Kufungiwa viwanja vya mpira Tanzania

Kufungiwa viwanja vya mpira Tanzania

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
TFF imeendelea kuvifungia viwanja ambavyo havina sifa mfano: Al Hassn Mwinyi, Kirumba na Jamhuri Dodoma.

Nashauri tena, viwanja vya CCM virudishwe serikalini, vikarabatiwe na visimamiwe na halmashauri vilipo viwanja ili kukuza soka na kuwasahaulisha Watanzania.

Kuna kipindi serikali ilisema imetenga bajeti ya kukarabati viwanja lakini mpaka sasa bila bila.

Viwanja hivi vikiwa chini ya halmashauri, angalau meneja wa uwanja atakuwa na hofu ya kuogopa uwanja wake kufungiwa tofauti na sasa viwanja vya CCM wanapiga hela bila hata mechi kwa sababu nje ya hivyo viwanja wamepangisha fremu za maduka na mastoo, hivyo hawajali ukarabati wa pichi na miundombinu mingine.

Kwa mfano, vikisimamiwa na halmashuri, zile kodi za mechi, pango za maduka na stoo zitaingia serikalini na kurudishwa kuhumia kiwanja. Pale kutakuwa na wafanyakazi ambao kazi yao kila siku ni kukiangalia kiwanja. Kwa mfano, wanaweza kuchimba visima katika viwanja kwa ajili ya umwagiliaji au kuweka nyasi bandia.

Mnajua kabisa mkiwekeza katika soka, Watanzania tunasahau shida zetu, lakini bado mnachezea tena sekta ya michezo.
 
Magufuli pekee ndiye angeweza kufanya hilo. Hawa wengine hawataki kugusana mikono wakiwa wanakula.
 
Magufuli pekee ndiye angeweza kufanya hilo. Hawa wengine hawataki kugusana mikono wakiwa wanakula.
Hahaha! Wanashangaza sana. Ukipita nje ya kiwanja fremu za maduka zimejaa. Hawa wote wanalipa pango, lakini wanashindwa kuhudumia kiwanja.
 
Back
Top Bottom