Kufungua BIASHARA kwa Kutegemea RESEARCH za Madalali, Uwezekano wa Kufeli ni zaidi ya 75%

Kufungua BIASHARA kwa Kutegemea RESEARCH za Madalali, Uwezekano wa Kufeli ni zaidi ya 75%

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Katika pitapita na harakati za hapa na pale huku nikitafiti vitu vidogovidogo nimona mfano wa kitu ambacho ni vizuri Tushiriki katika kujadili na kubadilishana maarifa.

Mzee mwenye mvi na mke wake kaletwa na madalali mtaa mmoja unaovutia kibiashara. Nasema unavutia kwa Sababu ya Wingi wa wapita njia, na wafanyabiashara.

Baada dalali kujua anafungua Mgahawa akaanza kumpamba, wote hawa watakuwa wateja wako, Hata hawa watoto wa chekechea utakuwa unawauzia wewe uji ukiwahi asubuhi (Bila kujua watoto hao wanautaratibu wao hapohapo shuleni kwao). Hao jamaa walioka kaa hapo (kuna kijiwe flani member zake wengi wamechomekeachomekea inaonekana wako vizuri)

Kwa mvuto wa eneo, bila kujua uhalisia akajikuta analipia Kodi 100,000 kwa mwezi huku aliyekimbia hapo baada ya kushindwa biashara yake alikuwa analipa 60,000 (Hii ilikuwa ni sherehe kwa madalali).

Siku ya kwanza ikafika, Kwa unafiki wa majirani wakaenda kujinunulisha ili kumkaribisha mtaani, baada ya hapo kila siku wananunua watu wawili au mmoja tu. Akiwa amekwisha panga majeshi yake anagundua amezungukwa na wauza misosi wenzake ambao pumzi zimekaribia kukata kutokana na ukata wa wateja wa kuaminika.

Baada ya hali kuwa mbaya. Akajipa siku tatu za mapumziko ili akatunge sheria. Aliporudi kwa bashasha akiwa tayari kwa lolote, akapata wateja kadhaa akadhani hali inaelekea kuzuri. Kesho yake akaandaa msosi wa kufa mtu lkn Hakuja mtu hata mmoja, hata wa kuomba maji ya kunywa. Mama kachanganyikiwa hajui afanye nini, akiiangalia kesho yake anaona giza.


FUNZO:

1Dalali ni mtu anayeangalia percent yake sio biashara na malengo yako. Usiamini kila anachokisema.

2:Utafiti wa kibiashara Ufanywe na Mwenyewe, kabla ya kuingiza miguu yote miwili.

3:Hakuna kukata tamaa, hata kama Mambo uliyotarajia hayajatokea. Mfano wa jamaa aliyemleta Mtoto wake Aponywe na yesu na akakosa pa kupitia maana mlangoni palikwa na watu. Yule jamaa hakulialia alipanda juu ya bati, likatobolewa mgonjwa akashushwa na kamba palepale alipokuwepo Yesu na akaponywa.(Luka 5:17-39)


Karibu kwa maoni yako, funzo ulilojifunza, na ushauri au uzoefu wako katika hali kama hizo...
 
Back
Top Bottom