafahamu haya:

a) Zipo sehemu nyingi dunia hii zinakubali dini moja tu - Pakistan, Afghanistan na Somalia, Georgia!!
b) Zipo nchi kadhaa ambazo haziruhusu nyumba za ibada za dini nyingine - Saudi Arabia, Somalia, Afghanistan, Somalia, Georgia!!

Ikiwa matakwa yetu ya kuabudu yatazuia wengine kuishi wanavotaka - maana yake hakuna "co-existence", hakuna kuvumiliana. Hata hivo vitabu vya imani unavovisema, havizuii wanaovifuata kuishi na wengine. Ninachoka kusikia "justifications" za mawazo ya makundi kadhaa ya watu kupitia vitabu ya dini!!

Mimi mkristu, sijaambiwa nisiishi na mtu wa dini nyingine. Ninafunzwa kuwavumilia wengine, na hata wale walio katika dini yangu!!
 
Radio
hii ilikuwa inachochea migomo ya wanafunzi wa kiislam kule Mtwara ikawa
ndo toipic kila kukucha ikahamasisha waislam kusafiri kwenda mtwara
kuwaunga mkono wanafunzi waliogoma wakitaka misikiti ijengwe mashuleni
kama ilivyo makanisa yaliyojengwa tangu enzi zamani shule zikiwa za
misheni kabla kutaifishwa na serikali na mengine mengi kila kukicha
inaongelea chuki kwa wakristo badala ya maendeleo na mafundisho mema
katika dini.

ivi TCRA hawakuona hayo unayosema hadi kuja na hoja ya sensa? Tafakari
 
kila mtu ana haki ya kuabudu. Amna mwenye haki ya kumzuia mwengine kufanya ibada ikiwa anafata kitabu cha imaan yake

Nadhani inabidi tufahamu kuwa demokrasia isiyo na mipaka si demokrasia hata vyombo vya habari japo kuna uhuru wa vyombo vya habari lakini lazima kuwe na mipaka isifike sehemu tukaacha vyombo vya habari vikaharibu amani ya nchi yetu kwa kisingizio cha uhuru wa vyombo vya habari la hasha lazima kuwe na mipaka kama chombo cha habari kinurusha habari ambazo zinaweza kuleta uchochezi au kuvunjika kwa amani ya nchi lazima vizibitiwe na si vinginevyo
 
kuna ubaya wowote kuzungumzia mfumo uwe wa kiislamu au kikristo? mtu kusema anaonewa ni kosa!? waislamu walichunguza na kuona kuwa baraza la mitihani lilifelisha watoto wa kiislamu makusudi katika mtihani wa islamic knowledge. baraza lilikiri na kusema lilikua kosa la kompyuta. pana madai kuwa katika bodi ya NECTA na wana kamati hakuna muislamu hata mmoja. redio ya kiislamu kuongelea suala hilo ni majungu / kosa!?

kwa nini kwa mwanasiasa kuchunguza jambo ni sahihi lakini kwa redio ya dini kuchunguza tatizo linalo athiri dini husika kwa hoja kwa liwe kosa?

naomba unijibu kuhusu madai yaliyotolewa dhidi ya baraza la mitihani. je madai haya yanahatarisha amani?

Ndugu zangu waisilamu acheni lawama zisizo na msingi pelekeni watoto wenu shule. Makanisa yana vyuo vikuu vingi nyie mnavyo vingapi? Angalia matokeo ya form IV mwaka huu, katika shule 10 bora kuna ngapi za kiisilamui? Kwa khali hiyo hata kama ungefanya interview leo ukawa fair katika watu 10 wanao qualify uwezekano mkubwa wa kukuta 7 ni wakristu ni mkubwa. Pamoja na hayo Mbona Raisi, makamu wake, IGP, Mkurugenzi wa usalama wa taifa, commissioner general wa TRA ni waisalamu lakini wakristu hawalalamiki?
 
Hapo naona umeitetea redio Imani tu. Kimsingi ilitakiwa iwe imefungiwa hata kabla ya mambo ya sensa hayajaanza kuwa public

nachofurah itarud hewan mwezi wa 8 mwezi ambao zoez la sensa lilifanyika.na naamin itarud kwa kasi zaid.
REDIO IMAAN,ELIM BILA MIPAKA
 
Ndugu zangu waisilamu acheni lawama zisizo na msingi pelekeni watoto wenu shule. Makanisa yana vyuo vikuu vingi nyie mnavyo vingapi? Angalia matokeo ya form IV mwaka huu, katika shule 10 bora kuna ngapi za kiisilamui? Kwa khali hiyo hata kama ungefanya interview leo ukawa fair katika watu 10 wanao qualify uwezekano mkubwa wa kukuta 7 ni wakristu ni mkubwa. Pamoja na hayo Mbona Raisi, makamu wake, IGP, Mkurugenzi wa usalama wa taifa, commissioner general wa TRA ni waisalamu lakini wakristu hawalalamiki?

Wewe muislamu wa wa kanisa gani? Acha udini, changia hoja.

Wewe ulisoma wapi na elimu yako imekusaidia nini mpaka sasa?
 
Mkuu Kwanza nomba wafanyakazi wote wa redio Iman mrudi shule, bora hata mkasome certificate ya uandishi wa habari, utangazaji wenu unaonyesha nikiasi gani mmemaliza digrii za madrasa tu, na izo madrasa mmesoma kwa kiarabu na mwalimu alikua hawambii maana, saa nyingine mnaongea pumba mpaka aibu, nyie mmesomea kupandikiza chuki.

Ombi langu kwa serikali, hiyo redio ifungiwe kabisa make hamna faida katika jamii, mimi muislamu lakini ninawachukia kabisaa, bora nisikilize wapo fm kuliko nyie mnaotangaza kutumia masabuli

inaelekea hujawahi kuisikiliza hiyo redio. mimi siyo mfanyakazi wa redio imaan. nimeleta mada hii kwa sababu leo redio imaan kesho zitakua redio nyingine. hoja yangu ni kwamba kuwe na sababu zenye mantiki za kukifungia chombo cha habari. leo hii watu wanalalamika kuhusu gazeti la mwanahalisi..........

umewahi kuisikiliza redio imaan? una uhakika kuwa mimi ni muislamu? jenga hoja acha ushabiki wa kijiweni
 
Ndugu zangu waisilamu acheni lawama zisizo na msingi pelekeni watoto wenu shule. Makanisa yana vyuo vikuu vingi nyie mnavyo vingapi? Angalia matokeo ya form IV mwaka huu, katika shule 10 bora kuna ngapi za kiisilamui? Kwa khali hiyo hata kama ungefanya interview leo ukawa fair katika watu 10 wanao qualify uwezekano mkubwa wa kukuta 7 ni wakristu ni mkubwa. Pamoja na hayo Mbona Raisi, makamu wake, IGP, Mkurugenzi wa usalama wa taifa, commissioner general wa TRA ni waisalamu lakini wakristu hawalalamiki?
ndo umeshachangia hapa,HUYO RAIS SI MMEMCHAGUA WENYWE,KWANI HAKUKUA NA MGOMBEA MKRISTO TENA MKATOLIKI
 
Ndugu zangu waisilamu acheni lawama zisizo na msingi pelekeni watoto wenu shule. Makanisa yana vyuo vikuu vingi nyie mnavyo vingapi? Angalia matokeo ya form IV mwaka huu, katika shule 10 bora kuna ngapi za kiisilamui? Kwa khali hiyo hata kama ungefanya interview leo ukawa fair katika watu 10 wanao qualify uwezekano mkubwa wa kukuta 7 ni wakristu ni mkubwa. Pamoja na hayo Mbona Raisi, makamu wake, IGP, Mkurugenzi wa usalama wa taifa, commissioner general wa TRA ni waisalamu lakini wakristu hawalalamiki?

mbona unaacha mada husika!? unaonesha jinsi ulivyo dhaifu! ustutoe kwenye mada iliyopo ya kuifungia redio imaan
 
Back
Top Bottom