Kichochoro
JF-Expert Member
- Jul 18, 2017
- 1,135
- 1,167
Faida kubwa ya kampuni ni kuwa katika wigo wa kufanya kazi na entities ( mashirika , serikali au makampuni)
Serikali , mashirika au makampuni hayafanyi kazi na mtu binafsi Bali Kampuni. Unaweza kuwa unaweza kufanya usafi lakini mwenzako mwenye kampuni ya kufanya usafi ndio akawa anapata tenda za kufanya usafi kwenye hayo maeneo.
Kwahyo faida kubwa ya kampuni ni wewe kuwa katika wigo mpana wa kufanya kazi zenye hela kubwa.
Kuhusu kufungua kampuni ingia Brela usajili kila kitu kipo mrandaoni. Kuhusu mtaji wa kampuni ni uwezo wako tu hata 200,000.
Kwa Tanzania ili kampuni iwe kampuni inabidi uwe na vifuatavyo
1. Incorporation Certificate ( Brela )
2. company TIN number Certificate
3. VAT certificate
4. Bussiness license ya Kitu unachotaka kufanya ( Kufanya usafi , Kuuza bidhaa n.k )....
5. EFD mashine ...
6. BANK ACCOUNT
Ukiwa na haya mavitu hii ndio kampuni. Mambo mengine ni kujuana mbele kwa mbele ...
NB : Issue sio kuwa na kampuni , issue uwe na sababu kwanini unakuwa na kampun. Naomba usome hii point utaelewa namaanisha nini. Maana Kama hujui unachofanya utabaki kukimbizana na TRA kwenye kulipa income TAX wakati biashara hazieleweki.
Kwa mfano deal Kama hizi huwez kuzipata bila kampuni...Umeongea point sana cha muhimu ni kuwa smart kwenye documentation na kulipa tra na documentation otherwise hukimbizani na mtu.
We umeshafungua?Mhh! Natamani 60% wawe na kampuni zao!..kifup kutokuwa na kampuni ni umasikini ulotopea!
Unapishana na millions of money inauma Sana!
Mkuu haina gharama kihivyo!
Fanya Sasa!
Sijafungua...We umeshafungua?
Ooh okaySijafungua...
Vipi?Ooh okay
NothingVipi?
We unayo?Nothing
Kuna videals vya ajabu ajabu lakini km huna kampuni ndo ntolee!😔Kuishi mpaka unazeeka karne hii bila kumiliki kakampuni inabidi ushtakiwe aisee.
Sina etiWe unayo?
Safi!Sina eti
Aisee tenda.Kuna videals vya ajabu ajabu lakini km huna kampuni ndo ntolee!😔
Umeshauri vizuri.Kuna faida nyingi za kuwa na kampuni kama walivyogusia wengine...mimi niongezee hizi;
1. Limited Liability.
Kampuni ina ukomo wa kuwajibika kwa wanahisa wake...linamkinga member wa kampuni na mali zake binafsi zisitumike kufidia madeni ya kampuni isipokuwa ktk kiwango cha hisa ambazo nember wa kampuni hajazilipia.
Mfano kama member ana hisa 50 na alilipia hisa 30 tu, ikitokea kampuni inavunjwa na kuna madeni, huyu member atalipa thamani ya hisa 20 tu ambazo hajazilipia...wala mali zake hazitatumika kufidia madeni ya kampuni.
Kampuni inamiliki mali zake yenyewe, inashitakiwa au kushitaki yenyewe na si members. Kampuni ni mtu kisheria anayejitegemea. Kampuni na wanahisa/members si kitu kimoja.
2. Going concern.
Kampuni inaweza ku survive miaka mingi, ikarithishwa vizazi na vizazi...hata founders wa kampuni wakifa, bado kampuni itaendelea kuwepo....ila mifumo mingine ya ufanyaji kazi ina disadvantage fulani...mmiliki wa biashara binafsi akifa na biashara imekufa. Kwenye ubia, akifa mbia mmoja, basi partnership nayo imekufa. Cocacola na Pepsi, Ford, n.k ni kampuni zenye umri wa zaidi ya miaka 100.