KUFUNGIWA REDIO IMAAN NA NYINGINEZO: haki haijatendwa!


Nashauri post zetu zizingatie udugu na amani tuliyo kuwa nayo kwa muda mrefu, tusitoe comments kwa chuki au hisia binafsi. Swala la kuifungia radio Iiman kwaajili ya sensa haliingii akilini, labda kama kuna sababu nyingine chini ya kapeti. Serikali ilitangaza swala la sensa kufanikiwa kwa asilimia mia (100%), zaidi ya hivyo; baadhi ya vipindi vya radio iiman vilikuwa vikichallenge takwimu zilizo tolewa kabla ya sensa hazikuwa sahihi na waislamu tukatoa mapendekezo yetu ya kuwepo kepengele cha dini katika dodoso la sensa ambazo kitafuta fikri na hisia mbaya zilizojengwa kutokana na takwili zilizotolewa awali na hazikukemewa na Serikali yetu, ukimya ambao mavuno yake ndio haya yote.


Ushauri wangu kwa wana JF na Serikali kwa ujumla; tunapotaka kutafuta sulhu katika jambo, tuzingatie chanzo cha tatizo na tusihukumu kwa kupima athari za tatizo, as according to my knowlege; we will always be wrong.

By knowing the source, we shall know course and by knowing the the course, we shall find the easy way to solve.

I don't support judgement basing on effects!
 

napenda kujua maoni yako kuhusu kufungiwa gazeti la mwanahalisi. unasemaje?
 


We ndugu wewe, computer huwa inakosea hata kuendesha ndege, inaanguka na kuua watu, sembuse baraza la mitihni kukosea kusahihisha Quran! Suala la baraza kuwa na mwislam ni dalili za wendawazimu ulipitiliza. Nani amekwambia kuwa akiwemo mwislam ndiyo mtapata akili ya kufaulu?
Wekezeni kwenye elimu ya ukweli. Elimu Dunia. Mkiweza hilo nina hakika hamtahitaji kuandamana popote kuwa mnaonewa. Kiukweli hakuna mtu anawaonea popote, ila mnajionea wenyewe. Hamsomi au kupeleka watoto shule zenye akili. Angalieni Waslamu wenzenu wa Turkey. Wako mbali sana na hivi sasa wanatetemesha soko la electrical and electronic items la Ulaya na Marekani. Hawa walikumbuka kuwekeza. Ukitua Instabul ukaingia mtaani unaweza usiamini kuwa siyo nchi ya Kiislamu. Totos ziko bwedebwede mitaani na min-skirts, Bar za kumwaga na life ya kileo kila kona. Hawa wenyewe Quran yao iliandikwa na nani ambaye alisahau kuweka kipengere cha kuwa wanaonewa!?

Amkeni ndugu zangu Waislamu wa Tanzania. Mtapiga kelele kuwa mko wengi na inaweza kuwa kweli. Lakini kuna umuhimu gani kuwa wengi na wengi wenu wajinga?
 
napenda kujua maoni yako kuhusu kufungiwa gazeti la mwanahalisi. unasemaje?

Hili Gazeti lilikuwa ni chai yangu ya asubuhi!! Ni gazeti pekee lililoweza kuweka bayaha hali na mustakabali wa nchi yetu likiwa na data kamili. Ni mwiba kwa mafisadi na wezi wote wa mali za umma. Halikuwahi kusemea udini hata siku moja tena ukizingatia Saed Kubenea ni mwislam. Kwa mantiki hii walianza kumhujumu mhusika Kubenea na timu yake na mwisho kabisa wakaamua kulifungia jumla kitu ambacho si sahihi!!! Lingekuwa linahubiri udini hasa uislam mmmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhh labda lingekula ban ya muda tu!!! But kwa kuwa lilikuwa linafukua uonzo basi life ban. Wewe unaonaje????
 
Japo umeegemea upande mmoja kuitetea radio imani lakini naona kuna tatizo TCRA hasa kushughulikia matatizo katika uendeshaji wa vituo vya habari!

Kwa makosa yaliyo ikuta radio imani ni wazi kuwa walitakiwa kuwapa barua ya onyo kuhusu hili swala na ukizingatia hili swala lilitendeka muda mrefu!

Lakini lazima ukumbuke kuna makosa yakifanyika haya hitaji onyo. Huwa ni adhabu papo kwa papo!
 

adhabu ya tukio la miezi 7 iliyopita ndiyo ya papo kwa papo!?
 

mwanahalisi lilikua linafukua uozo pamoja na ufisadi. unajua maana ya uozo? unajua maana ya ufisadi? hudhani kuwa redio imaan inapofukua ukanda au udini katika sekta za uma nayo unafaa kuiunga mkono? vyote ni vyombo vya habari. kwa nini uunge mkono mwanahalisi lkn usiunge mkono redio imaan! ? vyote vinasema ukweli. kwa mfano chombo cha taifa kama necta kutokua na muislamu katika bodi ya utendaji hata mmoja! madai ya wanafunzi waislamu kufelishwa nk..... mambo yote haya ndiyo uozo na ufisadi. kwa mwanahalisi poa kwa redio iman hapana!? au kwa sababu ya neno NI REDIO YA WAISLAMU!?

acheni hizo ndugu zanguni. nchi hii ni ya wote!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 


inaelekea uturuki ulienda kweli kwenye starehe. tunazungumzia kufungia chombo cha habari wewe unaleta mambo ya elimu!? tumia kichwa na akili kufikiri. acha uvivu wa fikra. ondoa bongo lala kichwani. sijazungumzia uislamu. nimezungumzia baadhi ya hoja zilizotolewa na redio imaan
 

Mbona hata Radio Neema FM imefungiwa na sijaitetea mkuu Scramble? Hapa ninamaaisha kuwa sitaki mambo ya udini kabisa ndani ya kichwa changu. Nataka niheshimu tu ile dini yangu basi na si kuanza kuhubiri udini. Yaani kila kitu nitupe jicho la udini? Hapana?? Kama hiyo kamati haina waislam waliochagua wana sababu zao!!! Si siamini kuwa kwa kuwa watakuwa ni wakristu basi watakuja na sababau za kutetea ukristu? Wanafunzi wamefeli wote, wakristo na waislam kwa pamoja. Ni janga la wote na suluhu itakuwa kwa wote. Ayway, sipendi mabishano ya dini ngoja niishie hapa kwa leo. Asante.
 

Ila pia Scramble hebu jaribu kutumia busara kujibu post hata kama imekugusa!! Just use polite and palatable language tu. Isije ikapelekea tena watu waanze kujiuliza maswali kuwa wewe ni wa hivi au vile. All the best.
 
hivi hao watoto mnaosema wamefelishwa, huku mnawafundisha mambo ya ndoa.. kwa ufahamu wenu mnafikiri watashika lipi?
 
Sijasema hivyo bali nime maanisha kuna adhabu haziitaji kuandikiwa barua na siku maanisha kwenye hili la radio imani!
Kama umeni soma vizuri utagundua nimepinga maamuzi haya ya tcra maana ni wazi kwa kosa hili walitakiwa kutoa barua ya onyo, kinyume na hapo adhabu ilitakiwa hitoke baada ya kosa kutokea na siyo kipindi hiki!

Na hili ndilo kosa kubwa la tcra, wana tatizo kubwa kwenye maamuzi na hapo na pata mashaka!



adhabu ya tukio la miezi 7 iliyopita ndiyo ya papo kwa papo!?
 
Naona mtoa mada anahaha kuitetea Radio yao kinafki tu, kana kwamba hajui kilichokuwa kinafanywa na Radio Iman.
Nakubaliana na wadau kuwa TCRA kuifungia Radio Iman kwa kosa la Sensa ni hatua iliyochelewa sana, lakn wanaINTELIJENSIA nao wanasema kuifungia mapema kipind kilekile ingeweza kusababisha fujo na utengano wa kidin nchin kwasababu ya presha kubwa waliojazwa waislam kupitia Radio hii wakiwemo akina Shekh Ponda. Kwahyo ukitafakar utaona pana ukwel kias.

Pamoja na hayo, Em mtoa mada tuthibitishie ni kwa kias gan Radio hii, mada zake zimewasaidia waislam nchin, kama sio kuchochea, kujaza chuk, pamoja na kudhalilisha ukristo.!?

Kwa kifup tu kama unatafuta sababu zaid kuhusu kufungiwa kwa radio hii, sababu zote zipo hapa JF, Kwan hii ndo Radio iliyoanzishiwa Thread nying za kuzipinga mada na mijadala yao, kwahyo ipitie ile mijadala yote utapata jibu, kwan hata mimi naamin TCRA hawajatumia kigezo hicho kimoja, bali na yale tuliyokuwa tukiyajadil hapa.
 

Sasa hapo kwenye red, radio imani ilikubali agizo la serikali kuhamasisha watu wote washiriki sensa? Hebu tumia kichwa kufikiri.
 

Kwa kweli wewe ni kichaa kabisa. Unaongeleaje radio iman bila kutaja uislam?! Hoja zipi huwa wanatoa zaidi ya hiyo fikra yako finyu ya udini? Na lile suala la kutokuwa na mwislam hata mmoja baraza la mitihani ulilozungumzia hapo juu linahusiana vipi na radio imani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…